Ahsante JF kuwa chuo kikuu bora kwangu

HFOOO

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
683
643
Bwana Yesu asifiwe wale wa Imani moja pamoja nami,shikamoni wakubwa zangu baba zangu ,dada zangu na kaka zangu, kwa wale wa rika langu habari zeni na mambo zenu vipi?

Natumaini kila mmoja wetu humu ndani huwa anajisikia furaha na faraja kubwa sana aingiapo humu jf kama ambavyo mimi tangu nijiunge humu jf sijawahi juta.

Naomba moja kwa moja kwenda kwenye mada kama ambavyo nimeitambulisha hapo juu kuwa jf ni chuo kikuu bora kwangu.

Naomba samahani wote humu ndani huenda sijui kupangilia sentensi vizuri na huenda ukasoma ukakwazika nakuomba nivumilie na chukua mda wako kunielekeza vizuri ili nami siku moja niwe mwalimu mzuri Zaidi yako.


Leo natimiza mwaka mmoja tangu kujiunga na JF na nimekuja mbele yenu leo ndugu zangu wote tuliopo humu ndani, ni siku ambayo nina furaha kubwa na Amani ya kutosha licha ya changamoto za hapa na pale, niyanayo mamneno mengi sana ambayo nimetamani kujiweka wazi kuwa moja kati ya vitu mimi nimejifunza hapa Jf na kujiona kuwa jf mda mwingine ni Zaidi ya chuo kikuu. Wakati najiunga na JF nilipata kuambiwa na moja Rafiki zangu kuwa kama unataka elimu ya bure alafu ni kubwa kuzidi hata ile ile inayotolewa chuoni na kuna elimu zingine huwezi kuzipata kwenye chuo chochote kamwe.

Niliamua kuchukua hatua na kujiunga humu ndani kisha nikaanza kupitia baadhii ya nyuzi na watoaji wa hizi nyuzi nikapitia nikasoma na kuna nyuzi zingine nikazitendea kazi na nikapata faida na zikaniletea matokeo mazuri na chanya maishani mwangu.


mfano:1. moja kati ya kitu nilikisoma na kukielewa vizuri na nikakiingiza kichwani mwangu na kujiongeza kwa akili zangu za kuzaliwa na nikaona matokeo mazuri na chanya ni Maisha ya shushushu ni mtu wa aina gani na muonekano wake na hata kama akijaribu kuishi Maisha ambayo sio uhalisia wake na kuweza kumtambua kwa haraka, hili nimefanikiwa sana. Nina Zaidi ya watu tisa walipokuwa kwenye shughuli zao za kawaida niliweza kuwajua vizuri sana mpaka ikanipelekea mmoja wao baada ya kumbana vizuri na maswali yaliyo na kona nyingi alijikuta amejiweka wazi lakini hakuishia hapo aliniomba nami nimweleze ukweli huenda nami ni mwanzake lakini kwa hilo alifeli kwa sababau mimi ni raia wa kawaida tu, hadi ,leo huwa haniamini kabisa hata nikimwambia naenda safari huwa ananiambia maneno ambayo huwa anamaanisha kuniona nami ni mmojawapo.

2.Kumtambua mtu hatari na ambaye anataka kusababisha machafuko eneo Fulani kwa hili nako nimejiona kuwa jf imenipa shule kubwa mnoo nimekatisha Zaidi ya watu hao hatari 20 mpaka sasa hadi imefikia mmoja nilimbana kanisani kwetu ninakoabudia baada ya kutoa taarifa police mpaka leo police wanjua kabisa kuwa mimi ni mtu wa idara lakini ukweli wangu ni kwamba haya yote nimejifunzia JF.

3.Kuzijua baadhi ya kanuni na sharia mbali mbali na kuitambua haki yangu na kuonesha nidhamu pale ninapotambua kuwa kweli hapa nimekosea na kuonyesha ukakamavu pale ninapoona nipo sawa na sharia hijanigusa au kunitia hatiani.Mwaka jana nilikamatwa na maafisa wa uhamiaji na kuambiwa kuwa wana mashaka na utaifa wangu kwa sababu ya sura umbo kidogo alinifannanisha na watu wa taifa Fulani jirani, na sikuwa na id yeyote ambayo ingeweza kunisaidia kujieleza kwao na kuwaonyesha na wao waamini, lakini nilitumia elimu ya jf na kujieleza vizuri mpaka mkuu wao akabaki amepigwa putwaa kuwa wewe ulijuwaje kuwa tunahitaji kupata maelezo kama haya kwa mtu ambaye tumekushukia ? nilimjibu kuwa Mungu amenijalia kunipa hekima hii ndipo akasema wewe sio kawaida inawezekana ni afisa Fulani ila umetuzuga tu ila nenda zako tunakupa na nauli, kwa kukamatwa nimekamatwa kama mara 4 hivi lakini ukweli mimi ni mtu wa kanda ya kati ambapo hakuna hata chembe ya uhusiano hata kidogo na watu wa taifa lile.

4. Baadhi ya haya na mengineyo mengi sana ambayo ningeandika humu naweza tumia hata wiki nzima bila kumaliza kuelezea ambayo yamenipa faida humu ndani kwenye majukwaa yote yaliyoko Jf.


BAADHI YA MAMBO AMBAYO SITAWEZA KUYAFANYA HAPA JF HATA UNILAZIMISHE VIPI

1.
JF KUNA TABIA YA WATU KUJIBU VIBAYA YAANI HATA KAMA JAMBO LINAELEWEKA VIPI YEYE AKISOMA TU ANISHIA KUJIBU KWA KEJELI AU KUTUKANA,MIMI KAMA MIMISITAKUWA TAYARI KWA NAMNA YEYOTE ILE SABABU SIKUJIUNGA JF KWA KUJA KUTOA LUGHA MBOVU AU MATUSI NIMEJIUNGA ILI KUJIFUNZA YALE NISIOYAJUA

2.UBISHI KWANGU MWIKO
3.KAMA KUNA UZI SIJAUELEWA SIWEZI KOMENTI CHOCHOTE
4.SITAWEZA KUJIBU TOFAUTI NA MAADADA


Mwisho kabisa naomba kuwaambia wale ambao wao kila nyuzi hawazielewi na wanaishia kukomenti ovyo wakati elimu yao ni chet ili hali wenye PHD wameelewa na kutoa majibu mazuri pia watu hao huwa sipati shida nao kwea sababu najua shida ni elimu yao. Kuna mtu hapa naomba kama nitakuwa nimekosea kukutaja hapa nisamehe kaka yangu JR MSHANA kaka Mungu akubariki sana hekima yako na nidhamu yako ndio nahisi imekufikisha hapo ulipo shule nyingi hapa Jf nimetoa kwako,Ubarikiwe hadi ushangae
 
Hata mimi mara ya kwanza nilipoona ID yako, nilidhani wewe ni mtu wa Idara fulani.
 
Ukitaka kuoa mwanamke JF uwe umemzidi kwa kila kitu. Pesa, Elimu na Mali. Hapo sawa. Otherwise Do not.

Unajua JF ni kama Dunia nyingine tofauti na unayoishi ww mtaani kwako. Hata ukilala Njaa as long as ww ni mwana JF try to feel proud of IT.

Maisha ya wana JF ni expensive sana.
hahahahahaha mkuu dada zetu humu wana majibu makubwaaaaa
 
Ukitaka kuoa mwanamke JF uwe umemzidi kwa kila kitu. Pesa, Elimu na Mali. Hapo sawa. Otherwise Do not.

Unajua JF ni kama Dunia nyingine tofauti na unayoishi ww mtaani kwako. Hata ukilala Njaa as long as ww ni mwana JF try to feel proud of IT.

Maisha ya wana JF ni expensive sana.
hapo umenena mkuu ngoja nimtafute mmoja hivi naona yeye kasoma UDOM hahahaha nahisi ni size yangu
 
Back
Top Bottom