Aibu ya mwaka: kumbe mahari ina umuhimu sana

kwenzi

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
669
666
Wasalam,

Juz nilikwenda kwenye msiba wa rafik yangu wa kike ambaye amefariki,Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Vituko vilivyo tokea huko daah nikajua kumbe mahari ni muhimu sana kuitoa kabla ya kuishi na mwanamke.

Jamaa yake alikuwa mchaga waliishi bila jamaa kutoa mahari wala ndoa.katika maisha yao walipata watoto wawil huyu wa tatu ni mchanga kabisa ambaye ndio chanzo cha kifo chake mtoto kaziliwa hai mama kafa.

Mziki ulipo anza sasa jamaa akataka akamzike moshi,ndugu wa mwanamke wakamuuliza umetoa mahari jamaa kimya....bhas wahehe wale wakamwambia hapa hazikwi mtu mosh wala nn.

Mahari itolewe Leo Leo ikishindikana tunaondoka na mtoto wetu tunaenda kuzika iringa.

Aibu ikawa sasa kwa wachaga ikabidi wakae kikao cha ghafla kuitafuta hiyo mahali,ambayo waliambiwa ni 1300000.

Baada ya changa ni kuchange wakaipata walipo itoa tena kwenye msiba ndio wakapewa ruhusa..
Ya kumzika moshi

Yani wakaoa maiti aibu ilioje hii...

Funzo: wanaume wezangu tusipende ganda la ndiz pambana toa mahari ya watu weka mtoto wa watu ndan kwa aman.
Kuliko kujipatia aibu kubwa namna hii tena mpaka kwa ndugu zako.

Mie nashukuru nimetoa yoteee.. sidaiwi hata senti moja.
 
Sio mahari tu. Mtu unakuta mwanaume anaishi na mwanamke na wameshazaa na mtotot na wanaishi pamoja hakuna kujishauri miaka kadhaa wanatakiwa kufunga ndoa.
Naamini kuna baraka nyingine wanazikosa toka kwa Mungu kosa dogo tu la kutokufunga ndoa
 
Duuu aibu. Nakumbuka nshawahi hudhuria msiba na mama wa rafiki yake Tanga huko!! Mume wa marehemu hivyo hivyo hakua amelipa mahari ndugu wa mke wakagoma kushiriki hadi walipwe mahari na faini za watoto au wanaondoka na maiti na watoto wao. Likapitishwa bakuli pale hadi waombolezaji tukachangia mahari.
Ila msiba ulichelewa mnooo kwasabu ya hizo mila zao.
 
Noma sana mpaka waombolezaje mkachangia mahari ..aisee bonge la aibu kwao
 
Yuko mtu alimchukua mamdogo bila mahari na akazaa nae watoto. Baadae yule mamdogo alifarikibna akazikwa upande wa mumewe. Kilichofuata ni mtoto wa kwanza wa kiume kushindwa kuzalisha wanawake karibia wawili aliokuwa nao. Ikabidi bamdogo ashauriwe kulipa mahari kwa babu na kuomba msamaha. Ndo dogo aoe tena kwa ndoa na mahari ili wapate mtoto. Hayo kashayatimiza sasa twasubiria.

Mambo mengine usipokumbushwa utaishia kudhani umelogwa. LIPA MAHARI.
 
Sio mahari tu. Mtu unakuta mwanaume anaishi na mwanamke na wameshazaa na mtotot na wanaishi pamoja hakuna kujishauri miaka kadhaa wanatakiwa kufunga ndoa.
Naamini kuna baraka nyingine wanazikosa toka kwa Mungu kosa dogo tu la kutokufunga ndoa
Ni kweli mkuu Mungu ajalie yangu nifunge mwakan japo kipengele çha mahar nimekimaliza
 
Nishaona huku kijijini wazazi wote wawili walishafariki, bibi wa kichaga kaja kumchukua mjukuu akamsomeshe, alilipa mahari kwanza ndo akapewa mtoto
 
Nyie mkifikiri mkopo upo bank tuu au kwenye vyama vya kuweka na kukopa hata kwenye kuoa upo, Ila kwangu mimi mtu akimpenda binti yangu na ana dhamira ya kuoa, aje tuu ajitambulishe ajibebee mke apeleke, mahari kwangu si lazima, cha msingi na cha sekondari waishi salama.
 
ujinga tu. waliacha kukomaa mtu yuko hai aondokane na zinaa wanadai pesa mtu kajifia. mila nyingine bwana.
 
Back
Top Bottom