Fahamu historia ya Diamond Platnumz juu ya maisha na muziki wake

Kidingi

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
1,872
1,832
Ukitaka kujua kuwa ku-shine hapa Bongo ni juhudi zako tu mwenyewe za kupiga kazi usiku na mchana,bila kulala na mwisho wa siku kufikia malengo yako basi mfano wa kuigwa ni huyu Birthday boy Diamond Platnumz.

Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam mnamo wa saa kumi na moja na kupewa jina la Nasibu Abdul Juma . Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote na ikabidi wahamie Tandale Magharibi kwa bibi yake mzaa mama, na hapo ndipo yakawa makazi yao.Historia yake ni ya kusikitisha kama alivyoelezea kwenye wimbo wa binadamu wabaya.

Mnamo mwaka 1995 alianza kupata elimu ya Nursery katika shule ya Chakula Bora iliyopo Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu ya Msingi yaani (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi Tandale magharibi iliyopo jijin Dar-es-salaam.

Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kucopy baadhi ya na kukrem nyimbo za wasanii waliokuwa wakihit ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehem tofautitofauti.

Mara nyingi mama yake alikuwa akimnunulia kanda za album za wasanii tofauti waliokuwa wakihit kipindi hicho na hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, na wakati mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofautitofauti ya tallent show ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya kumuhimiza kimasomo.

Kiukweli hali ya maisha yao ilikuwa ni ngumu saana, maana mama Diamond hakuwa hana source ya kumuingizia kipato, hivyo ilibidi atumie kias kidogo anachokipata toka kwa kodi ya vyumba viwili alivyopewa na Mama yake yaani bibi yake diamond na vibiashara vyake vidogovidogo vya mikopo kwa kumsomeshea na kumlea diamond, hakika hali yao ya Kimaisha ilikuwa ni ngumu sana, hivyo iliwaradhimu wote kuhamia katika chumba cha bibi huyo ili kupangisha vyumba vile viwili alivyopewa mama diamond.

Baada ya kuhitimu shule ya Msingi mwaka 2002 na kutaka kuanza masomo ya Secondary mwaka 2003 mama yake alimwambia aachane na Muziki kabisa na azingatie na Masomo ili aweze kupata elimu itayomsaidia hata kwa muziki wake baadae kwa maana asingeweza kushika vitu viwili kwa pamoja muda huo.

Akiwa secondary diamond aliendelea kufanya muziki kisirisiri bila mama yake kujua na kufikia mwaka 2004 taratibu akaanza kujifunza kuandika nyimbo zake mwenyewe. Baada ya kuhitimu elimu yake ya Secondary mwaka 2006 mwaka 2007 alijikita rasmi katkia sughuri za muziki ili kujaribu kutimiza ndoto zake.

Kiukweli haikuwa ni safari rahisi kama alivyotegemea hadi kupelekea time kuanza kutafuta vibarua toafauti tofauti ili mradi aweze kupata riziki na kuepuka hali ya kushinda nyumbani, ikiwemo kuuza mitumba, petrol station, kupiga picha, kupigisha simu, kazi za viwandani hata wakati mwingine kuingia kwenye makundi ya kucheza kamali za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia studio kurecord lakini bila kufanikiwa, kiukweli ulikuwa ni wakati mgumu sana hadi ikamradhimu kuuza pete ya Dhahabu ambayo alipewa na mama yake mzazi aivae na kumdanganya kuwa ameipoteza na ndipo hapo alipofanikiwa kuingia studio kurecord nyimbo ya kwanza iitwayo toka mwanzo.

Kutokana na kutokuwa na mazoea ya kurecord hakuweza kutengeneza nyimbo ambayo ni hit lakini wimbo ule ulianza kumpa conections tofauti tofauti maana wengi walishangazwa jinsi alivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kuweza kutengeneza wimbo kama mtu ambae ni mzoefu, hivyo iliwafanya kuamini kuwa akipata nafasi ya kurecord mara kadhaa angeweza kufanya kitu kikubwa.

Wimbo ule ulimfanya aweze kukutana na Chizo mapene ambae alijitolea kumsimamia, na kweli wakaanza kurecord album lakini bahati mbaya wakiwa katikati ya kurekodi album hiyo anayemsaidia alipata matatizo ya kifedha na hakuweza tena kumsaidia hivyo ilimbidi Diamond aanze tena upya kuzunguka katika studio tofauti kuomba kusigniwa kwenye record label lakini kote hakuweza kufanikiwa, wote walimwambia bado kuimba hajui na kuto kutaka kumsikiliza kabisa.

Kiukweli kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana hata yule mpenzi wake ambae alikuwa nae alimuacha kwakua alikuwa ameshachoshwa na ndoto hewa ambazo alikuwa akiziota kila siku diamond kuwa ipo siku atafanikiwa kimuziki na kuwa mwanamuziki mkubwa na wao kuish maisha mazuri, kitu ambacho kilimchanganya na kumuumiza sana diamond hususan kwa kauli aliyomuambia ya "skiza Diamond mi kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana maslahi kwangu" kutwa ilikuwa ikimpitia kwenye kichwa na kujiona kama mwenye mikosi.

Mwaka 2009, Diamond alikutana na Bwana Msafiri Peter maarufu kama Papaa Misifa ambae alikubali kumsaidia kimuziki na Kurecord wimbo wa kwanza ulioenda kwa jina la "Nenda kamwambie", wimbo ambao Diamond aliimba kwa uchungu huku akimuimbia mpenzi wake huyo aliyemuacha (Sarah Sadiki) kuelezea kiasi gani aliumia kwa yeye kumuacha kwake, na hapo ndipo taratiibu nyota yake ikaanza kung'aa na wimbo huo kukua siku hadi siku.Maisha yake yakabadilika na Diamond kuweza kununua gari aina ya Toyota Celica.

Tarehe 14/02/2010 Diamond aliachia album yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo 10 ambazo ni kamwambie , Mbagala , Nitarejea , Nalia na mengi , Binadamu , Nakupa , Usisahau , Uko tayari , Wakunesanesa , Toka mwanzo na Jisachi.

Mnamo tarehe 04 mwezi wa 4 mwaka 2010 , Diamond aliandika record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tunzo tatu za Tanzania Kili Music Awards kwa pamoja ambazo ni: Msanii bora Chipukizi, Wimbo bora wa Mwaka (KAMWAMBIE) na Wimbo bora wa R&B(KAMWAMBIE), tunzo ambazo zilimfanya achaguliwe kuwa balozi wa Malaria nchini Tanzania.

Baada ya kuachia wimbo wake wa pili unaoitwa Mbagala, Diamond alichaguliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete kuwa Entertainer katika tour nzima ya Kampeni yake.

Tarehe 02 mwezi wa 10 mwaka 2010 alipata tour ya kwanza kwenda England mjini LONDON,MILTON KEYNES, na COVENTRY. Baada ya kuachia wimbo wake wa tatu mwaka 2011 , Diamond alishinda tuzo ya Nzumari Award nchini Kenya akiwa kama Msanii bora wa Kiume toka Tanzania.

Diamond alirelease nyimbo yake ya nne na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza na pekee kujaza Club Maisha hadi watu kushindwa kuingia na hata wengine kuzimia baada kutokupata hewa ya kutosha kutokna na wingi ujaaji huo.

Mwaka mpya wa 2012, tarehe 1 mwezi wa kwanza mwaka 2012 , Diamond Platnumz aliachia album yake ya pili na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuuza zaidi ya 1200,000 ulbum Copies. Mwanzoni mwa mwaka 2012 Diamond aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show ya Corparate iliyoitwa " Diamons are forever" iliyofanyika Mlimani City kwa kiinglio cha shilingi elf hamsini 50,000 za kitanzania akiwa pekeake na show kuwa sold ot kwa zaidi ya ticket 1,500.

Mnamo mwezi wa tano mwaka 2012 , Diamond Platnumz aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza kufanya show na kujaza zaidi ya watu 10'000 kwa kiingilio cha 20,000 katika kiwanja cha Darlive huku akishuka na Helicopter kwenye Stage.

Mwaka huohuo Diamond alifanya ziara yake ya Europe ikiwemo Italy, Holland,Sweden , Greece na kumalizia ziara yake ya arabuni. nchini Masqat Oman.

Mwishoni mwa mwaka 2012 ulikua mzuri kwa Diamond Platnumz kwani aliweza kuachia nyimbo mbili kwa mpigo za "Nataka kulewa " na "Kesho " zilizoambata na video zake.Mwezi wa kumi na mbili mwaka 2012 diamond alitajwa kuwa ni msanii wa kwanza anaelipwa Pesa nyingi kwenye Show toka Tanzania Mwanzoni mwa mwaka 2013 , Diamond Platnumz alichaguliwa na Cocacola kuwa Brand Ambassador wa Kinywaji Cha Cocacola, na kufuatiwa na ziara yake ya East Africa na ikiwemo Burundi , Congo na Kenya n.k. na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza East Africa kuweza kupiga show pekeake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000.

Mnamo June 2013 Diamond alishinda tuzo mbili za Tanzania Kili Music Award akiwa kama Msanii bora wa kiume Bongoflavour na Msanii bora wa kiume kwa wanamziki wote Tanzania Mwezi wa saba mwaka 2013 , Diamond alirelease next single yake iliyokwenda kwa jina la Number One ambayo aliifanyia Video Capetown South Africa Chini ya kampuni ya Ogopa Videos na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza kulaunch video bila kiingilio katika Hotel ya SERENA na kuwaalika CEO's , mameneja na viongozi toka sehemu tofauti tofauti.

Katika launching hiyo akamzawadia Gari moja ya Malegend wakubwa katika mziki wa Tanzania , Marehemu Mwidini Gurumo. mwezi 10 mwaka 2013 , Diamond aliifanya Collabo na msanii toka Nigeria Davido ya ngoma ya Number one kama Remix na kisha kwenda nchini Nigeria kwajili ya kusomea Markert ya West Africa na kushoot video ya wimbo huo ulio shootiwa na Kampuni ya Capital Dreams iliyo chini ya Director Clarence Peter.

Nyimbo hii ilimtambulisha Diamond Platnumz nchini Nigeria na barani Africa kiujumla na kumuwezesha kupata nominations mbalimbali kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo , MTV MAMA awards ambayo aliperform nyimbo hii live na Davido, BET Awards na tuzo zinazotegemea kufanyika za AFRIMAMA , MTV Europe , Channel O awards na awards nyingine kutoka nchi mbalimbali.

Tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 2014 , wakati Diamond akisherekea Birthday ya mama yake alimzawadia mama yake gari pamoja na kuachia video mbili za mdogomdogo aliyoifanyia nchini Uingereza na BumBum aliyomshirikisha Iyanya kutoka Nigeria aliifanyia Afrika Kusini. Video hizi kwa pamoja zilimgarimu Diamond dola 78,000 za kimarekani.
 
Kiukweli.. Kila kitu kiukweli!.. Wasanii badilikeni na hili neno.( kiukweli)


I hate this word!
 
Na yule DJ wake na ndugu yake aliyekua anafanya clouds anasema yeye ndiye aliyempa connection na watu wa clouds na akawa anasimamia mwenyewe kuhakikisha kamwambie inapigwa ktk kila kipindi na kuingizwa top ten. Hapo ndipo alipotokea domo hizo nyingine ni mbwembwe tu. Mnalazimisha domo aonekane ni kiumbe wa ajabu aliyepitia mateso wakati aliishi na mama na bibi alikua na nyumba mjini. Stori za kutengeneza hizo wenye akili zetu tunazipotezea tu!!
 
Dah hii historia ingetengenezewa movie ingekua bonge la movie!

Na kwenye hiyo muvi awataje wote waliomsaidia na kumuonyesha njia kama huyu!! Kiburi si maungwana
 

Attachments

  • IMG_8895909971717.jpeg
    IMG_8895909971717.jpeg
    36.6 KB · Views: 1,168
Na yule DJ wake na ndugu yake aliyekua anafanya clouds anasema yeye ndiye aliyempa connection na watu wa clouds na akawa anasimamia mwenyewe kuhakikisha kamwambie inapigwa ktk kila kipindi na kuingizwa top ten. Hapo ndipo alipotokea domo hizo nyingine ni mbwembwe tu. Mnalazimisha domo aonekane ni kiumbe wa ajabu aliyepitia mateso wakati aliishi na mama na bibi alikua na nyumba mjini. Stori za kutengeneza hizo wenye akili zetu tunazipotezea tu!!

Mkuu kwani wewe Chibu unamkubali au haumkubali?
 
Na yule DJ wake na ndugu yake aliyekua anafanya clouds anasema yeye ndiye aliyempa connection na watu wa clouds na akawa anasimamia mwenyewe kuhakikisha kamwambie inapigwa ktk kila kipindi na kuingizwa top ten. Hapo ndipo alipotokea domo hizo nyingine ni mbwembwe tu. Mnalazimisha domo aonekane ni kiumbe wa ajabu aliyepitia mateso wakati aliishi na mama na bibi alikua na nyumba mjini. Stori za kutengeneza hizo wenye akili zetu tunazipotezea tu!!

IPO hivi, diamond baada ya kutoka vizuri na kamwambie na kumsaidia kupata tuzo 3, akatoa Mbagala na juu yake akatoa shavu kwa brother ake Romyjonnes awe model wa ile video. sijui hats kama uliiona au unaropoka tu!!!!.
Then after rommy akapata ka umaarufu flani hivi, ndipo alipoenda kufanyiwa dili clouds apate ishu yoyote ya kufanya, na kwa wakati huo hakuwa akifahamu uDJ ndipo alipoanza kujifuza akiwa hukohuko Clouds...

So uelewe tu, Diamond alikuwa mwanamuziki mwenye air time ya kutosha tu kwa kipindi hicho
 
Na kwenye hiyo muvi awataje wote waliomsaidia na kumuonyesha njia kama huyu!! Kiburi si maungwana

Wewe kumbe umekuja na yako kubali husikubali maidha hayo ameyapitia

Haya kaa chini na unayetaka jysikia bio yake akwambie uje uandike

Kupiga picha, kujuana na watu, ili na kike mwisho wa siku Diamond ni mmoja wala hayupo katika kikundi cha kuimba usisahau hilo.
 
Hyo histori yenu ina mapungufu makubwa mno..

Nadhani huko kaburini Marehemu NGWAIR na GEEZ MABOVU watakuwa wanasikitikita kusahaulika kwenye historia ya diamond..
 
Back
Top Bottom