Ahmed Rajabu, hili la uamsho vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahmed Rajabu, hili la uamsho vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 2, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Yanayoendelea Zanzibar yanamwacha kila mtanzania kutafakari kivyake nini hasa kiini, nia na malengo mahsusi ya wanauamsho. Wao ni kikundi cha 'kidini' ambacho kinapigania Zanzibar kujitoa kwenye muungano ambalo ni jambo la kisiasa na kisheria pia. Si vibaya kwa mwanauamsho mmoja mmoja kuwa na msimamo na mtazamo wake kuhusu muungano lakini kwa uamsho kama taasisi ya 'kidini' kuwa na msimamo na mtazamo rasmi katika jambo ambalo si la kidini bali la kisiasa/kisheria inaleta tabu kueleweka na kuleta hisia kuwa huenda uamsho una ajenda mahsusi ambayo imefunikwa tu katika ajenda ya kupinga muungano. Tafakari uchomwaji wa makanisa!

  Nikiendelea kutafakari yanayotokea visiwani napata wasiwasi na ukimya wa mwandishi mkongwe na wa kimataifa AHMED RAJABU, mwandishi huyu ameandika mfululizo wa makala zisizopungua tano kwenye gazeti la RAIA MWEMA kuhusu suala hili nyeti la muungano. Katika maandishi yake yote alionyesha dhahiri kutopenda muungano kwa kuutuhumu kuwa umewafukarisha wazanzibari japo hakuwa jasiri kusema umewatajirisha akina nani. Nilitegemea katika gazeti la RAIA MWEMA la tarehe 30 mei, 2012 angeandika lolote kuhusu vurugu zinazoendelea Zanzibar lakini kakwepa na badala yake kazungumzia uadilifu wa uongozi.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160

  Mkuu nakubaliana na wewe huyu Ahmed Rajabu kafanya uchochezi mkubwa sana kupitia kalamu yake sina hakika kama hajatumia pia njia nyengine zaidi ya kalamu kupandikiza chuki dhidi ya muungano,Nyerere, watanganyika. Na hawa ndiyo wanaowaponza wazanzibari, wao wako mbali huko ughaibuni wanawachochea ndugu zao huku kikinuka wao na familia zao wako salama ughaibuni wakila tambuu.
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Hapo hakuna madai ya muungano kuna udini, hilo halifichiki kabisa.
   
 4. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Akishamaliza kuitenganisha Zanzbar, kalamu yake haitatulia ataona hata Pemba inafukarishwa na Unguja
   
 5. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,032
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Kaka huyo mzee nimdini tu. Unakumbuka wabara walipochomewa mabanda yao ya biashara aliandika kuwasifu Wazanzibar wenzake kwakitendo chao. Alidai kuwa wabara wanawabadilisha tabia na mienendo (dini ikiwemo) kwa kuingiza ukristo na kilabu za pombe. Kwake yeye Ukristo ni janga la Uzanzibari, Ukristo haustahili kuwepo huo, Wabara ni watu wa ovyo wanaowaharibu watoto wao. Alichosahau ni kuwa watu wa Bara bila kujali dini zao ni watu wa DEMOKRASIA, kila mtu kujirusha sawa na urefu wa kamba yake.

  Nauliza tu! Hivi anaishi Zanzibar au bado yupo Uingereza na gazeti lake la AFRIKA NOW? Nikijibiwa hilo ntarudi na tafakauri shadidi kumhusu.
   
 6. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,317
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160

  tatizo sisi watanganyika tumenyweshwa sana hii zanzibar kwa sababu ya ufala wetu

  hatuwezi kufikiri mbali zaidi ya zanzibar ,

  Tanganyika tupo zaidi ya watu milioni 40 , matatizo tuliyonayo yametuzidi kimo , lakini badala ya kushughulika na ka nchi yetu tumekuwa Programmed na kupata ugonjwa wa Zanzibar mpaka usiku tunaota na kuweweseka Zanzibar

  Tunasahau kuwa huko nyuma ilikuwepo Tanganyika na ilikuwepo Zanzibai , kila mtu na nchi yake na mambo yalikuwa poa.

  Kwa nini tusiwaachie nchi yao wakasolve wenyewe mambo yao???

  TUTAKOSA NINI HUKO ?????

  Mitandaoni , JF, Radio, TV, Magazeti yote ni zanzibar ka visiwa viwili visivyozidi watu milioni 1 na nusu .

  Tunaendeshwa na hii ndoto Zanzibar kama vile ndio Roho ya Tanganyika ,

  Masikini Watanganyika ,
  Masikini Great thinkers

  Kwa mawazo haya na fikira hizi maisha tutaendelea kulala na kuwaacha Mafisadi wakipeta huku tukiota Zanzibar
   
 7. p

  petrol JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  nani aliwambieni kuwa kuna dini siyo siasa. kwani wakoloni walipokuwa wanachukua makoloni hawakutanguliza bibli, na waarabu walipokuwa wanawinda ndugu zetu na kuwaswaga utumwani hawakutangukliza Kurani? Ya zanzibar tumeyalea kwa kutoruhusu mjadala wa wazi katika masuala mengi ya kisiasa, muungano likiwa mojawapo. sasa tutavuna tulichopanda. tusilalamike sana na kuanza kuita watu majina ya hovyo.
   
 8. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  jana kwenye Kipima joto (ITV) camanda Lisu alisema kuwa wale watu wasioupenda Muungano wa visiwani na bara hawana forum yakutoa maoni yao Kwenye Tume ya kuunda katiba mpya, wamepigwa marufuku na JK kujadili swala la uwepo wa Muungano au kutokuwepo muungano. Wanaruhusiwa kujadili maboresho tu ya huu muungano feki. sasa wewe unafikiri watatoa maoni yao wapi-iliobaki kwao kupitia udini ndio watapata fursa hiyo ya kuukataa muungano huu. Mimi ni mdanganyika na muungano huu siutaki maana hauna faida yoyote kwangu hasa nikifikiria tunaowabembeleza (Wazenj) hawatutaki.

  This is the beginning of the end of UNION, it is just a matter of time
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Unataka aandike nini wakati hayo ndio anayoyataka,lakini hata mimi nafurahia hiyo hali wacha muungano uvunjike hawa wazenj wamekuwa kupe,sioni huo muungano unavyotusaidia sisi Watanganyika,zaidi ya kuwanufaisha viongozi wa CCM.Kwanza hao watu tuko tofauti sana nao kwa kila kitu waache watawaliwe na Oman ni watu waopendwa kutawaliwa na waarabu,wajomba zao pia ndio hao wa Mombasa repulican,wimbo wao ni kutaka maendeleo ,wanataka maendeleo wapewe kwenye sahani
   
 10. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama nakuelewaelewa vile
   
 11. salito

  salito JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,366
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  hapa naona chenga tu..
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Huyu mzee hakai zanzibar, huwa anakwenda kusalimia na kuondoka zake. Naambiwa alikuwa huko hivi karibuni kati ya march na april. Sasa mwaga radhi mkuu!!
   
 13. u

  umsolopagaz Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .....ndugu...umeongea maneno mengi mbofumbofu...! na si ujiulize;..kuna ukaribu gani kati ya mmasai na mswahili wa bagamoyo? na kuna tofauti gani kati mndengereko na muunguja yeyote "aswadi"?
   
 14. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  kwani majority ya wazanzibari wakiamua nchi yao iongozwe na udini, kuna kosa gani?

   
Loading...