Inategemea una uhusiano gani na mgonjwa..labda alikuwa dada/shangazi/mama etc, hapo utapaswa kutoka nje, kama huna imani na Dokta, basi omba nesi awepo wakati anampima. Kama alikuwa mpenzi wako , basi ulikuwa na haki ya kuwepo na ulikuwa sahihi kubana mpaka penati..ila kama mlikuwa mmefuata huduma ya kupima VVU, na dada hakusema kuwa yuko comfortable kuongea na Dokta huku ukiwepo, pia ilibidi utoke nje..lakini kama wote mlikuwa comfortable kupata ushauri nasaha na kupima pamoja na kujuzana majibu..bali ulikuwa na haki tena ya kukaba mpaka penati. Kwa hiyo inategemea na mazingira..kuna mazingira yanakunyima haki ya kuwepo ofisini kwa Dokta akimpima binti uliyempeleka..na mengine yanakuruhusu!