Aina za ndoa

sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
5,272
7,870
1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu. Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!

2. NDOA YA MIHEMKO (KUTAMANIANA)
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18 mke 16. Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.

4. NDOA YA MAONESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani. Ila ndani hazina utii. Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini. Mahari hutoa anayetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1.

7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWA SABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa. Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.

9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya Kagera. Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA KUCHUMA
Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta wanakufa wao kwanza.

Hebu jiulize wewe upo kwenye aina gani ya ndoa.
 
11. NDOA YA VITISHO.
Hii mwanamke huolewa kwa vitisho vya kilaghai.

Jamaa hutumia njia za hila baada ya kuona mwanamke anasimamia 'sitaki' yake.

Huanza kutoa vitisho kwamba 'tutaona', hapo maana yake kuroga na kuigiza kama kweli kadhamiria kuua mtu kwa ndumba.

Ama mwanamke kuburuzwa kwenye vyombo vya sheria kukandamizwa kutokana na maneno yake ya kejeli ama kiburi aliyoyatoa akipinga kuolewa huko.

Mwisho wa siku mwanamke hulegeza masharti na jamaa kuokota dodo kwa tabu.

Ndoa hizi hudumu kwa sababu jamaa humlea mwanamke kama yai, kwa kuwa alimpata kwa kugaragazwa na kudhalilishwa mno, hawezi kuchezea shilingi chooni.

Kubembelezwa na kudekezwa kote huko, saazingine mimba za dabodabo huwekwa sawa, mwishowe mwanamke hujishitukia kapenda kidhati juu kwa juu na kudumu kwenye ndoa mazima.
 
Write your reply... 12. Ndoa ya kishirikina, muoaji au muolewaji hutumia njia za giza kumpata mwenzake ili waanze maisha, hizi kudumu kwake kunategemea na juhudi za alietumia uchawi kurenew kimbola chake
 
Write your reply... 12. Ndoa ya kishirikina, muoaji au muolewaji hutumia njia za giza kumpata mwenzake ili waanze maisha, hizi kudumu kwake kunategemea na juhudi za alietumia uchawi kurenew kimbola chake
Hizo hudumu kwa kutengeneza mazingira ya upendo wa kweli. Ukitegemea ku renew kizizi wakati tabia mienendo ni mbofumbofu, hufika sehemu kizizi kinadunda na ndoa kusambaratika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom