Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Lakini mkuu wangu yeye ni mwana CCM umesema mwenyewe na ndicho wanachokisimamia kwa wingi zaidi wakijua posho ndizo zitakazo warudisha bungeni ktk kufanyia kampeni. Wao hawafikirii wewe mwananchi isipokuwa maslahi yao wenyewe kurudi mjengoni kwa kutumia Takrima..Peter Serukamba ni mbunge wa Kigoma Ujiji,na ni mjumbe wa NEC ya CCM, ni krimu ya siasa za Kijani na ni sura ya Ujana ya CCM,
Wakati taifa na wanamageuzi kwa ujumla wakipambana kukemea ukwasi tata wa Bunge letu chini ya Mama Makinda aka Bibi Kiroboto, Serukamba kupitia mtandao wa kijamii wa twita @serukamba bila haya wala kihoro, apambana waziwazi na wapinga posho kwa kusema "Kama Bunge haliongezi POSHO basi Bunge lifutwe!
Kwa maneno hayo tu, mimi binafsi namuona ni janga la kitaifa na lisiposhughulikiwa litaliangamiza taifa!
Kumbuka kila aliye mtz na alipae kodi ya haki basi kodi hiyo hutumiwa ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kukaa bungeni wabunge na watumishi wengine, hivyo dhana ya Serukamba kuwa wengi wawanaopiga ukelele wa kupinga posha hasa kwake yeye hawamsaidii kwani hawakumchagua na hawatamchagua!
Lakini mkuu wangu yeye ni mwana CCM umesema mwenyewe na ndicho wanachokisimamia kwa wingi zaidi wakijua posho ndizo zitakazo warudisha bungeni ktk kufanyia kampeni. Wao hawafikirii wewe mwananchi isipokuwa maslahi yao wenyewe kurudi mjengoni kwa kutumia Takrima..
Mkuu kuna kilicho nyuma ya pazia hapo? Hebu pembua bila mawaa!Peter sio ndio petro....nadhani mtandao wao unahesabika siku zake za kuchuma
Njaa zinamsumbua kilaza tu
Unamaanisha kuwa idadi ya wapiga kura wake 98% ni elimu zao ni darasa la saba?wewe unategemea nini kwa mtu ambaye kura kapigiwa na 98% darasa la saba? tena hawana kazi!
Hata kama mimi si mbunge naweza kuunga mkono suala la wabunge kulipwa vizuri zaidi (si lazima kwa njia ya posho ya vikao). Nianze kwa mambo mawili: Kwanza, kwa jinsi nilivyofuatilia suala hili, si kweli kwamba wabunge wanaoshabikia posho ni wa CCM tu. Asilimia 90 ya wabunge wa Chadema wanataka sana hizo posho, isipokuwa wengi wao wanawaogopa kama chui viongozi wao wakuu wanaopinga posho hizi. Pili, kusema kwamba wabunge wakafanye kazi walizotumwa na wapigakura wao, badala ya kudai posho ni kutojua kwamba wabunge hawana job description maalum ya kazi zao. Wabunge hawa wakishachaguliwa, kila jambo jimboni kwao ni kazi yao - kuanzia ufuatiliaji wa utekelezaji wa ahadi za serikali na za kwao wenyewe, kufuatilia kero za wananchi za aina yoyote ile, kusaidia wananchi kwa shida zao za kijamii (kama michango kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi, ujenzi na misaada ya makanisani na misikitini, misaada ya michezo na burudani) na shida binafsi za wananchi kama magonjwa, elimu ya watoto, michango ya misiba na harusi. Nilivyofuatilia wabunge wote wanaopinga posho hizi (kutoka CCM na upinzani) ni wale wabunge matajiri na wafanyabiashara kama vile Mbowe, Mohamed Dewji, Mkono, Ndensamburo n.k. na pia wabunge wanaopata misaada kwenye NGOs zao kama vile Zitto anayepata hela nyingi toka kwa wafadhili (Ujerumani) na chinichini kutoka kwa viongozi wa mashirika ya Umma wanaomwogopa kama mkt wa POAC, na wengine wenye NGOs kama January n.k. Hawa wana vyanzo vizuri tu vya kuhudumia majimbo yao kwa shida zote za wananchi. Lakini kwa wabunge wanaotegemea malipo ya Bunge tu wana hali mbaya sana. Na bahati mbaya, wananchi na viongozi wa dini mnaolaumu suala la posho ndio wa kwanza kuleta kadi za michango kwa wabunge. Mimi ningependekeza kwamba badala ya posho, wabunge wangelipwa tu mishahara mikubwa kama milioni kumi kwa mwezi. wala sitaweza kuwaonea wivu hata kama mimi mshahara wangu ni kiduchu. Wana majukumu makubwa. Wala simlaumu Serukamba kwa msimamo wake huo.Hakuna mbunge wa ccm ambaye hashabikii posho,kwao hawana mpango na mlala hoi kwani wanapaswa kufanya kazi walizotumwa na wananchi wao.Na wala hawakutumwa kwenda kudai posho, hayo ni mawazo binafsi ambayo hayawasaidii wapiga kura.
Lakini mkuu wangu yeye ni mwana CCM umesema mwenyewe na ndicho wanachokisimamia kwa wingi zaidi wakijua posho ndizo zitakazo warudisha bungeni ktk kufanyia kampeni. Wao hawafikirii wewe mwananchi isipokuwa maslahi yao wenyewe kurudi mjengoni kwa kutumia Takrima..
unauhakika gani kama hiyo akounti ya twitter ni yake? Anaitumia yeye mwenyewe?