Aibu, fedhea ya DART, Jiji, Manispa Dar

Aibu, fedhea ya DART, Jiji, Manispa Dar

Yaani sisi bado sana kwa kweli,utajisaidiaje kwenye kituo cha basi jamani,kabla ya vituo hivyo walikuwa wanajisaidia wapi?ila pia inatakiwa kuwe na wafanya usafi,ila jamani waweke ulinzi ili watu wasijisadie kabisa,yaani sisi watu weusi bila viboko ni sio wastaarabu hata kidogo
inasikitisha sana mle kwenye basi pale mlangoni pameandikwa "no standing zone" lakini watu wanasimama hapohapo na wakati basi wala halina watu wengi....watz ni matatizo.
 
hahahahah,labda hawaelewi ,walitakiwa waandike kiswahili
 
Jamani leo nimepanda ukitoa buku wanasema hawana chenji kuweni makini wanakusanya pesa nyingi tena wanasema km hutaki basi nenda..leo nimeacha 350 pale nauli posta hadi ubungo 650
 
wenzako tulikomaa pale ubungo hadi chenji zikaletwa huduma ikaendelea...pole mkuu kwa kusafiri kwa buku.
 
Ikiwa ni siku tano kupita baada ya mabasi ya mwendo kasi kuanza kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam, hali ya vituo vyake inatisha

Baadhi ya vituo hivyo vinatoa harufu kali, vimeenea mikojo, kinyesi na takataka ngumu ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa husika vimedai kutohusika na usafi wake.

Miongoni mwa vituo alivyotembelea mwandishi wa habari hii ni pamoja na Moroco (Kinondoni), Kinondoni B, Manyanya na Kimara Baruti ambapo vituo hivyo vimekuwa na hali inayotia shaka usalama wa abiria wanaotumia vituo hivyo kusubiri usafiri.

Gatson Makwembe, msemaji wa Jiji alipoulizwa kuhusu ufuatiliaji wa usafi kwenye vituo hivyo baada ya hali kuwa mbaya, amedai jiji halihusiki.

“Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo kwani sisi halituhusu labda uwatafute DART au Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni,” amesema Makwembe.

Sebastian Mhowera, Ofisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni alipoulizwa, alidai kazi ya Manispaa ya Kinondoni ni kusimamia usafi wa barabarani pekee.

“Sisi kazi yetu ni kusimamia usafi barabarani ndani ya manspaa hii na sio uchafu uliopo ndani ya vituo vya mabasi ya UDA. Siwezi kuzungumzia uchafu uliopo kwenye nyumba ya jirani,” amesema.

Alipotafutwa William Gatambi, Msemaji wa Kampuni ya DART inayosimamia UDA hakupatikana kujibu aliye na dhamana ya kufanya usafi kwenye vituo hivyo.

Hali ya wasiwasi inaendelea kutawala kwa wananchi kutokana na vituo hivyo kuwa na hali mbaya, kukosa ulinzi na hata kugeuka kuwa maeneo ya vibaka, mateja na watoto wa mitaani kupata hifadhi ya usingizi.

Kituo cha Kimara Baruti kimekuwa na mlundikano mkubwa wa watu, harufu mbaya inayotokana na kinyesi, mkojo huku mwingine ukiwa umefungwa kwenye chupa za maji na kutupwa hovyo. Uchafu wa kituo hicho unafanana na vituo vingine.

John Mgonja, mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri usafiri katika Kituo cha Moroco ameeleza kushangazwa na huduma mbovu za vituo hivyo.

“Kwanini vituo havina ulinzi, hakuna maji, sakafu chafu, taka ngumu kila mahali na harufu mbaya mpaka imekuwa kero.

“Sijui sisi tuna tatizo gani, hivi haya mambo yote hayakuwa kwenye mpango wao. Wao wanachojua ni kukusanya fedha kwa ajili ya nauli tu?” amehoji Mgonja.

Amesema, watu wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa, kama amebanwa na haja na vyoo vipo kwake anaona ni bora kikudhi haja yake kwanza mengine mbele kwa mbele.

“Sasa kama umefika hapa na umebanwa kwanini usijisaidie, lakini hata kama utaacha vyoo vichafu nani atakukamata? Hakuna mlinzi na hakuna usalama wowote,” amesema.
Hili lakini ni la kulaumu watumiaji hivyo vituo na vyoo. Kwanini wachafue ovyo? Kwani hakuna maji? UDART wanatakiwa kuweka watu wa usafi kila kituo. Nadhani haya ni matokeo ya poor planning. Kwanini waliweka vyoo halafu suala la usafi halikufikiriwa? Ni nani anavisimamia hivyo vituo? Serikali au UDART? Anayesimamia ana wajibu pia kuhakikisha vituo ni visafi. Hii ni aibu kwa Taifa!!! Vituo hata havijamaliza wiki mbili toka vianze vinanuka!!!!!
 
Mleta uzi kijana Mwampamba hakuna siasa chafu za majitaka hapa? Kimtazamo umeona na kutaarifu bila kutoa njia ya nini kifanyike. Hii ni siasa tena chafu kwelikweli inayofanywa na kuasisiwa au na wewe mwenyewe na wanaokufadhili ili kuuonyesha umma kuwa upinzani hawafai kuongoza. Ni wazo haribifu na lisilojenga. Je, ni wapinzani wanaopanda hayo mabasi peke yao? Ni kwanini basi usingeshauri watumiaji wa vituo hivyo kuwa wastaarabu na wasafi ili kudumisha lile la mkuu wa mkoa la kulifanya jiji letu kuwa safi muda wote?
Binafsi siiafiki njia ya kulaumu bila kutoa njia mbadala. Watu wapewe elimu na ikibidi wahusika waweke mabango na matangazo ya kuhimiza usafi na ikibidi vituo vya redio, tv na magazeti yahusishwe kutoa elimu hiyo kwani watu wote waliopo Dar wanatumia usafiri huu na vituo hivyo bila kujali itikadi zao. Ondoeni na acheni kuwawekea siasa za matopeni wananchi kwa kujiona ninyi mliokosa fursa ya kuliongoza jiji mlifaa zaidi. Bila kubadili mindset zenu hakuna litalofanyika la maendeleo zaidi ya kukwazana tu tena kijinga hivi.
Nimewaza kwa sauti kuu ili na wewe uje na njia mbadala tusilaumu tu!!!!
 
Ikiwa ni siku tano kupita baada ya mabasi ya mwendo kasi kuanza kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam, hali ya vituo vyake inatisha

Baadhi ya vituo hivyo vinatoa harufu kali, vimeenea mikojo, kinyesi na takataka ngumu ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa husika vimedai kutohusika na usafi wake.

Miongoni mwa vituo alivyotembelea mwandishi wa habari hii ni pamoja na Moroco (Kinondoni), Kinondoni B, Manyanya na Kimara Baruti ambapo vituo hivyo vimekuwa na hali inayotia shaka usalama wa abiria wanaotumia vituo hivyo kusubiri usafiri.

Gatson Makwembe, msemaji wa Jiji alipoulizwa kuhusu ufuatiliaji wa usafi kwenye vituo hivyo baada ya hali kuwa mbaya, amedai jiji halihusiki.

“Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo kwani sisi halituhusu labda uwatafute DART au Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni,” amesema Makwembe.

Maendeleo ni mchakato ambao una stages nyingi za kukua. Kila stage moja hutegemea nyingine. Ni dhahiri kwamba kuna vitu vingine watanzania tunarushwa stages na hivyo kutuletea usumbufu mkubwa sana kwani hatujajiandaa kuingia stage ambayo muda wake haujafika. Tutarudi tu kwenye stage ambayo ni muafaka mpaka tu- graduate

Back
Top Bottom