Aibu hii mpaka lini!!!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,891
Katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu hakuna shule ya umma hata moja iliyoingia top ten ifahamike kua idadi ya shule za serikali ni zaidi ya asilimia themanini ya shule zote nchini ni katika shule hizi ndiko wanasoma zaidi ya asilimia 90%ya watoto wa watanzania hasa maskini huku watoto wa matajiri na viongozi wetu wakisoma kwenye shule bora kabisa za binafsi zikiwa na kila kitu hata hivyo kuna utoto mwingi unaofanywa na wizara husika kwani badala ya kulitatua tatizo kwa kulikabili wanajaribu kuuzunguka mbuyu ikiwemo kuwatisha waalimu hasa ambao shule zao hazikufanya vizuri, kutoa motisha kwa wanafunzi waliofanya vizuri, kuzitambua shule zilizofanya vizuri, na upuuzi mwingine mwingi naita upuuzi kwa sababu siamini kua Kuna uhalali wowote kushindanisha shule za umma na shule binafsi alafu mshindi unampa zawadi unaiadhibu shule ambayo hujaipelekea waalim haina majengo hujaipelekea vitabu wala vifaa vya maabara ni dhahiri kua utakua unamhamasisha mkuu wa shule kuiba mtihani ili akuridhishe wewe au aondokane na aibu kwani ni dhahiri kua hakuna miujiza katika elimu napendekeza serikali iongeze uwekezaji kwenye elimu ndipo idai kwa nguvu matokeo ya uwekezaji wake vinginevyo kinachoendelea sasa ni kuwatisha tamaa watoto wa maskini ili wajipambanue kama wasio na akili
 
Unawezaje kusimamia kitu kikamilifu/kwa dhati kama hakikugusi
Watendaji wakuu wizara ya Elimu/Balaza la mitihani,na watumishi wengi wa umma watoto wao wanasoma ktk shule binafsi,
Swala la Elimu bure na bora ni kitendawili,
JMP toa tamko watumishi wote wa umma watoto wote katika ngazi Elimu ya msingi /o level lazima wasome shule za Goverment.
Utaona Elimu itapaa Tz.
 
Unawezaje kusimamia kitu kikamilifu/kwa dhati kama hakikugusi
Watendaji wakuu wizara ya Elimu/Balaza la mitihani,na watumishi wengi wa umma watoto wao wanasoma ktk shule binafsi,
Swala la Elimu bure na bora ni kitendawili,
JMP toa tamko watumishi wote wa umma watoto wote katika ngazi Elimu ya msingi /o level lazima wasome shule za Goverment.
Utaona Elimu itapaa Tz.
Hawez wake mwenyewe hawasomi huko........shule za kata ni kwajili ya mtaji wa kura za ccm....na private ndo za viongoz wa ccm wanajiandaa kuwa watawala
 
Sasa kama watoto wa wakubwa hawasomi shule hizo za serikali nani atakuwa nazo serious?
 
aibu hii mpaka pale watumishi wa umma na viongozi wakubwa wa serikali wawapeleke watoto wao shule za serikali ndipo aibu itaisha nje ya hapo aibu hii itatuvaa mpaka kaburini
 
Back
Top Bottom