Aibu Gani hii - ITV Television

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
Yaani nilikuwa naangalia kipindi cha mapishi mida mchache uliopita ,wakionyesha sijui wanaita Bif diana ,sasa kubwa ambalo niliona aibu wakati nikiwa na wageni zangu kutoka Ulaya tukiangalia ,aibu yenyewe ni jamaa ambae akiitwa akijijulisha kwa jina la Shefu Asha akisaga nyama ,aloo sauti iliyokuwa ikitokeza wakati akiigonga hiyo nyama utadhani wapo gereji ya magari ,ukiangalia kipande cha nyama akifiki ata robo kilo ,haya weka mbali kubwa ambalo ndio hapo niliona aibu ya aina yake ni kikaangio ,aloo kimechoka na hakina mkono, Nikawaza na kujisemea hawa watu wanafikiri hii Tv wanatazama peke yao,hivi hawaoni kama hizi Tv za hapa nchini zinatuwakilisha na wengine huwa tunajilabu ,yaani kwa hili la leo nimeona aibu kubwa sana na jamaa walitucheka,aloo kikaangio hakina mkono nafikiri mhusika na mtayarishaji inabidi wapewe onyo. Hebu waangalie vipindi vya nchi jirani waone ,vyombo vyao ni vipya kabisa ,yaani ni spesho kwa kuonyeshwa kwenye TV ,sasa hapa ITV mnaonyesha matangazo kienyeji .Nie vipi ?
 

Mwiba, nadhani huna zababu ya kuona aibu. Mbona hiyo ndiyo hali halisi ya waTZ wengi ... uswazi ni mwendo wa robo kilo na vikaangio visivyokuwa na mikono..
 
hakuna cha kuwashobokea watu wa ulaya wa nini, TV zetu sometime zinaboa! sasa kuonesha vyombo ambavyo ni vichafu na vibovu ndio maisha yetu! acheni huo ujinga msishabikie upumbavu unaooneshwa katika baadhi ya TV zetu kwa kisingizio cha ndio hali halisi ya mtanzania. Mbona mmebebea bango la zahma ya umeme kwanini msiseme ndio hali halisi ya serikali yetu! huo mfano tu!
 

usidandie gari kwa mbele...prove kwamba vyombo ni vichafu .... yawezekana macho yako na fikra zako ni chafu ndiyo maana mkaona vyombo ni vichafu ..... wewe hujui huyo mwiba anahubiri nini ..unacharuka
 
usidandie gari kwa mbele...prove kwamba vyombo ni vichafu .... yawezekana macho yako na fikra zako ni chafu ndiyo maana mkaona vyombo ni vichafu ..... wewe hujui huyo mwiba anahubiri nini ..unacharuka

Dah, bro we ni Prof wa chuo gani? Yani we ni bonge la greatthinker... Safi sana!
 

Yaani wewe ulitaka waonyeshe uzungu uzungu kwa sana, lazima tujitofautishe na wazungu na tutetee misimamo yetu, tena ingekuwa vema wangetumia chungu cha udongo na vitu vingine vya kiafrika. I love Afican cultures and I hate african who feel shy of thier cultures!
Mmesababisha hata baadhi ya dada zetu wanakataa ngozi za kiafrica,wengi wao ni kujichubua tu siku hizi
 
Ndo hapo. Hawajui kuweka soap. Ndo maana wengi wakiangalia movie au tamthilia za nje wanadhani nako vitu viko ivyo ivyo kwa kila mtu.
Kumbe ni njia ya kujipa sifa. Hii ni aibu kwa tv kufanya kitu kama hicho.
 
usidandie gari kwa mbele...prove kwamba vyombo ni vichafu .... yawezekana macho yako na fikra zako ni chafu ndiyo maana mkaona vyombo ni vichafu ..... wewe hujui huyo mwiba anahubiri nini ..unacharuka
Bro kama kipindi kilichoonyweshwa jana kuhusiana na upishi wa kipande cha nyama(Bief diana) ,nakuhakikishia vikaangio vilikuwa ni vya aibu yaani vinanikumbusha vile vijungu vya shamba ,visufuria vinang'ara katikati tu kulikobakia ni masinzi,kumbuka linalotimika ni gas coocker.

Aloo hii Tv inaonekana huko maulaya na ndugu zetu walio huko huwa na marafiki zao,mimi hapa Ngorongoro nilikuwa nimekaa na watalii,inakuwaje Kenya,Uganda Msumbiji na hata Sudani ,huwaga wanatumia vitu vipya,au unataka kusema ITV inashindwa kusponsa ,hicho kikaangio ?
 
tatizo lenu mkiangalia movie mnajua ndio maisha halisi,wengine hata hivyo vikaangio vilivyokatika mikono hawana:rain:
 

mwiba ..ninajua unachohubiri ....
 
Nafikiri mwiba na matajiri wako wa kizungu hakuelewa kipindi haikuwa beaf bali kiti motoz
 
Unatema Big G kwa karanga za kuonja mwana JF, Hapa ni home hukuwa na sababu ya kuona aib kwani Donkey hata umpake rangi waezi kuwa zebra, Meza hiyo alafu huenda hao jamaa walifurahi kuona kitu live then wewe ukahisi wanakucheka.
 

Asante angeweza kubadili channel ili kuepuka fedheha, Hikua lazima sana yeye kuangalia!
Halipii chochote na wala hao wazungu au wagen wake wanatoa nini!
 
acha hizo mazee uliona aibu kisa umekaa na wadosi, unawashobokea wadosi sana ee! ningekuona wamaana kama ungekoment jinsi nafsi yako binafsi ilivyochukizwa na hilo tukio sio kwa kuwa ulikaa na wadosi.
 
Inabidi uone aibu kwakuona aibu... hayo ndo maisha yetu watanzania... haina haja ya kuonyesha vyombo vipyaaa ambavyo katika hali halisi havitumiki... Eti kisa wazungu!? Ah!..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…