Ahmed Shabiby Mbunge wa Gairo katika Ubora wake!

Jul 24, 2015
80
38
Pongezi kwa Mh. Ahmed Shabiby kwa kuwatendea haki wadau wa bidhaa za Petroli kuhusu uchakachuaji na uwekaji wa Vinasaba wakati ukichangia bajeti ya Wazara ya Nishati na Madini. Hongera Mh. Ahmed Shabiby!
 
Huyu ni mkwepa kodi ndiyo maana amechukizwa na mchango wa mh. Shabiby, hata kama shabiby ni ccm lakini kama amekemea wakwepa kodi namuunga mkono
 
Utakamatwa kwa kosa la kuangalia bunge saa za kazi!! Au wewe ndio Shabiby unajifagilia hapa maana tumeambiwa hakuna bunge live hapa kazi tu
 
Kituo cha mafuta cha shabibby kilichopo makore dodoma kiliwahi kukamatwa na ewura kwa uchakachuzi wa mafuta , ushahidi umo humuhumu jf , hatoaminika tena .
 
Shabiby hajakemea ukwepaji Kodi, bali anataka ukaguzi wa wachakachuaji upigwe marufuku eti wanaonewa wauza mafuta. Alikamatwa January mwaka huu, akalia kwa Prof Muhongo ewura hawakumwachia, akalia kwa PM hakuachiwa, sasa anataka utaratibu huo uachwe.
 
Akumbuke jimbo lake,miaka Kumi maji hakuna na bado kuna watu wanajitokeza kumpongeza!!,kisa kuwatendea haki wadau wa bidhaa ya mafuta ya Petrol kwa uchakachukuaji na kuweka vinasaba
 
Back
Top Bottom