Aina mpya ya wizi Vodacom

Aina mpya ya wizi Vodacom

Wanachofanya kukuibia ni hivii:-
Ukinunua "bando" i.e la internet kwa M-Pesa hawakupi majibu ya ukamilifu wa muamala, ukiangalia salio unakuta lipo vile vile.

Muda ukipita utajaribu mara ingine kununua, pia hutapewa report ya kufanikiwa, kwa kuwa salio halitakatwa, utaridhika kuwa muamala haujakamilika.

Utajaribu mara ya tatu au hata nne, ukiisha kata tamaa na kuacha baada ya nusu saa au zaidi kidogo wanakuuzia miamala ya bando zooote ulizojaribu kununua na mbaya zaidi uwe ulinunua bando za siku, unaweza kujikuta umeibiwa hadi 10,000/ kwa staili hii walioibuni hawa vodacom.

Natafuta njia bora kabisa ya kuachana nao maana tazama wanatumia mabilioni ya shilingi kutafuta wateja kwa matangazo ya biashara yao, lakini wanashindwa kutumia mtaji mdogo kabisa kuendelea kunipa huduma niwe sehemu ya kuwaingizia faida iliyokusudiwa na matangazo ya kuwalipa kina daimond kusaka wateja.

Piga costomer care yao uone majibu yao ya kukariri, AIBU.
 
Leo nimenunua mda wa maongez 2200 kutaka kujiunga ikagoma kbsa km mara mbili mara ya tatu naambiwa salio halitoshi...kucheki imebaki km sh 200 zimeliwaje wanajua hao wezi...kwa kweli TCRA wawashughulikie voda
 
Ili jambo linakela sana unaweza nimejikuta nimejiunga mara tano elfu moja mia tano
Tunawezaje kutoka tukiwaachia maumivu makali?
Hapo ndio nataka kujua
 
Leo nimenunua mda wa maongez 2200 kutaka kujiunga ikagoma kbsa km mara mbili mara ya tatu naambiwa salio halitoshi...kucheki imebaki km sh 200 zimeliwaje wanajua hao wezi...kwa kweli TCRA wawashughulikie voda
Hivi ili ukope kwenye mpawa yao masharti yakoje?
 
Wanachofanya kukuibia ni hivii:-
Ukinunua "bando" i.e la internet kwa M-Pesa hawakupi majibu ya ukamilifu wa muamala, ukiangalia salio unakuta lipo vile vile.

Muda ukipita utajaribu mara ingine kununua, pia hutapewa report ya kufanikiwa, kwa kuwa salio halitakatwa, utaridhika kuwa muamala haujakamilika.

Utajaribu mara ya tatu au hata nne, ukiisha kata tamaa na kuacha baada ya nusu saa au zaidi kidogo wanakuuzia miamala ya bando zooote ulizojaribu kununua na mbaya zaidi uwe ulinunua bando za siku, unaweza kujikuta umeibiwa hadi 10,000/ kwa staili hii walioibuni hawa vodacom.

Natafuta njia bora kabisa ya kuachana nao maana tazama wanatumia mabilioni ya shilingi kutafuta wateja kwa matangazo ya biashara yao, lakini wanashindwa kutumia mtaji mdogo kabisa kuendelea kunipa huduma niwe sehemu ya kuwaingizia faida iliyokusudiwa na matangazo ya kuwalipa kina daimond kusaka wateja.

Piga costomer care yao uone majibu yao ya kukariri, AIBU.

Ila ili lina ukweli,juzi Kati imenikuta Mimi katika number yangu #847159___nimenunua Mara mbili bundle LA 24hrs bila kupanga
 
me mambo ya internet huwa nanunua bundle za halotel,voda hawajala jerojero zangu cku nyingi sana japo nilikuwa mteja wao mzuri na mwenye mahaba kwao.
 
Wameniliza jumapili mimi kila nikiweka mb dkk tatu wameshapita nazo nikapiga simu huduma kwa wateja wakanijibu uliacha data wazi nikawajibu mbona miaka yote hamkati!? Utanikata vipi mb 1500 kwa mara moja pasipo kutumia data !? Nikaweka elfu moja nayo wakapita nayo!! Nikaamua kurudi airtel.
 
Voda wezi siku zote,kama hii ya dabo bando hakuna chochote usijaribu kabisa utalia
 
Voda wezi siku zote,kama hii ya dabo bando hakuna chochote usijaribu kabisa utalia

Dabo Bando! Labda unakosea Mkuu mi huwa ndo naikamua sana tu,sema inachanganya, kuna muda naanza kumaliza bonus na wakati mwingine naanza kumaliza bando lenyewe
 
Nachelewa kulipa, sitoweki mkuu

Kama Mimi? Wananidai tangu 2014 mpaka leo sijawalipa, walianza kunipiga mikwara weee, eti ooh utaorodheshwa kama mdaiwa sugu katika asasi za mikopo, lakini wapi, sasa wamezima zao wananibembeleza nilipe kidogo kidogo ila soon ntawalipa. Mimi kuna mambo mawili wamenishinda, kwanza... Napigiwa simu mtu anajibiwa namba haipatikani wakati nipo hewani na Network ipo full na simu napiga kama kawaida, nikapiga customer care wakaniambia nizime simu kisha niiwashe, na kweli nilipofanya hivyo simu zikawa zinaingia kama kawaida, sasa unaweza kukaa siku nzima usipokee simu mpaka uje kushtuka imekula kwako, la pili.....msg za Goodnight kuingia saa nne asubuhi, yaani natumiwa msg saa tatu na nusu usiku inaingia saa 4 asubuhi!!!!!! Kuna siku nasafiri natoka Moro naenda Tanga, napewa maelekezo kwa njia ya simu sasa vuta picha kilichotokea njia nzima nikawa mtu wa kuzima simu na kuwasha mpaka nikamwambia muhusika tumia WhatsApp. Aah!!! Yaani Vodacom waacheni tu kama walivyo,ila nawakubali kwenye Internet kwa mimi sina tatizo nao maana hata kama hakuna 3G nastream YouTube kama kawaida
 
kwan huko ulipo Halotel haishiki, kwanini unajipa presha nahao wezi , mi mwenyewe pins nipo coda nimewahi kuibiwa zaid ya Mara 2, nikachukua uamuzi wa kuhama mapema
 
customer care washakariri jibu uliacha bundle wazi...Wezi tuu hao...
 
Na mpesa ikishafika jioni kuanzia sa kumi na mbili haifanyi kazi unaambiwa tunashughulikia tatzo hili nalo jipu...m skuiz nmerud zangu tigo

Ungepitiliza hadi halotel tigo ni majizi kama voda tuu mkuu..
 
Back
Top Bottom