kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,676
MKAZI wa kijiji cha Kidamali, Joseph Balami juzi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu kanda ya Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Stani Singaile (42) kwa makusudi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Balami alitenda kosa hilo Oktoba 15, 2011 katika kijiji cha Kidamali, Wilayani Iringa, mkoani hapa.
Akisoma hukumu hiyo kwa saa mbili, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Iringa, Mary Shangali alisema amekubaliana na ushahidi uliotolewa kwamba pasipo shaka mtuhumuwa alitenda kosa hilo.
“Kwenye kesi hii upande wa mashitaka ulileta mashihidi watano na upande wa utetezi ulileta mashahidi wawili ambao ni mtuhumiwa mwenywe na mke wake," alisema Jaji Shangali.
"Mahakama imekubaliana na upande wa mashitaka kuwa mtuhumuwa ametenda kosa na imemtia hatiani kwa kosa la kuua kwa makusudi.
"Kwa kuwa adhabu inayotolewa kwa kosa hilo ni moja kwa mjibu wa sheria... ninakuhukumu kunyongwa hadi kufa.”
Kabla ya hukumu kusomwa, wakili wa serilali Felix Chakela aliitaka mahakama kumpa adhabu kali mtuhumiwa ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo wakati.
Wakili wa utetezi, Chakela Lwezaula alisema yeye anasubiri hukumu ya mahakama.
Jaji huyo asema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 15, katika kilabu cha pombe za kienyeji.
Alisema mashahidi wa mashitaka wamethibitisha bila kuacha shaka kuwa siku hiyo mtuhumiwa alikwenda kwenye kilabu hicho kumfuata marehemu kisha kumchoma na kisu kifuani.
Alisema kitendo cha mtu kumfuata mtu na kumchoma kisu kifuani, hususani upande wa kushoto kinaonyesha alidhamiria kuua na kwamba kwa kitendo hicho, mahakama inamtia hatini kwa kosa la mauaji ya kukusudia.
Pia alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa pamoja na maoni yaliyotolewa na waungwana wa mahakama, yanakubaliana kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukuacha shaka kwa mtuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Balami anadaiwa kuwa katika kijiji cha Kidamali Wilaya ya Iringa majira ya saa moja usiku, alimuua Singaile kwa kumchoma na kisu wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.
Ilidawa mahakamani hapo kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia, lakini alikamatwa saa mbili usiku na kufikishwa kwenye ofisi ya serikali ya kijiji na baadae katika kituo cha polisi kwa hatua zaidi.
Chanzo: NIPASHE