Aina nyingine ya wizi mpakani Tunduma

dali kimoko

Senior Member
Jan 25, 2021
114
138
Habari ya asubuhi wanajamii, sasa naomba vyombo vya dola viangalie hili tatizo pale Tunduma border. kumezuka kikundi cha watu wanajiita umoja wa madriver wa IT.

Yaani gari zinazovuka mpaka wetu, hawa jamaa wanachukua eti ushuru wa shs 5000/ kila gari tena ni lazima, ukiwauliza wanasema ni Chama, sasa chama kwani ni lazima ujiunge?

Pili, hizo risiti zao hazina hat tin na wala sio za EFD kwa hiyo mapato ya Serikali yanapotea, tatu wanaongeza changamoto na kama si mzigo kwa wateja wa hizo gari.

Sasa basi tunaomba Serikali ya Mkoa iingilie kati hili swala kabla mambo hayajaharibika, sisi tunaona huu ni wizi, imagine pale zinavuka gari ngapi kwa siku?

DC Songwe, RPC na TRA fuatilieni hili ni tatizo hivi kuna gari pale hazijavuka eti mpaka walipwe.
 
Huo upuuzi mumeulea nyie kwa kukubali kuwapa hizo hela. Mnatoa pesa ambayo hamsomewi mapato na matumizi yake?
 
Poleni sana.. ila ni vyema ungeliwasilisha mamlaka husika ukiwa pamoja na vielelezo vyote..
 
Back
Top Bottom