Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kuwa usajili utakaofanywa na Simba safari hii utakuwa na umakini wa kiwango cha ICU (Intensive Care).
"Taarifa tu ni kwamba usajili wetu safari hii unafanyika kwa umakini wa ICU, na wachezaji waliopendekezwa na mwalimu wameshasajiliwa, na wengine wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili," ameandika Ahmed Ally kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Aidha, ameongeza kuwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuna taarifa mbalimbali kuhusu usajili wa Simba, ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakiihusisha Simba na kila mchezaji ili kuwapa thamani wachezaji wanaotaka kuwasajili.
"Kwa sasa tunamalizia kutoa barua kwa wale tunaoachana nao, kisha tuanze kuvurumisha Thank You na baada ya hapo tuanze kudondosha chuma kimoja baada ya kingine," amesema Ahmed Ally.