Ahadi za 2005 zinamtesa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi za 2005 zinamtesa JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAMBLER, Dec 19, 2009.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahadi za urais 2005 zamtesa Kikwete uchaguzi wa mwakani[​IMG]Rais Jakaya Kikwet, mzigo mzito wa ahadi zake za mwaka 2005 unamkabili uchaguzi ujao 2010.[​IMG]Na Mwandishi Wetu

  MIEZI michache ikiwa imebaki kabla ya kuanza kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano, Rais Jakaya Kikwete anaonekana kukabiliwa na mzigo mzito wa kutekeleza ahadi nyingi alizozitoa wakati wa kampeni za mwaka 2005.

  Kikwete alipata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 baada ya kunyakua takriban asilimia 80 ya kura, akiwa pia ameshinda kwa kishindo dhidi ya wapinzani wake kwenye uteuzi wa mgombea wa CCM.

  Lakini kadri muda unavyokwenda ndivyo umaarufu wake unaonekana kupungua huku tafiti mbalimbali zikionyesha kuwa umaarufu aliokuwa nao wakati akiingia madarakani unaendelea kuporomoka, ikiwa ni miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Wakati akizunguka sehemu mbalimbali nchini kuomba kura za wananchi, Kikwete alikuwa akitoa ahadi kem kem ambazo alizielezea kwa kifupi kwenye kauli mbiu yake ya “Naisha Bora kwa Kila Mtanzania” ambayo mkakati wake wa kuitekeleza ulikuwa ni “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya”.

  Mbali na ahadi ambazo alikuwa akizitoa kwa wananchi kila sehemu alipoelezwa tatizo, ikiwa ni pamoja na matatizo sugu ya maji, miundombinu, huduma za afya na pembejeo, Rais Kikwete pia alitoa ahadi za ujumla kabla na baada ya kushinda uchaguzi kumrithi Benjamin Mkapa.

  Baadhi ya ahadi hizo za Rais Kikwete kabla na baada ya kuingia madarakani ni pamoja na kuweka kipaumbele katika kilimo, akitumia kaulimbiu ya Kilimo Kwanza, kupitia upya mikataba ya madini ili inufaishe nchi na wawekezaji, na kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi wa elimu ya juu anayekosa masomo kwa kukosa karo.

  Ahadi nyingine ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za umma, kuumaliza mgogoro wa Zanzibar, kuimarisha uhusiano wa kimataifa, kukomesha tatizo la ufisadi, kupambana na tatizo la uhalifu, ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya na ujambazi, kuandaa mdahalo wa kitaifa wa michezo kwa lengo la kuinua michezo na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Lakini wasomi na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kuwa ahadi nyingi hazitekelezeki na nyingi hazijawekewa mkakati wa kuzitekeleza na hivyo wanaona zitakuwa mzigo kwa mbunge huyo wa zamani wa Chalinze.

  Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili, tayari ahadi hizo zimeanza kumtesa Rais Kikwete imeaanza kumtesa na kumpotezea umaarufu mbele ya wananchi, huku mjadala juu ya udhaifu wake katika utendaji kazi ukizidi kupamba moto.

  “Ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania ilikuwa ni ndoto ya kisiasa,” anasema mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alitakiwa na Mwananchi Jumapili kutoa maoni yake kuhusu ahadi za Rais Kikwete.

  Dk Bana alisema pamoja na kuwa serikali imejitahidi katika suala la elimu, imekosea katika suala la elimu ya watu wazima kwa kuwa imeachwa na haijapewa kipaumbele.

  “Elimu ya watu wazima ingekuwa imepewa kipaumbele, tusingekuwa tunazungumzia elimu ya kilimo kwanza kwa kuwa wananchi wangekuwa hivi sasa wanafundishana wenyewe.”

  Dk Bana, ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya Demokarsia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Redet), alisema baadhi ya ahadi hizo hazitekelezeki.

  Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo alisema kuwa si kwamba Rais Kikwete hajafanya kitu, bali ameshindwa kutekeleza ahadi zake nyingi.

  Alisema suala alilokuwa akilizungumzia la maisha bora kwa kila Mtanzania ndoto na kwamba kauli mbiu ya “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” ilikuwa ni siasa ambayo itamtesa.

  “Serikali huwa inataka kushinda uchaguzi, ahadi nyingi hazitekelezeki; ameshindwa mengi na amejitahidi machache,” alisema Ndesamburo.

  Naye Dk Azavael Lwaitama wa UDSM alisema suala si la Rais Kikwete bali kujiuliza CCM imefanya nini mpaka sasa kwa kuwa ndicho chama kilicho madarakani.

  “Wananchi wanaishi kwa matumaini kwa sababu kuongeza shule nyingi si maendeleo kwa kuwa wanafunzi wengi wanafeli; kukosekana kwa waalimu ni tatizo,” alisema Dk Lwaitama.

  Alisema kuwa ni kitu cha ajabu kwa katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba kusema kuwa Kikwete ndiyo anakibeba chama, wakati chama kipo tangu alipokuwepo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na amefariki na kukiacha.

  “Inashangaza Makamba kusema Rais Kikwete ndio anakibeba chama wakati Nyerere alikuwepo, amefariki na amekiacha chama, kilichopo ni kuangalia mustakhabali wa chama na si kumsifia mtu,” alisema Dk Lwaitama.

  Wakati wakisema hayo, Makamba alishawahi kukaririwa akisema Rais Kikwete atatimiza ahadi zake alizotoa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kama atapatiwa muda.

  Hivi karibuni balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Tim Clarke aliambia Mwananchi Jumapili kuwa anashangaa kuona serikali inasema inakwenda kwa mwendo wa kasi, lakini mambo mengi yapo kama yalivyo.

  Clarke alisema wabia wa maendeleo ya Tanzania wamefanya mapitio ya mwaka na hali inaonekana si nzuri kama ilivyotarajiwa kwa kuwa alama za utekelezaji ziko wastani, huku maeneo kama vile mageuzi katika sekta ya umma yakionyesha alama zinazotia wasiwasi wa kutopata mafanikio.

  Alisema kuwa pamoja na kuwa wabia wamekuwa wakitoa misaada kwa Tanzania, baadhi wanafikiria kupunguza ahadi na utoaji wa misaada kwa kuwa hawaoni mpango ulio wazi wa kushughulikia matatizo katika njia inayoeleweka.

  Naye askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alikaririwa wiki hii akisema kuna kila dalili za kukwama kwa mkakati wa kilimo kwanza, kutokana na kushindwa kuelekeza nguvu za kutoa elimu kwa wakulima ili waendeleze sekta hiyo.

  Akionyesha mtazamo huo tofauti, Pengo alisema:"Kaulimbiu inayotumiwa na viongozi wa nchi (Kilimo Kwanza), haiwezi kubadili au kuleta maendeleo katika kilimo. Cha msingi hapa ni kumwezeshe mkulima kwanza ili apate elimu ya kuendeleza kilimo.” Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Itabidi ufike wakati Watanzania tuwaamue viongozi kwa ahadi walizozitoa na kuzitimiza/kutotimiza. Nakumbua George Bush the father alipotoa ahadi ya "read my lips, no new taxes, na akawatoza wapiga kura kodi, walimpa term moja. Tumpime kiongozi kwa ahadi alizotoa mwenyewe. Tusikubali haya ya kuambiwa, kama alivyofanya Mkapa, kuwa hazitekelezeki. Kama hazitekelezeki what the hell were you doing giving them in the first place?
   
 3. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Jasusi:

  Kwa hiyo ina maana wachague Mbowe kwa sababu JK kashindwa? Wakati mwingine watu wanamchagua mtu kutokana na alternative iliyopo kuwa bomu.

  Na Bush kutochaguliwa inawezekana kulitokana na Ross Perot kujiingiza kwenye uchaguzi na kugawanya kura za republicans na sio kukumbuka masuala ya tax. Kwani Clinton na democrats ni wapenda kutoza tax.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana,
  Sijasema hivyo. Ninachosema ni kwamba JK hastahili kupewa another 5 years.
  The first 5 have been a mess. And then again I am not in the position kuwachagulia Watanzania. I am sure among 40 million Tanzanians there must be someone who can do better than Kikwete. Point ya Bush ni kwamba he made a promise he did not keep. At least American voters do not forget, Ross Perot notwithstanding.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Dec 19, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tumsubiri kwenye kampeni zake tusikie atasemanini.
  Sana sana ataomba aongezewe muda ili aweze kumalizia ahadi zake!
   
 7. H

  Hhm Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Eeeh amalize kwani kuna ipi so far imetekelezeka!!!
   
Loading...