Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Aibu ya mwaka yampata Lissu!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.
 
Unaonekana kutokuwa mwelewa wa kinachotakiwa. Ngoja waiwakilishe hadharani ndipo utakopogundua kwanini ilikuwa inafichwa kiasi hicho. Kumbukumbu kama hizo kama ziko kamilifu hazifichwi bali huwa zinawekwa kwenye jumba maalumu kwa ajili ya watu wote wananchi na wageni kuziona, kulikoni zifichwe kwenye safe?
Cha kwanza cha kujiuliza ni je kama ulikuwa muumhgano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar, leo hii Zanzibar ipo Tanganyika ilienda wapi??? Hiyo hati iliandikwa iwe hivyo?? Je hati hiyo ilitamka kuwa Zanzibar wawe na katiba yao peke yao na Tanzania ya muungano iwe na yake tofauti?
Hebu jitahidi kutafakari zaidi kabla ya kuandika humu Mkuu.
Nimeamngalia ITV leo jinsi Waziri wa Nchi Wasira alivyokuwa anaongea kwa kutamba nikashangaa anchotambia ni nini? kwamba hati ipo? Je anakifahamu kilichopo ndani ya hiyo hati? na kwamba je makubaliano hayo yanatekelezwa kwa dhati na pande zote mbili? Kukosa busara ni kitu kigumu sana.
Asante.
 
Je muungano huu ni halali?
Hati hii ni halali?
Sahihi ya nyerere ni halisi?
Sahihi ya karume ni halisi?

Hayo maswali atayajibu Lisu wakati akichangia hoja,labda aingie mitini
 
Mimi naona wewe ndie umepata aibu ya mwaka maana hata ulichokiandika hakieleweki.

Kama ujui kusoma hilo sio tatizo langu.

Jambo la kufanya ni kuwalaumu wazazi wako ambao wameshindwa kukusomesha.

Who knows, huenda hata wazazi wako hawakwenda shule so hawakuona umuhimu wa ikukupeleka shule.
 
Je muungano huu ni halali?
Hati hii ni halali?
Sahihi ya nyerere ni halisi?
Sahihi ya karume ni halisi?

Sasa wewe unachekesha yaani unataka Tundu Lisu akuambie hati ni halali ndio ukubali? Sahihi ya Nyerere na Karume unazijua mpaka uhoji sio halali???
 
Ni aibu kwa Ikulu kutoa hati hiyo baada ya watu kuidai kwa nguvu kubwa.

Kifuatacho ni kujibu maswali haya ya Lissu

1.Je,hati hiyo ni halali

2.Kama hati hiyo ni halali,je muungano huu ni halali?

Hayo ndio maswali ya Lissu yanayosubiri majibu
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu, sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo, jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa hati ya muungano hauna tena soko.

Ni aibu sana kwa mwanasheria kama yeye!! Japo hazijui vizuri sheria huwa anazichanganya
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu, sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo, jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa hati ya muungano hauna tena soko.

Naamini kuna na wengine ambao kama ulivyo wewe, hamkumwelewa Tundu Lissu alikuwa anasema nini. Ila kwa tuliomwelewa anachokifanya kinakubalika.

Kupatikana kwa hati ya Muungano siyo kitu kigumu kiasi cha serikali bila aibu kudai iko UN! Kwamba mnataka tueleweje? Ukipangishwa nyumba Mkataba anakaa nao mwenye nyumba au?

Chochote ambacho kilisemwa ni baada ya kigugumizi cha Serikali kuitoa hati hiyo, hata pale ambapo iliombwa na Kamati za bunge maalum la katiba! Ni serikali ya ajabu na iliyojaa upuuzi inayoweza kufanyia mzaha hata swala kama hilo. Vinginevyo ni wazi kuwa nia ya serikali haikuwa njema kwa kuificha hati hiyo.

Hata sasa, pamoja na kutolewa kwa hati hiyo kila mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza hati hiyo ilikuwa wapi? Na huko ilikokuwa ilikuwa inafanyiwa nini ndo itolewe leo? Ni kweli Watanzania wanapaswa kuiamini hati hiyo? je! HATI HIYO ILIYOTOLEWA PAMOJA NA KUFICHWA KOTE HUKO NI HATI HALISI NA HALALI?

Nasikitika tu kuwa pamoja na mwamko walio nao Watanzania wengi, bado kuna wanaofikiria kama wewe out there!
 
Unaonekana kutokuwa mwelewa wa kinachotakiwa. Ngoja waiwakilishe hadharani ndipo utakopogundua kwanini ilikuwa inafichwa kiasi hicho. Kumbukumbu kama hizo kama ziko kamilifu hazifichwi bali huwa zinawekwa kwenye jumba maalumu kwa ajili ya watu wote wananchi na wageni kuziona, kulikoni zifichwe kwenye safe?

Kwanini umejawa na "negative attitude"!?

Nyaraka ipo wazi, sasa wasiwasi wako wa nini?

Tuliitaka hati, sasa ipo hadharani. Leo mnakuja na mambo mengine tena. What's wrong with you guys?
 
Na wewe mbona hueleweki,

Hati bado haijawasilishwa.. Pia hata kama ikiwasilishwa je ni halali? Haikupata kibali cha BWZ.. Sasa TL ameumbuka vp? Na wewe PATIENT ZERO wacha ulimbukeni.

Njama

Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu, sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo, jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa hati ya muungano hauna tena soko.
 
Hayo maswali atayajibu Lisu wakati akichangia hoja,labda aingie mitini

Lissu hawezi ingia mitini. Alichokifanya ni kutafuta njia ya kumtoa nyoka pangoni ili ampige rungu la kichwa. Kumbuka wajumbe wengi wa CCM walikuwa wanazungumzia misingi ya kuanzishwa muungano ilindwe kulingana na makubaliano ya awali ya waasisi wake. Sasa ndio ( kama hati hiyo ni halali) tutakapo ona kuwa muungano huu uliopo sasa ambao serikali ya Zanzibar imeshajitenga kuwa sio misingi ile ya awali kwa hiyo yale aliyosema Warioba ndiyo yanayopaswa kufanywa sasa katika kuunda katiba mpya.
Nakuhakikishia usione Lissu na wenzie wanacheka ukadhani ni machizi, wameshajua wapi pa kuwapiga bao. Maana sidhani kama hayo yaliyofanyika siku za karibuni yako kwenye hati ya makubaliano ya awali. Tatizo la wale wanaofata msimamo wa Chama na kutukana na kuzomea wanaiga style ya kasuku tuu.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Unaonekana kutokuwa mwelewa wa kinachotakiwa. Ngoja waiwakilishe hadharani ndipo utakopogundua kwanini ilikuwa inafichwa kiasi hicho. Kumbukumbu kama hizo kama ziko kamilifu hazifichwi bali huwa zinawekwa kwenye jumba maalumu kwa ajili ya watu wote wananchi na wageni kuziona, kulikoni zifichwe kwenye safe?
Cha kwanza cha kujiuliza ni je kama ulikuwa muumhgano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar, leo hii Zanzibar ipo Tanganyika ilienda wapi??? Hiyo hati iliandikwa iwe hivyo?? Je hati hiyo ilitamka kuwa Zanzibar wawe na katiba yao peke yao na Tanzania ya muungano iwe na yake tofauti?
Hebu jitahidi kutafakari zaidi kabla ya kuandika humu Mkuu.
Nimeamngalia ITV leo jinsi Waziri wa Nchi Wasira alivyokuwa anaongea kwa kutamba nikashangaa anchotambia ni nini? kwamba hati ipo? Je anakifahamu kilichopo ndani ya hiyo hati? na kwamba je makubaliano hayo yanatekelezwa kwa dhati na pande zote mbili? Kukosa busara ni kitu kigumu sana.
Asante.

nimelike mkuu
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa upotoshaji juu hati ya muungano hauna tena soko.
Mkuu tambua kuwa Game ndo kwanza linaanza! Kwanini Serikali ilishindwa kuiweka hadharani miaka yote hiyo? content za hiyo hati zikoje? Kwangu mimi haya yote ni malumbano yasiyokuwa na tija! MUHIMU kwangu ni kuondoa kero zote za Muungano kwa maslahi mapana ya wananchi wa Tanzania... tuwe na serikali 1,2,3 poa tu alimradi Muungano huu hautawakwaza wananchi wa pande moja ya Muungano ....
 
Lissu hawezi ingia mitini. Alichokifanya ni kutafuta njia ya kumtoa nyoka pangoni ili ampige rungu la kichwa. Kumbuka wajumbe wengi wa CCM walikuwa wanazungumzia misingi ya kuanzishwa muungano ilindwe kulingana na makubaliano ya awali ya waasisi wake. Sasa ndio ( kama hati hiyo ni halali) tutakapo ona kuwa muungano huu uliopo sasa ambao serikali ya Zanzibar imeshajitenga kuwa sio misingi ile ya awali kwa hiyo yale aliyosema Warioba ndiyo yanayopaswa kufanywa sasa katika kuunda katiba mpya.
Nakuhakikishia usione Lissu na wenzie wanacheka ukadhani ni machizi, wameshajua wapi pa kuwapiga bao. Maana sidhani kama hayo yaliyofanyika siku za karibuni yako kwenye hati ya makubaliano ya awali. Tatizo la wale wanaofata msimamo wa Chama na kutukana na kuzomea wanaiga style ya kasuku tuu.

Sent from my iPad using JamiiForums

I like it
 
Hata hivyo kama ikulu ingekuwa makini, isingesubiri hadi maswali yame mengi kiasi hiki, inaonekana kabisa kuna utata fulani kuhusu hiyo hati. Sijawahi kuwa na wasi wasi kuhusu hilo, lakini sasa nina wasi wasi
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lako la wahuni, tafuteni uongo mwingine, maana wa upotoshaji juu hati ya muungano hauna tena soko.
Du naona umetoka kunywa mbitu na upo hoi, haya bwana wahi lumumba square uchukue buku saba za mbitu ya kesho
 
Back
Top Bottom