Aina za Omba omba!

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,774
Tukiweka mbali wale ombaomba tuliowazoea Barabarani,kuna kundi lingine linakuja kwa kasi na kukua hasa katika jamii yetu la vijana ambao wana nguvu za kutosha Tu na maarifa lakini wameshazoea na kuweka utaratibu maalum wa kujipatia mkate wao wa kila siku!

1.Ombaomba wa Mtaa-Hawa hawana rika maalum wala jinsia kwa siku unaweza pishana nao hata kumi kila mtu ana staili yake ya kuomba.

2.Warembo ombaomba-Kuna watoto wazuri kitaa huwezi amini Aisee ila kazi yao kubwa ni kuamka asbh kujipodoa na kukaa barazani,barabarani au anaweza zunguka mji mzima akirudi home anahesabu mapato.

3.Ombaomba Masela-dah! Hawa huwa wananisikitisha sana kutwa wapo kijiweni,kuongea mambo wenyewe wanayaita ya kijanja wengi wanategemea kengere kwa msosi..Daladala huwa zinawakoma hawa.

4.Ombaomba wa DIGITAL-Hawa ndio wanajumuisha makundi yote hapo juu,ila wao wapo kidigitali zaidi anaweza kupiga simu kwa watu zaidi ya Ishirini kwa siku na kila mtu akamweleza shida yake hili kundi wahusika wengi ni jinsia ya kike unaweza ukawa karibu asikwambie shida yake...Mara nyingi wanapenda kuwa mbali na wapenzi wao ili kufanikisha.

5.Omba omba KIBOKO!!- Hawa ni kiboko kwelikweli Hawaingii kwenye mahusiano mpaka wakupige mizinga ya kutosha,Na Akiwa mpenzi wako Cha moto Utakiona..Hawaangalii maisha hawa ni mizinga kwa kwenda mbele.
 
Hiyo namba tatu ndo iliyonimaliza nguvu kabisa.

Utakuta msela ana minguvu na yupo vizuri bila ulemavu wowote lakini hiyo kasi ya kupiga vizinga haina kipimo.
Badala mtu akapige day worker apate walau 10-15k, yeye yupo kijuweni siku nzima.

Utasikia mwanangu nitoe fegi moja....hapa nilipo nina ubao kise.nge fanya manuva basi......Fanya mpango wa buku n.k

NB Kusaidiana ni moja ya mbinu za ku-survive lakini too much omba omba ni choice.
 
Back
Top Bottom