Ahsante JF.

Ahsante JF.

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Ninachukua nafasi hii kuwashukuru watendaji na waanzilishi wa huu mtandao wa kijamii unao tuma fursa sisi wananchi kueleza hisia na mawazo yetu kwa viongozi kwa uwazi.!

Pili namshukuru Mh Rais John Joseph Pombe Magufuli kww kusoma maoni yetu awali aliposema huwa anapata fursa ya kusoma vinavyojadiliwa humu nilikuwa siamini sana..
lakini baada ya hoja zangu mbili nilizowahi zitoa hapa ndani kuona zikizungumziwa na Mh Rais nimeona thamani ya mchango wangu kwa jamii yangu.

1: nilileta hoja ya kubadirisha tozo ushuru wa barabara Road licence kutoka ule mfumo wa awali wa TRA na kuwekwa kwenye mafuta..
baada ya wiki kadhaa nikasikia wazo lile likifanyiwa kazi..

2: nilileta wazo la kuanzisha utaratibu wa sare za wanafunzi na watumishi wa umma kushonwa hapa hapa Tanzania kwa kutumia material na teknolojia tuliyo nayo.!

Jana wakati Mh Rais akizungumza na wafanyabiashara nimemsikia akigusia suala hili. Ki ukweli nimesikia faraja sana.

Yamkini mimi sio wa mwanzo kuwa na mawazo kama hayo au hoja hizo .
lakini mimi kuwa miongoni mwa wale wanaolitakia mema Taifa hili na Mh Rais akaona uzito wa mawazo yetu!
Najisikia kutimiza wajibu wangu kama MTANZANIA.
ahsante Jf.
 
Tutamuelewa tu Mh. Rais. Ahsante pia kwa kutuletea mrejesho na kutukumbusha wajibu wetu Kama Watanzania wenye akili timamu na Busara. URAIS ni taasisi, heshima kwa kwa taasisi hiyo ni wajibu wa kila MTANZANIA mwenye nia njema na Taifa letu.
 
Back
Top Bottom