Agundua namna ya kuishi milele....

Agundua namna ya kuishi milele....

Hahahaaa...not buying it one bit.

Junk science from a junk scientist.


Ila umewahi wasikia wanasayansi wanaoamini
in a few years tutaanza kuishi milele as robots?
tutakuwa tunatumia artifial inteligence na viungo vya robots?
akiwemo ceo wa google pia wanaamini hili
kuna mrusi kaanzisha program by 2045 anasema it will be possible
 
Ila umewahi wasikia wanasayansi wanaoamini
in a few years tutaanza kuishi milele as robots?
tutakuwa tunatumia artifial inteligence na viungo vya robots?
akiwemo ceo wa google pia wanaamini hili
kuna mrusi kaanzisha program by 2045 anasema it will be possible

Wao kuamini ni sawa tu.

Ila mimi nitausubiri huo uhalisia wa imani zao niushuhudie ndipo nitakubali.....
 
Kuna watu hawataki kufa
mimi naona kukataa kufa ni kama kukataa kumaliza shule
utaishia kugeuka kituko shuleni

Haswaaaa
Mwisho watajikuta wapweke
Au maradhi ya uzee
Au utegemezi
Kama sio kujikuta wamechoka tu na maisha.....

Unless hiyo program iwe na uwezekano wa kuzima mtu akichoka kuishi
 
Hii inawezekana kabisa, kingunge lowasa malkia elizabeth wanamiaka mia bado wapo, lowasa ndo kwanza anawania urais, mbeleni watu wataishi milele.
 
Haswaaaa
Mwisho watajikuta wapweke
Au maradhi ya uzee
Au utegemezi
Kama sio kujikuta wamechoka tu na maisha.....

Unless hiyo program iwe na uwezekano wa kuzima mtu akichoka kuishi


Upweke lazima
we watu wa zamani tu wanachoshwa na dunia ya sasa ndo waishi milele?
zamani ilikuwa ndoa ni mwanaume na mwanamke
hereni ni wanawake tu wanavaa
sasa ukiishi milele si utakuja shuhudia ndoa za binadamu na wanyama?
nguo uni sex..na kila aina ya vituko,,,lazima uwe mpweke...
 
What a good news. Kama hizo njia zitafanya kazi basi ntazijaribu. Kifo sio kitu cha kufurahisha hata kidogo.
 
Hii inawezekana kabisa, kingunge lowasa malkia elizabeth wanamiaka mia bado wapo, lowasa ndo kwanza anawania urais, mbeleni watu wataishi milele.

Acha hizo mkuu maana naona hata umri wa Lowassa huujui
 
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:



كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور

((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]



Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam عليه السلام hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]



Vile vile Anasema Allaah سبحانه وتعالى :



((كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَان&#1613😉) ((وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَا&#1605😉)



((Kila kilioko juu Yake kitatoweka)) ((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]



Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah سبحانه وتعالى. Kisha Allaah سبحانه وتعالى Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah سبحانه وتعالى Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah سبحانه وتعالى Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,



((وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِه&#1616😉)



((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67]



Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنه kwamba:



((يطوي السموات والأرض بيده، ثم يقول: أنا الملك، أنا الجبار، أنا المتكبر، أين ملوك الأرض؟ أين الجبارون؟ أين المتكبرون&#1567😉) مسلم



((Allaah Atazikunja mbingu katika Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?)) [Muslim]



Hapo tena Atauliza mara tatu:

((لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْم&#1614😉)

((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16]



Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,

((لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّا&#1585😉)



((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16]



Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah سبحانه وتعالى Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.



((الْيَوْمَ تُجْزَى كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَاب&#1616😉)



((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]
 
Kuna watu hawataki kufa
mimi naona kukataa kufa ni kama kukataa kumaliza shule
utaishia kugeuka kituko shuleni

Dunia yenyewe humu tunamoishi itakufa; tena inakufa kwa haraka zaidi kuliko jamii ya binadamu na ufaji wake ndio huathiri sana na kupunguza uhai wa mwanadamu. Wangeanzia na hilo kwanza; la kuifanya dunia yenyewe iishi milele
 
Back
Top Bottom