Aibu, fedhea ya DART, Jiji, Manispa Dar

inasikitisha sana mle kwenye basi pale mlangoni pameandikwa "no standing zone" lakini watu wanasimama hapohapo na wakati basi wala halina watu wengi....watz ni matatizo.
 
inasikitisha sana mle kwenye basi pale mlangoni pameandikwa "no standing zone" lakini watu wanasimama hapohapo na wakati basi wala halina watu wengi....watz ni matatizo.
hahahahah,labda hawaelewi ,walitakiwa waandike kiswahili
 
Jamani leo nimepanda ukitoa buku wanasema hawana chenji kuweni makini wanakusanya pesa nyingi tena wanasema km hutaki basi nenda..leo nimeacha 350 pale nauli posta hadi ubungo 650
 
Jamani leo nimepanda ukitoa buku wanasema hawana chenji kuweni makini wanakusanya pesa nyingi tena wanasema km hutaki basi nenda..leo nimeacha 350 pale nauli posta hadi ubungo 650

wenzako tulikomaa pale ubungo hadi chenji zikaletwa huduma ikaendelea...pole mkuu kwa kusafiri kwa buku.
 
Hili lakini ni la kulaumu watumiaji hivyo vituo na vyoo. Kwanini wachafue ovyo? Kwani hakuna maji? UDART wanatakiwa kuweka watu wa usafi kila kituo. Nadhani haya ni matokeo ya poor planning. Kwanini waliweka vyoo halafu suala la usafi halikufikiriwa? Ni nani anavisimamia hivyo vituo? Serikali au UDART? Anayesimamia ana wajibu pia kuhakikisha vituo ni visafi. Hii ni aibu kwa Taifa!!! Vituo hata havijamaliza wiki mbili toka vianze vinanuka!!!!!
 
Mleta uzi kijana Mwampamba hakuna siasa chafu za majitaka hapa? Kimtazamo umeona na kutaarifu bila kutoa njia ya nini kifanyike. Hii ni siasa tena chafu kwelikweli inayofanywa na kuasisiwa au na wewe mwenyewe na wanaokufadhili ili kuuonyesha umma kuwa upinzani hawafai kuongoza. Ni wazo haribifu na lisilojenga. Je, ni wapinzani wanaopanda hayo mabasi peke yao? Ni kwanini basi usingeshauri watumiaji wa vituo hivyo kuwa wastaarabu na wasafi ili kudumisha lile la mkuu wa mkoa la kulifanya jiji letu kuwa safi muda wote?
Binafsi siiafiki njia ya kulaumu bila kutoa njia mbadala. Watu wapewe elimu na ikibidi wahusika waweke mabango na matangazo ya kuhimiza usafi na ikibidi vituo vya redio, tv na magazeti yahusishwe kutoa elimu hiyo kwani watu wote waliopo Dar wanatumia usafiri huu na vituo hivyo bila kujali itikadi zao. Ondoeni na acheni kuwawekea siasa za matopeni wananchi kwa kujiona ninyi mliokosa fursa ya kuliongoza jiji mlifaa zaidi. Bila kubadili mindset zenu hakuna litalofanyika la maendeleo zaidi ya kukwazana tu tena kijinga hivi.
Nimewaza kwa sauti kuu ili na wewe uje na njia mbadala tusilaumu tu!!!!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…