Sio kweli, katafute cv ya ahmed Ally before you come here spitting rubbish. Ahmed Ally ni muajiriwa wa mkataba simba kama waajiriwa wengine. Kapewa cheo cha afisa habari wa Simba.
Kuna utofauti mkubwa kati ya mfanyakazi na shabiki.. Kwenye hoja ya kuwa mshabiki wa Yanga naweza kubaliana na wewe... Unaweza kuwa mshabiki wa upande A lakini mfanyakazi wa upande B.
Kazi yake si kupumbaza wanasimba... Nadhani utamkosea pia heshima kwa kutothamini mchango wake pale simba.
Ahmed Ally, hajaajiriwa na Mo.. kaajiriwa na Simba Sc, anafanya kazi yake kiweledi mkubwa.. Je ulitaka simba ikifanya vibaya ajiuzulu? Kwani yeye anacheza?
Kazi yake ni uafisa habari, si mchezaji, si skout, si kocha etc.
Wanasimba tukitaka tumfurahie kazi yake, basi tuwe na timu nzuri na strong la sivyo tutamtupia lawama j3 mpk j2...
Wanaomzungumzia mangungu ni sababu yeye ni mwakilishi wa wanachama. Zile share 51% za wanachama, boss ni mangungu ndiye mwenye uwezo wa kupambania...