Aina za wasukuma na kisukuma

Hovyo kabisa, kama hujui kaa kimya
Shida ni pale mnaojua mnapokaa kimya lazima wasiojua waje kuongea ila ukweli nimekaa na wasukuma mwaka wa 3 sasa katikati yao mnyantuzu ni wa kuwa makini nae baadhi yao sio watu wazuri kabisa wanathamini mali kuliko utu ila wana mabinti wazuri sana na sio wachoyo
 
Uko sawa sana lakini sehemu moja tu uliposema kwamba bila msukuma wa bariadi kutapakaa nchini pengine kabila hili lisingejulikana.hii hapana.wasukuma tupo wengi sana sana,na wote tumetapakaa nchini mpka nje ya mipaka kama Zambia Malawi na Msumbiji tukitafuta malisho ya mifugo.tunajulikana nchini kwa sababu moja tu kubwa kwamba tupo wengi sana.kumbuka kwa sasa tunamiliki mikoa mitano,na hii isichukuliwe kua ni majivuno la hasha..ni hali halisi,karibuni Mwanza,Tabora,Shinyanga,Geita na Simiyu.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Gawiza...!!

Lugha ya kisukuma ina lahaja kuu nne; ginantuzu, ginang'weli, ginangw'agala na gidakama. Vivyo hivyo, Wasukuma wamegawanyika katika misingi ya lahaja za lugha ya kisukuma.

1.Bhadakama. Hawa wanapatikana sehemu za mji wa Shinyanga, sehemu za Gahama na sehemu za Igunga na Nzega. Kwa idadi, hawa ndiyo Wasukuma wachache sana. Ni watu wenye aibu, wakimya mno... wana muingiliano na utamaduni wa Wanyamwezi. Pengine hawa ndiyo Wasukuma masikini kuliko aina yoyote ya Wasukuma!

2. Bhanang'weli.
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa mikoa ya Mwanza, Geita, na kusini - Magharibi mwa Mkoa wa SIMIYU. Kiidadi, hawa ndiyo Wasukuma wengi sana... katika ongea yao, wana matumizi mengi ya 'shi' kwa mfano, shikolo, shiliwa. Pia hawatumii 'ng'wadila' katika salamu za jioni. Wao hutumia 'gawiza' au 'dillo gawiza' Kwa sababu wanaishi katika strategic areas, wana muingiliano na watu wa makabila mbalimbali. Au tuseme wamemezwa na watu wa kuja. Ukienda Geita wenyeji hawaonekani, labda kukimbiza daladala za baiskeli. Mwanza ndiyo usiseme kabisa.

3. Bhanang'wagalla.
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa Wilaya za Meatu, Kishapu na Maswa na sehemu za Igunga. Ukikutana nao ni rahisi mno kuwasikia wakisema, 'yombaga bhahebhu', ong'wawiya, kaaa, aghayaa... ni nadra sana kuwasikia wakisalimia, 'ng'wadila' Wao hufupisha, 'dilla mayu' au dilla bhabha. Majina ya maeneo mengi huanza na Ng'wa. Kwa mfano, ng'wabagimu, ng'wajidalala, ng'wanhuzi... Utajiri wao uko kwenye mifugo.
Vijana wa huko hulizika mapema. Kwa mfano, kama mavuno ya matobholwa, karanga, alizeti na pamba ni mazuri, vijana wa maeneo haya hushinda kwenye ngoma za jadi. Hawajui kusaka ridhiki nje ya maeneo yao, utafikiri wako kisiwani. Wanaotoka nje ya maeneo yao ni wafugaji tu. Wanawake wa huko hupenda kuvaa shanga kiunoni na shingoni ingawa sio wajuzi wa mambo ya Tanga. Wavulana nao huvaa miguuni. Soko la wasichana liko juu sana. Pengine huu ukanda, hasa Meatu, ndiyo unaongoza kwa kutoa mahari kubwa Tanzania nzima.

4.Bhanantuzu /Wanyantuzu
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa Wilaya za Bariadi na Itilima. Hawa ndiyo Wasukuma waliotapakaa kila kona ya nchi hii. Na pengine bila ya hawa kabila la Wasukuma
lisingejulikana kwa namna hii. Kisukuma chao hakina 'shi' bali hutumia 'si' kwa mfano, sikolo, siliwa....Jamaa hawa wanajua kuchakalika kutafuta mali. Hawaogopi kitu, hawaogopi mtu. Jamaa hawa ndiyo Wasukuma pekee wanaothubutu kwenda kupora ng'ombe za Wamasaai. Ni Wasukuma wenye dharau na mikogo mingi. Kama unasikia watu wanaopenda utani na masihara, basi hawa ni kiboko. Si unamjua Danni Makanga? Mambo ya ujanja ujanja na upigaji dili, hapa ndipo penyewe. We mwangalie Chenge tu, au hata Cheyo au hata Mbunge Njaru. Utanipa jibu. Wanaume wa huko hupenda kuoa wake weupe. Kama sio mweupe basi awe na sifa za ziada. Michepuko kwa mwanaume ni kitu cha kawaida.

Swala la ni msukuma yupi anaongoza kwa ushamba na ukilaza, halikuwa lengo la utafiti huu.

Mobheja sana.

UTAFITI WAKO HAUNA MAANTIKI YA KABILA LA WASUKUMA. “UNACHANGANYA”
 
Mm msukuma wa Mallya wilaya ya kwimba ila ukoo wetu umeingiliana na mtabaka yote maaana bariadi mwamapalala ndo baba yangu mdogo anakaa na shangazi yangu kaolewa huko ...shinyanga,igunga,nzega tabora,misasi,jihu,malampaka isagenhe misungwi ilula mwanza mjini na sehemu kibao huko kote na ndugu tena wa dam kabisa
 
Alichokiongea n sahihi kabisa, pia wanyantuzu wako vizuri hata kwenye elimu halaf mkoa wa simiyu kwa ujmla wakazi wake wana kipato cha kati ukilinganisha na mikoa mingine kama geita, shinyanga , au mwanza" kwahyo wako vzr halaf wapo mpka kariakoo wana maduka makubwa , kwenye dhahabu ndo usiseme kila sehem wapo , geita wamedominate wao upande wa dhahabu , kwa kweli n wapambanaji sana, hongera yao
Tatizo kubwa walionalo n wabishi sana kila mtu anajifanya anajua
 
Kiasi amejitahidi, ukweli ni Kwamba hakuna kabila la kisukuma ila sukuma ni upande wa kazikazini kwahiyo wenyeji walitambuana kutokana na upande unakoishi hivyo basi pande nne za dunia ndiyo ulileta kabila la wasukuma, tukianza na SUKUMA ni KASIKAZINI yaani SENGEREMA, MWANZA, DAKAMA ni KUSINI yaani NZEGA, TABORA utakutana na WANYAMWEZI , KEEYA ni MASHARIKI yaaniSHINYANGA, MASWA, SIMIYU utakutana na WANYANTUZU . MGHWELI ni MAGHARIBI yaani KAHAMA, GEITA ambako utakutana na WASUMBWA. Kwa rahaja zao yupo sawa kabisa na hasa hawa wanakiya wananaweza kuuza mama zao ili kupata malí.
 
Back
Top Bottom