Agundua namna ya kuishi milele....

Agundua namna ya kuishi milele....

Km nitabaki kijana hivi hivi sawa niish milele ila nikizeeka hapana nife coz ukizeeka unakuwa mpweke mno
 
kifo kipo pale pale hakiepukiki
Miaka 150 hivi iliyopita ilikuwa ni muujiza mkubwa kuwa Mbeya ukaongea ukasikika Musoma, na miaka 80 hivi iliyopita ilikuwa ni muujiza au hata uchawi mkubwa na ndoto pia kwamba waweza kuwa Dar na mtu aliyopo Kigoma akakuona wakati huo huo. Leo hii haya ni mambo ya kawaida mno na sioni kwanini suala la kuongeza umri wa kuishi angalau mpaka miaka 1000 liwe jambo lisilowezekana.
 
Utaishi milele ukiwa na ukimwi wako?na cancer yako? Na hata baada ya ajali mbaya ya toyo au gari?utaendelea kuishi milele huku figo,maini na moyo vinapolazimika ku quit kutokana na hewa za sumu tunazovuta daily?tuwe serious jamani,niliangalia documentary ya mrusi mwingine anaye dhamini research nyingine eti ya kuhamisha conscious from one person to another nikashangaa, eti unapokaribia kufa kuna uwezekano wa kuuhamisha ufahamu wako na kuwekwa kwa mtu mwingine electronical na ukaendelea kuishi ndani ya mwili wa mtu mwingine,this is intensely a wealthy paradox.
 
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:



كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور

((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]



Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam عليه السلام hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]



Vile vile Anasema Allaah سبحانه وتعالى :



((كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَان&#1613😉) ((وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَا&#1605😉)



((Kila kilioko juu Yake kitatoweka)) ((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]



Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah سبحانه وتعالى. Kisha Allaah سبحانه وتعالى Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah سبحانه وتعالى Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah سبحانه وتعالى Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,



((وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِه&#1616😉)



((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67]



Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنه kwamba:



((يطوي السموات والأرض بيده، ثم يقول: أنا الملك، أنا الجبار، أنا المتكبر، أين ملوك الأرض؟ أين الجبارون؟ أين المتكبرون&#1567😉) مسلم



((Allaah Atazikunja mbingu katika Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?)) [Muslim]



Hapo tena Atauliza mara tatu:

((لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْم&#1614😉)

((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16]



Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,

((لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّا&#1585😉)



((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16]



Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah سبحانه وتعالى Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.



((الْيَوْمَ تُجْزَى كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَاب&#1616😉)



((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]

mashallah elimu nzuri kwa wenye mazingatio,huu ndio ukweli ALLAH AKBAR
 
Nataka kuishi milele mbinguni kwa baba,nikiimba na kukizunguka kiti cha enzi pamoja na Elia Elisha na Yakobo.
Duniani sitaki kuishi milele maana sio nyumbani kwetu.
Wanaotaka kuishi duniani hawajui kuna sehemu nyingine nzuri zaidi ya hapa
 
Ila umewahi wasikia wanasayansi wanaoamini
in a few years tutaanza kuishi milele as robots?
tutakuwa tunatumia artifial inteligence na viungo vya robots?
akiwemo ceo wa google pia wanaamini hili
kuna mrusi kaanzisha program by 2045 anasema it will be possible

Hapa zile hisia za kujitambua kwamba wewe ni wewe (hapa naizungumzia roho ambayo Muumba mwenyewe ndio anaitambua) zitakuwepo? Au ndio watu wanaokutazama tu ndio watakuwa wanakuona upo duniani lakini kumbe haupo
 
Back
Top Bottom