Aina tatu za wanawake ambazo manamume hukolea nazo

ugaibuni

Member
Jan 5, 2012
15
9
[h=2]Aina tatu za wanawake ambazo manamume hukolea nazo[/h]
Mimi sio mtaalamu kwa sana ila leo nitawaletea nini ninakijua nanyi mupate kuchangia

thumb_imaghes.jpg
Mwanamke mcheshi


Mwanamke ambaye hupenda kutabasamu(mcheshi) humfanya mwanamme asisite kutaka kuongea naye au hata kutaka mahusiano zaidi. We fikiria wale akina dada ambao muda wote wao wameuchuna, kabla ya
kwenda unafikiria uanzie wapi. Siku moja baada ya kazi tukawa katika majadiliano kuhusu masuala ya mahusiano. Binafsi nikataka kujua sababu ambayo inawafanya akina dada wengi weusi kuwa serious muda mwingi kitu kinachopelekea wanamme wengi weusi kuamua kutoka na akina dada weupe au wa kiasia kutokana na hurka yao ya kuwa wacheshi kwa wanamme. Yeye alijibu kwa kusema ukijichekesha kwa mwanamme mweusi inamaanisha unampa nafasi hivyo basi ni heri kuwa ngangari. Nimekuwa nikisoma sehemu nyingi mno wakisema wanawake weusi wana hurka ya kutokuwa na ucheshi kwa wanamme labda awe amevutiwa sana.Sijui munaonaje hili?



thumb_womanlisten.jpg
Mwanawake msikivu.

Amini usiamini, wanamume wengi hupenda wanawake wasikivu, sina maana mwanamke anatakiwa kumsikiliza na kumkubalia mwanamme kwa kila anachosema,la hasha. Nina maanisha pindi unapokuwa pamoja na mwanamme (mume,rafiki au hata mchumba) jaribu kumpa nafasi ya kuongea. Kuna siku nilikuwa naangalia kipindi kimoja cha kutafuta wachumba, Katika kipindi hicho mwanamme hupata nafasi ya kukutana na warembo watano, baada ya maongezi machache huchagua watatu ambao wataenda date kwa mida tofauti. Basi kidume kilikutana na mrembo mmoja ambaye muda wote alikuwa anamgonga maswali jamaa na kumfanya asipate hata muda wa kuongea alichotaka. Yule jamaa alitosa palepale.Wanaume wengi huchukia warembo wanaochonga sana.
Chukulia siku unakutana na mrembo anayesikiliza kwa kutumia macho yake,kuitikia kwa kichwa na ishara tofauti. Ni dhahiri mwanamume atakolea ipasavyo na kutaka muda wote kuongea na wewe.

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]

thumb_mya-hairstyle.jpg
Mwanamke anayevutia kimavazi
[/FONT]

Amini usiamini,wanamume wengi hupenda wanawake wanaopendeza na kuvutia kimavazi. Kuna baadhi ya wanawake husema mwanamme hawezi kuvutiwa na mwanamke ambaye sio chaguo lake. Hii si kweli kwani wanamume wengi huanza kuvutiwa machoni halafu mambo mengine huendelea. Chukua mfano wamekaa vidume vitatu halafu akapita binti aliyevalia vyema(simaanishi lazima awe kavaa kimtego), ni lazima wawili kama sio wote watageuza macho(si unakumbuka ile picha ya Obama na Santosi?), kutathmini halafu kuendelea na hatua inayofuata ni hulka ya wanamume.




hayo ndio niliyotaka kuwaambia dada zetu kwa leo.


[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Source: Ughaibuni.com[/FONT]
 
Kwa mwanamke msikivu hapo atakuwa amemshika mwanaume sana ila km si msikivu mapenzi huisha kabisa
 
Mkuu kwa kuongezea, ungegusia na suala la Tabia njema, ufahamu, busara and attitude yake mbele za watu huusika sana. Pia Receiption na mara nyingine hata umbile lina nafasi kiasi.
Ni mtazamo tu. :nerd:
 
Kwa mwanamke msikivu hapo atakuwa amemshika mwanaume sana ila km si msikivu mapenzi huisha kabisa

usikivu mambo yote mkuu.
ukimwambia jambo atabadilka sababu ni msikivu.
kama ni mchafu, akiwa msikivu atabadilika na kuwa msafi.
kama ana kiburi, akiwa msikivu atabadilka na kuwa mnyenyekevu.
yani lkila jambo libnabebwa na uskivu PROVIDED SHE LOVES YOU..
 
mambo yote uchangamfu na muonekano; kama mtu mwenyewe kununa ndo kawaida yake hata kitandani atakuwa mlalamishi tu...mtazamo tu
 
vyaa gaguloo,skintyt,shumizii,kishidaaa na sketii ndefuu,yenye pichaa ya mauwa uwaa na marindaa,pigaa mkanda wako wa kipepeo hakikaa utakuwaa burudaniii
Ngoja nijifunze kutabasamu, kusikiliza na kupendeza.

Swali. . . mavazi gani niwe navaa?
 
Ngoja nijifunze kutabasamu, kusikiliza na kupendeza.

Swali. . . mavazi gani niwe navaa?

...lol...mie huvutiwa na anayevaa bai bui, kujifunika ushungi na mwenye mwanya!...ati nawewe 'unakolea' na wanaume gani achilia u 'gentleman?'

...nilimsoma Afrodenzi yeye hukolea na mwenye Bass, BJ mwenye kifua...na wewe?!
 
usikivu mambo yote mkuu.
ukimwambia jambo atabadilka sababu ni msikivu.
kama ni mchafu, akiwa msikivu atabadilika na kuwa msafi.
kama ana kiburi, akiwa msikivu atabadilka na kuwa mnyenyekevu.
yani lkila jambo libnabebwa na uskivu PROVIDED SHE LOVES YOU..

Msikivu ndo kila kitu!
 
[COLOR=#ff0000 said:
Ndokeji;[/COLOR]3145499]Napenda weupe wanavutia balaa

Wasukuma wengi hasa wa vijijini ni jadi yenu, mnazimikaga sana kwa totos white. Hata ID yako inaonyesha hivyo. Ndokeji.
 
Msikivu ndo kila kitu!

Mkuu hapo kwenye red vipi? Usikivu ndo kila kitu?
Nafikiri mwanaume ili akolee ki-sawa sawa, anahitaji afanyiwe combination ya mambo mengi kama vile, Uchangamfu, Mavazi, heshima, tabia njema, umbile, busara n.k.
 
vyaa gaguloo,skintyt,shumizii,kishidaaa na sketii ndefuu,yenye pichaa ya mauwa uwaa na marindaa,pigaa mkanda wako wa kipepeo hakikaa utakuwaa burudaniii
Mbona navaa hivyo vyote sasa hivi na sioni kama kuna anaevutiwa? Yani hamna hata anaeniangalia mara mbili.
 
Back
Top Bottom