Ahsante Rais Samia kwa Elimu Bure kidato cha 5 na 6

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,123
7,709
Kwa mwendo huu na kasi ya Mhe. Rais Mama Samia nimekubali kweli kwenye kasi ya kuleta maendeleo kwa wananchi Mama SSH na Hayati JPM ni kitu kimoja.

Ndani ya mwaka mmoja tumeshuhudia kasi ya mendeleo ktk kila kona ya nchi yetu, kaifungua nchi ndani na nje.

Kama haitoshi katika kuboresha zaidi elimu mwaka huu katangaza elimu Bure kidato cha tano na cha sita, ahsante sana Rais.

Kwa mara ya kwanza tangu uhuru tumeshuhudia madarasa yenye hadhi ya ulaya kwa fedha za uviko 19, ahsante sana Rais.

Mabilioni ya fedha yametolewa kwenye ujenzi wa barabara za mijini na vijijini TARURA.

Miradi ya ujenzi wa barabara inaendelea kila kona ya nchi hii, fedha zimemwagwa kila kona.

Mama ni mkali kwenye matumizi ya ovyo ya fedha za umma, ukitaka uzijue rangi zake zote wewe jaribu kufuja fedha za umma halafu utaona utakavyo ungua hadi mifupa.

Fedha zimemwagwa kila jimbo, ruzuku za kilkmo, madai ya watumishi, n.k

Vituo vya afya, maji vimeboreshwa zaidi.

Kwakweli mambo ni mengi mengi mazuri sana

Ahadi yetu sisi wananchi ni kuzidi kumuombea Mungu amlinde na amtunze Rais wetu.

Ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu, mwenye huruma, asiye penda kujilimbikizia mali kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi wanao pata nafasi basi huanza kujikusanyia wao na ndugu zao, sio kwa Mama. ni kiongozi wa kipekee asiye na majivuno wala majigambo. ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine.
Mungu mbariki Rais wetu Mama Samia Hasani.

Ushauri kwa Waziri wa Elimu;
Hakikisha unatumia maarifa yako yote wewe pamoja na wasaidizi wako ktk elimu wanaboresha Elimu kwa shule zote za Serikali, kwani shule hizi ndio kimbilio la watanzania walio wengi na wasio na uwezo wa kipato hivyo wanayo Haki kabisa ya kupata elimu bora.
Tuboreshe elimu yetu kwa kuajiri walimu na wataalamu wenye sifa na uwezo wa hali ya juu.

Kazi iendelee..........
 
Sipingi elimu kuwa bure, ila kuna muda inabidi tujitathimini hatujafikia uchumi huo ni bora huduma za afya zikawa bure ila elimu
 
Mengine ni sifa tu unawapa, hayo ni majukumu ya serikali kuleta maendeleo kwa wananchi kutokana na uhitaji.
 
sawa kabisa lkn kuna baadhi ya viongozi huwa wanashindwa kutimiza wajibu wao,

mfano kuna hata baadhi ya wazazi hushindwa kutimiza wajibu wao wa kuwahudumia watoto wake mwenyewe hata kama anao uwezo wa kifedha na akishia kutumbua starehe na wangine!!

sasa unapo pata kiongozi mwenye kujali shida za wananchi wake na kuzitatua basi huyo ni kiongozi bora na ni neema kutoka kwa Mungu.

Tumshukuru Mungu kwa neema aliyetupa ya kuwa na Rais Mama Samia.
tuache chuki pembeni.
 
kwa mwendo huu na kasi ya Mhe. Rais Mama Samia nimekubali kweli kwenye kasi ya kuleta maendeleo kwa wananchi Mama SSH na Hayati JPM ni kitu kimoja.

ndani ya mwaka mmoja tumeshuhudia kasi ya mendeleo ktk kila kona ya nchi yetu, kaifungua nchi ndani na nje.

kama haitoshi katika kuboresha zaidi elimu mwaka huu katangaza elimu Bure kidato cha tano na cha sita, ahsante sana Rais.

Kwa mara ya kwanza tangu uhuru tumeshuhudia madarasa yenye hadhi ya ulaya kwa fedha za uviko 19, ahsante sana Rais.

Mabilioni ya fedha yametolewa kwenye ujenzi wa barabara za mijini na vijijini TARURA.

Miradi ya ujenzi wa barabara inaendelea kila kona ya nchi hii, fedha zimemwagwa kila kona.

Mama ni mkali kwenye matumizi ya ovyo ya fedha za umma, ukitaka uzijue rangi zake zote wewe jaribu kufuja fedha za umma halafu utaona utakavyo ungua hadi mifupa.

Fedha zimemwagwa kila jimbo, ruzuku za kilkmo, madai ya watumishi, n.k

vituo vya afya, maji vimeboreshwa zaidi.

kwakweli mambo ni mengi mengi mazuri sana

Ahadi yetu sisi wananchi ni kuzidi kumuombea Mungu amlinde na amtunze Rais wetu.

Ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu, mwenye huruma, asiye penda kujilimbikizia mali kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi wanao pata nafasi basi huanza kujikusanyia wao na ndugu zao, sio kwa Mama. ni kiongozi wa kipekee asiye na majivuno wala majigambo. ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine.
Mungu mbariki Rais wetu Mama Samia Hasani.

Ushauri kwa Waziri wa Elimu;
Hakikisha unatumia maarifa yako yote wewe pamoja na wasaidizi wako ktk elimu wanaboresha Elimu kwa shule zote za Serikali, kwani shule hizi ndio kimbilio la watanzania walio wengi na wasio na uwezo wa kipato hivyo wanayo Haki kabisa ya kupata elimu bora.
Tuboreshe elimu yetu kwa kuajiri walimu na wataalamu wenye sifa na uwezo wa hali ya juu.

kazi iendelee..........
Kwa wenzetu wenye uelewa mzuri, wananchi na wabunge wao huihoji serikali ifafanue kiwango cha elimu itakayotolewa, gharama zake na itakakotoa pesa za kulipia mahitaji ya hiyo elimu ya “bure”. Kama serikali itafanya “adjust” katika bajeti basi ieleze itapunguza wapi/mradi gani/huduma ipi kupata hizo pesa. Athari zipi zitajitokeza. Huo huwa mjadala bungeni kabla pendekezo halijakubalika.

Wanajua serikali haina pesa za kuamua kutoa fadhila nje ya mapato yake rasmi (kodi/mikopo/misaada). Hapa kwetu huwa tunamshangilia tu Rais kama kwamba ni tajiri mmoja hivi mwenye huruma kwa wananchi wake kama vile hatujui kuwa zote tunahusika kinamna na gharama hizo.

Marekani Obama alipopendekeza bima ya afya kwa wote (Obamacare) alipambana na mjadala mkali kuhusu athari kubwa ya gharama za kuwezesha mpango huo. Hapa kwetu isingeeleweka: Rais ametuletea bima ya bure kwa wote halafu kuna watu wanapinga?
 
Mengine ni sifa tu unawapa, hayo ni majukumu ya serikali kuleta maendeleo kwa wananchi kutokana na uhitaji.
Tena wasichokijua ni kwamba wanalipwa kila mwezi na kupewa motisha kibao ili wawaletee wananchi hizo huduma..
 
Hii idea ilikuwa ya Wapinzani,

Nakumbuka wakati wa campaign ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka ule wa 2015 if not mistaken.

Mojawapo ya faida ya kuwa na vyama vingi nchini ni mambo kama haya.
 
Sasa kwenye utekelezaji,

Je Shule zitaongezewa ruzuku ya uendeshaji maradufu?

Je haitapelekea wazazi kukamuliwa michango chungunzima ?
 
Mnawachanganya wazazi kwa makusudi, sijui mnapata nini. Ni elimu bila Ada, sio elimu bure, michango yote ipo palepale na wazazi wanaendelea kutoa, Ada ilikuwa na 70,000 kwa mwaka, lakini michango inafika karibu 270,000. Bado hatujui Kama Ada ya mtihani imefutwa!!

Ile ya O level ni elimu bure kwa maana michango yote ilifutwa, kuna waliotumbuliwa kwa kutoza michango wanafunzi
 
Iyo Elimu ya bure ndyo inazalisha vijana wa hovyo kama ww ulieleta mada, Elimu icyokua na msaada wowote kwa mwanafunzi akimaliza iyo form6 anaishia kua CHAWA hta kwenye soko la ajira ataonekana kituko na iyo Elimu
 
kwa mwendo huu na kasi ya Mhe. Rais Mama Samia nimekubali kweli kwenye kasi ya kuleta maendeleo kwa wananchi Mama SSH na Hayati JPM ni kitu kimoja.

ndani ya mwaka mmoja tumeshuhudia kasi ya mendeleo ktk kila kona ya nchi yetu, kaifungua nchi ndani na nje.

kama haitoshi katika kuboresha zaidi elimu mwaka huu katangaza elimu Bure kidato cha tano na cha sita, ahsante sana Rais.

Kwa mara ya kwanza tangu uhuru tumeshuhudia madarasa yenye hadhi ya ulaya kwa fedha za uviko 19, ahsante sana Rais.

Mabilioni ya fedha yametolewa kwenye ujenzi wa barabara za mijini na vijijini TARURA.

Miradi ya ujenzi wa barabara inaendelea kila kona ya nchi hii, fedha zimemwagwa kila kona.

Mama ni mkali kwenye matumizi ya ovyo ya fedha za umma, ukitaka uzijue rangi zake zote wewe jaribu kufuja fedha za umma halafu utaona utakavyo ungua hadi mifupa.

Fedha zimemwagwa kila jimbo, ruzuku za kilkmo, madai ya watumishi, n.k

vituo vya afya, maji vimeboreshwa zaidi.

kwakweli mambo ni mengi mengi mazuri sana

Ahadi yetu sisi wananchi ni kuzidi kumuombea Mungu amlinde na amtunze Rais wetu.

Ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu, mwenye huruma, asiye penda kujilimbikizia mali kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi wanao pata nafasi basi huanza kujikusanyia wao na ndugu zao, sio kwa Mama. ni kiongozi wa kipekee asiye na majivuno wala majigambo. ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine.
Mungu mbariki Rais wetu Mama Samia Hasani.

Ushauri kwa Waziri wa Elimu;
Hakikisha unatumia maarifa yako yote wewe pamoja na wasaidizi wako ktk elimu wanaboresha Elimu kwa shule zote za Serikali, kwani shule hizi ndio kimbilio la watanzania walio wengi na wasio na uwezo wa kipato hivyo wanayo Haki kabisa ya kupata elimu bora.
Tuboreshe elimu yetu kwa kuajiri walimu na wataalamu wenye sifa na uwezo wa hali ya juu.

kazi iendelee..........
Ndo umeandika utopolo gani huu mkuu.
 
Mnawachanganya wazazi kwa makusudi, sijui mnapata nini. Ni elimu bila Ada, sio elimu bure, michango yote ipo palepale na wazazi wanaendelea kutoa, Ada ilikuwa na 70,000 kwa mwaka, lakini michango inafika karibu 270,000. Bado hatujui Kama Ada ya mtihani imefutwa!!

Ile ya O level ni elimu bure kwa maana michango yote ilifutwa, kuna waliotumbuliwa kwa kutoza michango wanafunzi
Hatari
 
Back
Top Bottom