Ahadi ni Deni

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Juzi nilikuwa naangalia kipindi cha Ahadi ni Deni kinachorushwa na Runinga ya ITV. Kuna mambo mawili ambayo niliyaona na kuyasikia ambayo ningependa kuwashirikisha:

Kwanza, ninachoweza kusema ni kwamba binafsi nilishindwa kuona mahusiano kati ya Jina la kipindi na yale ambayo yalikuwa yakiongelewa. Mimi nilitarajia kwamba waandaaji wa kipindi walilenga kufanya tathmini ya utekelezwaji wa ahadi zilizotolewa na Wabunge pamoja na Madiwani wakati wakiomba kura. Lakini sikuona wala kusikia hilo. Nitoe mfano wa wabunge watatu na mambo waliyoyaongelea; Mhe. Anne Kilango Malechela yeye alikuwa anaongelea uchafuzi wa vyanzo vya maji na namna alivyojiandaa kuikwamisha bajeti ya Wizara ya Maliasili; Mbunge wa Vitu Maalumu Mara (Jina nimelisahau) yeye aliongelea mambo ya Katiba mpya; na Mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Tabora (Jina nimelisahau) yeye aliongelea namna alivyochangia maendeleo kwenye jimbo lake kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo.

Ushauri wangu kwa waandaaji wa kipindi cha Ahadi ni Deni ni kwamba kabla ya kumfuata mhusika watafute na kuwa nazo ahadi alizotoa mhusika na hizo ndiyo ziwe mwongozo wa muendeshaji wa kipindi katika kudadisi utekelezaji wake vinginevyo wabadili jina la kipindi.

Suala la pili ni kuhusu fedha za Mfuko wa Jimbo. Katika hili mimi nina maswali ambayo yananikireketa baada ya kumsikiliza yule Mbunge wa Tabora. Yeye alisema Mbunge wenu amechangia sh. milioni 90 na ushehe (sikumbuki tarakimu sahihi) kwa miaka miwili. Hivi hizi fedha za Mfuko wa Jimbo ni za Mbunge? Inamaana Mbunge ndo Jimbo au vipi? Je, na yale majimbo ambayo kwa sababu moja au nyingine huwa hayana wabunge kwa nyakati fulani huwa hayapatiwi mgao wa fedha hizo hadi Mbunge atakapopatikana?

Mwisho nawapongeza ITV kwani wameonyesha kuwa na ubunifu wa vipindi ila tu wajitahidi kuongeza umakini katika kuviandaa ili vibebe maudhui muafaka
 
Back
Top Bottom