Airtel nao wafanya yao tena

Airtel nao wafanya yao tena

Uwiiiiiii niende wapi mimi jamani?
Hao Hallotel si waanze kuuza line watu tuhamie huko?
Hawa watu wa mitandao wanataka kutufanya shamba la bibi,tufanye mabadiliko kotekote Watanzania.

Hata halotel watakuwa chini ya TCRA, so lazima wasikilize big boys wanasemaje.

Usitegemee makubwa sana mkuu.

Wajanja wachache wanaitumia TCRA kujinufaisha.
 
Zantel badala ya kupunguza wao wameongeza, raha sana.
Yaani 7mins, 100sms mitandao yote na 25mb kwa shs 300 tu japo inaisha saa 11:59 usiku, lakini wapo juu hawa wa Zanzibar Telecom.
 
habari zenu,

sijajua nafasi ya tcra ni ipi ktk kumlinda mlaji. Naona makampuni ya simu yanafanya yatakavyo.

Airtel hatimaye na wao kifurushi cha 500 cha yatosha sasa sio cha masaa 24. Kama una dk zako zimebakia ikifika saa sita usiku, zinapukutika.

Pia nilikuwa na dk kadhaa za yatosha ya 500 ambazo nilikuwa na carry forward kama sizitumii zote ila naona sasa hamna ku carry forward maana dk zangu zote nazo wamekwapua licha ya kutop up ndani ya muda.

Huu ni ukiritimba uliovuka mipaka, juzi juzi voda nao wefinya mb mpaka 1, haipendezi kabisa. Na hawa jamaa huwa wanafanya mabadiliko kwa kuambiana, tujiandae na tigo nao watabadili kitu si muda mrefu.

hii ni offa. Usilazimishe ndio iwe bei. Bei zinajulikana. Tofaitisha kati ya promotion na bei halali. Sasa tcra wawalazimishe airtel wakupe offa kama utakavyo? Hizo ni akili za wanao jiita ukawa.
 
Uwiiiiiii niende wapi mimi jamani?
Hao Hallotel si waanze kuuza line watu tuhamie huko?
Hawa watu wa mitandao wanataka kutufanya shamba la bibi,tufanye mabadiliko kotekote Watanzania.

Kazi za wahindi unazijua poleni sana ndugu zangu jamani. That's pure imperialism business, kuna watu wanafaidika sna hapo usione tuu watu wa mamlaka husika wamekaa kimya. Tanzania nzima tatizo ni UONGOZI Tuu hakuna kingine.
 
hii ni offa. Usilazimishe ndio iwe bei. Bei zinajulikana. Tofaitisha kati ya promotion na bei halali. Sasa tcra wawalazimishe airtel wakupe offa kama utakavyo? Hizo ni akili za wanao jiita ukawa.

vipi?
mbona umekuja spidi hivi? unafanya kazi airtel nini? haiya ebu niambie basi bei halali ni ipi, na kama ilikuwa promotion walikutangangazia wewe peke yako? watoto wa kishua mna matatizo sana.
 
Habari zenu,

Sijajua nafasi ya TCRA ni ipi ktk kumlinda mlaji. Naona makampuni ya simu yanafanya yatakavyo.

Airtel hatimaye na wao kifurushi cha 500 cha yatosha sasa SIO CHA MASAA 24. Kama una dk zako zimebakia ikifika saa sita usiku, ZINAPUKUTIKA.

Pia nilikuwa na dk kadhaa za yatosha ya 500 ambazo nilikuwa na carry forward kama sizitumii zote ila naona sasa HAMNA ku carry forward maana dk zangu zote nazo wamekwapua licha ya kutop up ndani ya muda.

Huu ni ukiritimba uliovuka mipaka, juzi juzi voda nao wefinya MB mpaka 1, HAIPENDEZI KABISA. Na hawa jamaa huwa wanafanya mabadiliko kwa kuambiana, Tujiandae na Tigo nao watabadili kitu si muda mrefu.

Kama movement ya kwanza ya kutoka MB60 hadi 8-10MB walifanikiwa lazima waje na movement ingine. Huu ni wizi wa mchana kweupe na wizi huu una Baraka zote za Serikali.

Hata January Makamba alichimba sana mkwara-mbuzi kipindi kile lakini leo kaufyata PENGINE baada ya kulainishwa. Watu ni opportunist kila wapatapo nafasi, sababu tu Watanzania tumekua waoga wa kufanya maamuzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom