Aibu!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Guyana Halima, Dec 24, 2009.

 1. Guyana Halima

  Guyana Halima Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani mmeona gazeti la [COLOR="Red[B]"]LEO TENA [/B][/COLOR]la leo!!!? Ivi ni gazeti linalotia aibu au ile picha ndo inayotia aibu!!? Kweli zile ni picha za kuweka front page?? Ivi watoto wetu watakuwa na maadili gani kwa mtindo huu!!? Hivi tunajenga au tunabomoa! Sababu ni picha za aibu watu wapo uchi kabisa,wameziba sehemu chache lakini sehemu kubwa ipo uchi! Unaweza kuwazuia watoto wasisome magazeti kama haya nyumbani lakini kwenye meza za magazeti je? maana na watoto siku izi wanasimama kusoma magazeti!! YANI ni AIBU!!
   
 2. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  duh mi nilishindwa hata kusimama kwenye meza ya magazeti leo na nimeshindwa hata kununua. ile ni aibu kwa gazeti kusema ukweli na kama kuna mamlaka husika wawachukulie hatua kwa kutoa picha za uchi wazi wazi mbele ya jamii. haya magazeti ya kina shigongo na ndugu zake wanaishia kutuhalibia watoto wetu tu jamani.
   
 3. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tutasema kwa wakubwa wakirudi baada ya uchaguzi kwani kwa sasa wako likizo ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2010. Kifupi serikali iko busy na mambo ya msingi na kujiimarisha kwa ajili ya mambo yajayo.

  Nakumbuka zamani (enzi za mwalimu) wizara ya yenye dhamana na mambo ya utamaduni ndio ilikuwa ikishughulikia mambo haya na ilikuwa inafanya kazi kweli kweli. Kwa sasa baada ya kuanza hiki kinachoitwa utandawazi hali imekuwa mbaya zaidi na hakuna udhibiti wowote. Nakumbuka hata nyimbo zilikuwa zinahaririwa kabla ya kufika sokoni kwa hiyo muziki wa wakati huo maneno yaliyokuwa yanatumika yalikuwa ni yale tu yanayokubalika katika maadili ya jamii ya kitanzania ya wakati huo. Kwa sasa hakuna gavana ukikosa cha kuuza na ukagundua kwamba watu wanapenda matusi basi waweza fanya hivyo.
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kwahali kama hizo bongo hatufiki...
   
 5. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Yawekwe sehemu maalum wakayauzie huku,ukipita kwenye vibanda vya magazeti mpaka noma
  aaghhhhhhhhhhhhh inakera
   
 6. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi huwa najiuliza,,, hawa wanaochapisha magazeti kama yale! hawana hata watoto! au hawana wazazi (mama/baba) kama yote hayo hawana basi hata hisia za AIBU ambazo kila binaadamu kamili anakua nazo,,pia hawana!
  Mwanzoni nilidhani labda mimi nimeachwa nyuma na haya tunayoyaita maendeleo? Nimefarijika sana leo kusikia kuna wengine nao wanakereketwa nayo.
  Sijui ndio kuiga!
  Hivi sisi wadanganyika wa kawaida,,,hakuna lolote tunaloweza kufanya kuondoa UOZO huu..
  INAKERA
   
Loading...