Captain22
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 623
- 279
Mradi huu ulizinduliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, mh Dr. J. M. Kikwete na aliyekuwa waziri wa ujenzi na mgombea urais, mh Dr. J. P. Magufuli. Mradi ni sehema ya ujenzi wa Namanga - Taveta - Voi highway. Kinachonisikitisha ni kuwa mpaka sasa hakuna hata sentimita moja ya lami iliyokamilika. Barabara hii ni urefu wa 14km na unatakiwa kukamilika ndani ya miezi 18. Ujenzi ulizinduliwa mara tuu ya mh Dr. J. P. Magufuli kupitishwa kuwa mgombea. Binafsi kwa jinsi ninavyoona vifaa duni, nguvu kazi hafifu na kutokuwepo na maendeleo yeyote ya mradi nashawishika kuamini kuwa uzinduzi uliharakishwa ama kwa sababu za kisiasa au nyinginezo. Wakazi wa Arusha ni mashahidi wa hili.