Ni takribani miezi miwili imepita tangu nilipoomba ushauri wa kitabibu pindi nilipopatwa na tatizo la Bawasili. Kwa hivi sasa nimepona kabisa lakini nitakuwa si mwingi wa fadhila kama sitafanya yafuatayo;
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali niliyofikia hivi sasa.
Pili nasema ahsante kwa jamii nzima ya JF kwa msaada wa mawazo na ushauri wa kitabibu kuhusiana na tatizo lililokuwa likinisumbua.
Ushauri na maelezo ya kitaalamu kuhusiana na ugonjwa huu niliyopata humu jamvini vilinisaidia sana kwanza kulijua tatizo kiundani.
Tatu kulikubali tatizo
Nne kuliona tatizo hili kuwa linatibika kwa tiba mbalimbali kama zilivyoelezewa na wanajamvi mbalimbali hapa JF.
Sina cha kuwalipa lakini narudia kusema AHSANTENI, NIMEPONA.
Mungu azibariki kazi za mikono yenu.