Aibu Kubwa kwa Jeshi La Polisi

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Habari Comrades..

Hii ni Aibu kabisa kwa Jeshi la Polisi kutokuwa na Receipt Books/ Stakabadhi za Malipo za serikali (zile za yellow) kwenye vituo vyake mbalimbali vilivyopo hapa DSM.

Malipo haya ya serikali hukusanywa pale mtu unapokwenda kwenye vituo vya polisi kuomba huduma kama ya kupotelewa (loss report) na nyaraka mbalimbali kama kadi za benki, vitambulisho, driving licence nk nk.

Leo nilikwenda kupata huduma hiyo pale kituo cha Mbezi kwa Yusuph nikaambiwa watanifungulia Taarifa tu ya kupotea kwa hivyo vitu vyangu lakini sitaweza kupata Loss Report maana hawana vitabu vya risiti.

Nikawauliza lini watakuwa navyo, hawajui lini watavipata.. Aibu kabisa.

Wakaniambia niende Kituo cha Urafiki Polisi nikaenda nao hawana. Wakaniambia niende Magomeni Polisi pale nao hamna receipt books.

Askari mmoja pale Magomeni akaniambia vituo vyote karibu vya Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni hawana vitabu vya risiti za malipo mpaka niende Central Polisi.

Mh Mwigulu upo hapa.. Hili jeshi limeoza kila sehemu!

Kamanda Simon Siro (RPC Dar)..Kamanda Susan Kaganda (RPC Kinondoni) hii aibu yote ya nini??

Sasa kweli kutakuwa na sababu gani ya msingi ya vituo vyetu vya polisi kutokuwa na Stakabadhi za Malipo ya serikali...!!??

Yani hili jeshi halina chochote cha kupigiwa mfano.. Kila uoza upo polisi..!!

Aibu kubwa sana kwa Jeshi la Polisi.
 
Umda haboob

Member
Aug 6, 2016
19
45
Sasa hapo ndugu yangu uozo wa polisi upo wapi? Kwani wao ndo wanazalisha vitabu vya risiti vya serikali? Mbona Uhamiaji walipokosa vitabu vya hati za kusafiria hukusema wameoza? Mimi nilidhani umechukuliwa pesa yako bila kupewa risiti kumbe wamekupa huduma waliokuwa na uwezo nao na kukueleza ukweli wa kile wasichoweza! Ungekuwa mstaarabu ungewaomba radhi polisi.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,456
2,000
Hivi makusany ya mwezi uliopita yalikuwa ni shilingi ngapi vile?

Hivi OC huko maofisini zipo?

Nauli za tu maana kila kitu kinahitaji fedha.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
10,840
2,000
Vitu vingine unaweza kulaumu Polisi kumbe tatizo liko hazina au mpigachapa wa serikali. Sidhani kama polisi wa DSM wanaweza kwa makusudi kuacha kuchukua vitabu hivi bohari kuu wakati wanajua vipo na vinahtajika kuhudumia wananchi. Kama polisi wetu(i.e. wahasibu wa polisi) wamefanya makusudi na kupelekea kukosekana vitabu hivi, basi kuna tatizo kubwa ndani ya Jeshi hili upande Wa uhasibu, otherwise sidhani kuwa ni sahihi kuwalaumu polisi hata kwa huduma ambazo wanatakiwa kutuhudumia baada ya wao kuwezeshwa na Idara nyingine. Polisi Dar naamini mmesikia kilio cha mtanzania huyu rekebisheni kama tatizo liko kwenu.
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,747
2,000
Habari Comrades..

Hii ni Aibu kabisa kwa Jeshi la Polisi kutokuwa na Receipt Books/ Stakabadhi za Malipo za serikali (zile za yellow) kwenye vituo vyake mbalimbali vilivyopo hapa DSM.

Malipo haya ya serikali hukusanywa pale mtu unapokwenda kwenye vituo vya polisi kuomba huduma kama ya kupotelewa (loss report) na nyaraka mbalimbali kama kadi za benki, vitambulisho, driving licence nk nk.

Leo nilikwenda kupata huduma hiyo pale kituo cha Mbezi kwa Yusuph nikaambiwa watanifungulia Taarifa tu ya kupotea kwa hivyo vitu vyangu lakini sitaweza kupata Loss Report maana hawana vitabu vya risiti.

Nikawauliza lini watakuwa navyo, hawajui lini watavipata.. Aibu kabisa.

Wakaniambia niende Kituo cha Urafiki Polisi nikaenda nao hawana. Wakaniambia niende Magomeni Polisi pale nao hamna receipt books.

Askari mmoja pale Magomeni akaniambia vituo vyote karibu vya Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni hawana vitabu vya risiti za malipo mpaka niende Central Polisi.

Mh Mwigulu upo hapa.. Hili jeshi limeoza kila sehemu!

Kamanda Simon Siro (RPC Dar)..Kamanda Susan Kaganda (RPC Kinondoni) hii aibu yote ya nini??

Sasa kweli kutakuwa na sababu gani ya msingi ya vituo vyetu vya polisi kutokuwa na Stakabadhi za Malipo ya serikali...!!??

Yani hili jeshi halina chochote cha kupigiwa mfano.. Kila uoza upo polisi..!!

Aibu kubwa sana kwa Jeshi la Polisi.
mkuu, wapo bize barabarani kukusanya hela wafikishe bajeti waliyopangiwa kwa December.
 
MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Oct 7, 2014
2,125

Kwanini usiseme aibu kwa serikali au unaogopa kufukuzwa uanachama?
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Kwanini usiseme aibu kwa serikali au unaogopa kufukuzwa uanachama?
Mimi si Mwanachama wa popote pale panapoweza kupelekea kufukuzwa kwa issue hii..
Na hata kama ningekuwa mwanachama popote pale, huwa sina nidhamu ya woga kwa mambo serious kama haya..
Kwa kusema ni aibu kwa Jeshi la Polisi it's obvious ni aibu kubwa kwa serikali ya CCM ya Awamu ya 5.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Vitu vingine unaweza kulaumu Polisi kumbe tatizo liko hazina au mpigachapa wa serikali. Sidhani kama polisi wa DSM wanaweza kwa makusudi kuacha kuchukua vitabu hivi bohari kuu wakati wanajua vipo na vinahtajika kuhudumia wananchi. Kama polisi wetu(i.e. wahasibu wa polisi) wamefanya makusudi na kupelekea kukosekana vitabu hivi, basi kuna tatizo kubwa ndani ya Jeshi hili upande Wa uhasibu, otherwise sidhani kuwa ni sahihi kuwalaumu polisi hata kwa huduma ambazo wanatakiwa kutuhudumia baada ya wao kuwezeshwa na Idara nyingine. Polisi Dar naamini mmesikia kilio cha mtanzania huyu rekebisheni kama tatizo liko kwenu.
Siwezi kulaumu hazina au bohari kuu maana Sijaenda huko Mkuu..
Nalaumu nilipoenda na kukuta huduma niliopaswa kuipata haipo ambapo ni Jeshi la Polisi.
 
Makoo

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
401
500
Nadhani tatizo litaisha soon kuna marekebisho na taratibu mpya zinafanyika.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Sasa hapo ndugu yangu uozo wa polisi upo wapi? Kwani wao ndo wanazalisha vitabu vya risiti vya serikali? Mbona Uhamiaji walipokosa vitabu vya hati za kusafiria hukusema wameoza? Mimi nilidhani umechukuliwa pesa yako bila kupewa risiti kumbe wamekupa huduma waliokuwa na uwezo nao na kukueleza ukweli wa kile wasichoweza! Ungekuwa mstaarabu ungewaomba radhi polisi.
Crap.
 
Kilwa94

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,920
2,000
Umekurupuka br..
Hivyo vitabu vinatolewa na serikali sawa!
So policie haina uozo kwa hilo.
Me@raiahuru tz.
 
dmketo

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
498
1,000
Siwezi kulaumu hazina au bohari kuu maana Sijaenda huko Mkuu..
Nalaumu nilipoenda na kukuta huduma niliopaswa kuipata haipo ambapo ni Jeshi la Polisi.
Mkuu naweza kukubaliana na wewe kwamba inawezekana kuna tatizo Fulani katika hivi vituo vyetu. Nimeona pale katika kituo cha Luguruni waendesha boda boda wakilipishwa fine wakishalipa pesa wanapewa ile karatasi ya notification bila risiti. Wakidai risiti wanaambiwa muhasibu hayupo na wengine wanatishiwa kuwekwa ndani wakidai risiti. Sijui kama zile pesa zinafika mahala husika. Kuna mapato ya Serikali yetu yanapotea kiholela sana.
 
Notification tu yenyewe inajitosheleza
Hakuna haja ya risiti
Me@raiahuru tz
 
dmketo

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
498
1,000
Notification tu yenyewe inajitosheleza
Hakuna haja ya risiti
Me@raiahuru tz
Inawezekana kweli ikawa inajitosheleza, je akitokea mtumishi asiye muaminifu akatumia mwanya huo kuwa na kitabu chake utajuaje mkuu? Bado nafikiri risiti ina umuhimu wake kwa muktadha huo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom