masatujr1985
JF-Expert Member
- Oct 27, 2011
- 1,980
- 780
Kwanza nitoe pongezi kwa serikali kufufua shirika hili la Ndege la Taifa.
Baada ya pongezi, nieleze masikitiko juu ya utaratibu mbovu wa uahirishaji wa muda wa safari za abiria bila kutoa taarifa.
Abiria wanaosafiri kutoka Mwanza, baadhi wanatoka mikoa ya jirani kama Mara, Simiyu, na Shinyanga. Wengi hulazimika kutafuta malazi hapo Mwanza ili kuwahi safari hasa za asubuhi. Ajabu ni kuwa Shirika bila kujali usumbufu na gharama wanazoingia abiria wake, linaahirisha muda wa safari mfano kwa leo toka saa 3 asubuhi kwenda saa 7 mchana. Mtu aliyejihimu saa 12 anafika airport na kukuta mabadiliko haya, anapata usumbufu mkubwa sana. Wengine wana wagonjwa, watoto wadogo na hata wengine wanawahi katika shughuli zao mbalimbali.
Nadhani ni busara, kwa ustawi wa Shirika, basi inapotokea kuna mabadiliko ya safari, wateja wataarifiwe. Hii ishanitokea sasa mara ya pili na mara zote nimeingia gharama zisizo za lazima sababu ya kukosekana kwa taarifa.
Air Tanzania tafadhalini sana, hii kero tunayokutana nayo abiria wenu inatupatia shida sana. Tuondoleeni kero hii na boresheni kitengo cha mawasiliano maana kila mteja mna mawasiliano yake.
Lingine ambalo ni la maboresho nadhani Lugha inayoanza kutumika kwenye system nashauri tuanze na Kiswahili kisha ndiyo Kiingereza na Kichina vifuatie.
Mungu Ibariki Tanzania