Airtel TIMIZA Riba yao inafikia hadi 24%

DISPLEI

Member
Oct 17, 2012
72
46
Kuna huduma ya Airtel inaitwa TIMIZA ambapo unaweza kopa hadi TZS 500,000 na kutakiwa kurejesha ndani ya siku 21

Tatizo ni Riba yao inafikia hadi 24% kwa muda huo. Hata kama ni mkopo husio na dhamana riba hiyo kwa muda huo ni kuubwa mno.

Utaratibu wa M-POWER ambao nao ukuaji wa kiwango cha kukopa ni taratibu sana ila wao muda wa kurejesha wa siku 30 kwa 9% unaonekana kumaanisha nia yao ya kutoa huduma.

Walaji hapa inabidi watetezi wetu waliangalie vinginevyo TIMIZA ni kichaka! pamoja na kwamba kutumia au kutotumia huduma ni ihali ya mtu!.
 
Ila kweli hili swala hata mm nimeliona, nafikiri hawa Airtel hawana dhamira ya kutoa msaada bali kunyonya wale wote wenye uhitaji. Nadhani wanatumia kauli ya UKUTAKA CHUKUA USIPOTAKA ACHA.
 
Ila kweli hili swala hata mm nimeliona, nafikiri hawa Airtel hawana dhamira ya kutoa msaada bali kunyonya wale wote wenye uhitaji. Nadhani wanatumia kauli ya UKUTAKA CHUKUA USIPOTAKA ACHA.
Hakuna mkopo wowote unaotolewa na taasisi yoyote ya kifaida ukawa na malengo yakumkomboa huyo aitwaye maskini/mnyonge...

Ni faida tu tu ndio inatafutwa tu
 
hivi ukishindwa kulipa inakuwaje!?
Ukishindwa kulipa utapelekwa kwenye CREDIT REFERENCE BUREAU kutumia usajiri wako ulipokuwa unapata namba hiyo.

Ila kama ukiendelea kitumia nr hiyo hela yoyote utakayotumiwa kwenye namba wanakata chao kwanza.

Penalty ya kuchelewa kulipa ni 10% ya kiasi ambapo hakijalipwa.
 
Hivi riba yao upande wa Akiba ikoje?
I mean kama ukihifadhi pesa zao kwenye akaunti ya Airatel timiza Akiba labda kiasi cha milioni moja kwa mwezi wanatoa riba (Bonus) kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilishawahi kukopa TIMIZA na laini yao nilivunjavunja kama nyumba za Kimara
Hili sasa ndio jibu kwa nini riba ipo juu.

Wasilianeni kwanza ninyi kwa ninyi raia muwe Waungwana na riba itashuka.

Riski ipo juu sana huo ndio ukweli.

Ila ombi langu kwao ni muda wa kulipa unatutesa sana, wafanye mwezi mzima.

Au basi waweke kiwango ambacho Mtu akifikia, labda kakopa kwa miaka miwili au mitatu alegezewe masharti ya muda wa mkopo, riba n.k.
 
Mimi nilianzia hii mikopo M pesa miaka kadhaa iliyopita, baadae nikahamia na TIMIZA.

Timiza nimeshafika 500,000, Mpesa nipo 35,000, na ni almost mwaka wa nne au tano sasa.

Nikiwauliza M pesa kulikoni kiwango hakipandi wanasema Wabongo sio kabisa, yaani wanavyopigwa mpaka wanakatishwa tamaa.
 
Timiza wapo vyema tatizo ni riba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom