Ahadi ya My Rais kwa wana Geita kuhusu magwangala haijatekelezwa

ngunde11

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
682
889
Ni masikitiko yangu makubwa kama mwana geita kwani ahadi aliyoitoa Mh Rais kuwa baada ya wiki tatu wizara ya madini kushirikiana na mgodi wa GGM wawe tayari wameandaa mpango na ugawaji wa magwangala aanze mara moja, lakini mpaka leo hii yapata wiki ya nane hakuna kinachoeleweka,

Kibaya zaidi tuliambiwa tujiunge kwenye vikundi vya saccos na michango tumekwishalipa, kwenye kikundi chetu ni 10000 achilia mbali muda tuliotumia kuzunguka kwa ajili ya usajili

Wakuu naomba ushauri inawezekana nikawashitaki ggm au wizara kwa kutotimiza agizo la Mh au naweza kumshitaki Mh mwenyewe kwa kutoa ahadi hewa nikitumia nguvu ile ile kama yeye anavyo deal na wafanyakazi hewa au naweza kuwaunganisha wote kwa umoja wao kwenye kesi moja

Natanguliza shukrani kwa michango yenu ya kujenga taifa
 
Kwa kiasi kikubwa wanasiasa wameiaminisha ama kuipotosha jamii ya wana Geita na Tanzania kwa ujumla kwamba unaweza kuchakata au kuchenjua magwangala (taka miamba/waste rocks) kwa faida kitu ambacho kitaalamu sio kweli.

Mwekezaji mkubwa kama AngloGold Ashanti-GGM anayetumia teknolojia ya hali ya juu (Communition + Carbon In Leach + Elution + Electrowinning + Smelting) kuipata dhahabu ameshakwambia haya mawe ni wastes (Gangue) then wewe mwanasiasa unawapotosha wananchi wanaoutumia teknolojia duni kabisa kataka kuchenjua dhahabu (Amalgamation au Vat Leaching technology) kwamba wanaweza kupata faida kwa ku-process magwangala?? What a big shame??

Waste rocks disposal tu inayofanywa na hii kampuni kubwa GGM wanatumia taaluma ya juu sana ya Utunzaji wa Mazingira, mchimbaji gani mdogo anayejua kutofautisha kati ya Potential Acid Forming (PAF) Rocks & Non Acid Forming (NAF) Rocks?? na hata wakitambua wanajua procedures ya disposal ya tailings zitakazatokana na Acid Forming Rocks ili wasilete uharibifu mkubwa wa mazingira hususa vyanzo vyao wenyewe vya maji?? Je uharibifu wa mazingira utakaotokana na shughuli hz nani atawajibika??

Hivyo nikiwa kama mtaalamu katika sekta hii ya madini naishauri Serikali yangu sikivu ikiongozwa na Raisi msomi Dr. John Magufuli waachane na mpango huu kwani wananchi wataenda kupata hasara za kutisha kwa kupoteza fedha zao nyingi sababu kitaalamu au kiuchumi hakuna faida kwa mchakato huu.
Pili madhara ya kimazingira na kijamii yatakayotokana na mchakato huu ni makubwa sana.
Serikali ifikiri namna nyingine ya kuwasaidia wananchi wake wa Geita hususa wachimbaji wadogo, kama vile kuwatengea maeneo yenye potential mineral resources kwa ajili ya uchimbaji na kwa hili wanaweza kukaa meza moja ya mazungumzo na huyu mwekezaji ili basi awaachie wananchi sehemu ndogo iliyo ndani ya leseni yake kwa ajili ya uchimbaji na uchenjuaji mdogo mdogo.
 
Itakapobainika kuwa hayo Magwangala mnayo lilia yana sumu hatari kwa afya zenu zikiingia kwenye maji na vyakula (mimea na visima) mnavyotumia ndipo mtakapogwangala vizuri.
 
Waliwambia yanasumu mkipewa mkafa na penyewe lawama wabongo bana mnakimbilia kifo wenyewe
 
Kwa kiasi kikubwa wanasiasa wameiaminisha ama kuipotosha jamii ya wana Geita na Tanzania kwa ujumla kwamba unaweza kuchakata au kuchenjua magwangala (taka miamba/waste rocks) kwa faida kitu ambacho kitaalamu sio kweli.

Mwekezaji mkubwa kama AngloGold Ashanti-GGM anayetumia teknolojia ya hali ya juu (Communition + Carbon In Leach + Elution + Electrowinning + Smelting) kuipata dhahabu ameshakwambia haya mawe ni wastes (Gangue) then wewe mwanasiasa unawapotosha wananchi wanaoutumia teknolojia duni kabisa kataka kuchenjua dhahabu (Amalgamation au Vat Leaching technology) kwamba wanaweza kupata faida kwa ku-process magwangala?? What a big shame??

Waste rocks disposal tu inayofanywa na hii kampuni kubwa GGM wanatumia taaluma ya juu sana ya Utunzaji wa Mazingira, mchimbaji gani mdogo anayejua kutofautisha kati ya Potential Acid Forming (PAF) Rocks & Non Acid Forming (NAF) Rocks?? na hata wakitambua wanajua procedures ya disposal ya tailings zitakazatokana na Acid Forming Rocks ili wasilete uharibifu mkubwa wa mazingira hususa vyanzo vyao wenyewe vya maji?? Je uharibifu wa mazingira utakaotokana na shughuli hz nani atawajibika??

Hivyo nikiwa kama mtaalamu katika sekta hii ya madini naishauri Serikali yangu sikivu ikiongozwa na Raisi msomi Dr. John Magufuli waachane na mpango huu kwani wananchi wataenda kupata hasara za kutisha kwa kupoteza fedha zao nyingi sababu kitaalamu au kiuchumi hakuna faida kwa mchakato huu.
Pili madhara ya kimazingira na kijamii yatakayotokana na mchakato huu ni makubwa sana.
Serikali ifikiri namna nyingine ya kuwasaidia wananchi wake wa Geita hususa wachimbaji wadogo, kama vile kuwatengea maeneo yenye potential mineral resources kwa ajili ya uchimbaji na kwa hili wanaweza kukaa meza moja ya mazungumzo na huyu mwekezaji ili basi awaachie wananchi sehemu ndogo iliyo ndani ya leseni yake kwa ajili ya uchimbaji na uchenjuaji mdogo mdogo.

Hongera sana kwa kuongea kitaalamu na ukweli mtupu japo wanasiasa wasioelewa watakataa. Waziri mhusika wa wizara ni mtaalam analitambua hilo na yawezekana ndo maana analipotezea. Wataalamu wa NEMC wanalijua hili kwa undani sana na wanajua madhara yake yawezekana ndo maana wanalipotezea pia. Watu wa kawaida na wanasiasa wasiojielewa wanwadanganya sana viongozi wakubwa. Hizo PAF & NAF Rocks ni topic kubwa kwa jamaa wa uchimbaji madini (waulize waliosoma kozi za madini na mazingira) kuzielewa. Hata kabla ya wachimbaji wakubwa hawajapata vibali vyao lazima waoneshe namna gani watadhibiti hizo waste product (acidified rocks) na ndo maana lazima wafanye kitu kinaitwa Environmental Impact Assesiment (EIA) na waoneshe namna ya kudhibiti taka (waste management). Sasa leo tu unamwambia mtu amwage tu material/waste ovyo baadae si utamgeuka baada ya madhara kutokea?

Suluhisho ni kuwatengea maeneo ya uchimbaji mdogomdogo, kuwapa/kukopesha mitaji, nyenzo na utaalamu wa jinsi ya kuchimba kwa faida. Zaidi ya hivyo ni siasa tu zisizo na maana.
 
tatizo hiyo ni mikataba ya kimataifa ambayo hakitupwi kitu kwa bebari sasa kuanza kuyagawa ni lazima mkataba upitiwe na urekebishwe kwanza na la msingi wataalamu wa afya wajirizishe kwa afya ya binadamu kwa kuwa yama madude huwa yanakuwa yameoshwa na mercury. Swala la mazingira wanamazingira lazima wajiridhishe pia ni wapi yatamwagwa na je mazingira hayo yatabaki salama? Issue ya ulinzi je hapo patakapo mwagwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao itakuaje. L a mwisho ni eneo la nani aliyetayari kukubali kutoa eneo ligeuzwe machimbo ya juu ya ardhi kwa maana maeneo yote yanayozunguka mgodi ni prime area viwanja vipo na bei juu sana. SASA WAKATI TAMKO LINATOLEWA HAYO YOTE YALIKUA HAYAJAWEKWA VIZURI SO TUWAPE MUDA WAJIPANGE NI MAWAZO YANGU TU.
 
Back
Top Bottom