Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amemuagiza Marry Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) ifikapo Agosti Mosi mwaka huu.
Mongella amesema kuwa, machinga katika mkoa huo, wamekuwa wakifanya biashara zao bila kufuata kanuni na sheria zilizopo hivyo amemtaka mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anasimamia zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao.
“Machinga unakuta anapanga biashara zake hadi kwenye mlango wa nyumba ya mtu, sasa hali hiyo haiwezi kuvumilika hata siku moja, tunajua ni ndugu zetu wanaopaswa kufanya biashara zao lakini hatuwezi kwenda kwa namna hiyo,” amesema Mongella.
Amesema kuwa, wafanyabiashara hao wanapaswa kufuata kanuni na sheria za nchi zilizopo, huku akiwataka kuhamia katika maeneo rasmi yaliopangwa yaliopangwa na halmashauri ya Jiji hilo kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.
Tesha amesema kuwa, atahakikisha anaendeleza alipoishia mtangulizi wake (Baraka Konisaga) katika kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Nyamagana.
Chanzo: mwanahalisi