Black_Mambazo
New Member
- Sep 30, 2021
- 4
- 3
Kwa kifupi:
Air Tz Mwanza hawatambui boarding pass za mtandaoni, wanakulazimisha upange tena foleni ya kaunta hata kama hauna mizigo.
Full:
Juzi nilikuwa nasafiri kutoka Mwanza na Air Tanzania. Usiku kabla ya safari nilitembelea tovuti ya ndege nika 'check in' kwa mtandao ili kuepuka kadhia ya kusubiri kwenye foleni ya kaunta siku ya safari.
Kesho yake, nikiwa na boarding pass kwenye simu, nilifika Mwanza Airport na kwakuwa sikuwa na mizigo isipokuwq begi la mgongoni nilivuka foleni nilioikuta kwenye kaunta ya ATCL na kwenda moja moja kwenye security check halafu eneo la kusubiria abiria.
Cha kushangazq ulipofika muda wa kupanda ndege mfanyakazi aliekuwa ana kagua boarding pass za abiria akanizuia kupanda eti kwasababu sina boarding pass ya karatasi. Jitihada za kujitetea kwangu na kumwonyesha boarding pass ya kidigital hazikuzaa matunda akanilazimisha nirudi tena nje kwenye kaunta yao ni check in tena wanitolee pass ya karatasi.
Nilipata boarding pass nyingine na seat ya katikati tofauti na ile niliochagua jana, ya pembeni. System ilikuwa haina rekodi kwamba kuna abiria alisha check in kupitia mtandao.
Kwa kifupi, utawala wa ATCL au Mwanza Airport, tafadhalini tatueni kero hii.