edu88
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 692
- 515
Good point Paskali. Tatizo waTZ wengi hawaoni hilo. Wao wanamuona Magufuli kama adui anayeleta njaa kumbe walisahau kile chakula walichokizoea kilipatikana kwa wizi, dhuluma, rushwa, nk. Yaani real estate ilikuwa na moto balaaa. Kila mwekezaji alikuwa akijenga high-end apartments, hotels, etc. Yaani walijisahau kabisa kwamba mtanzania wa kawaida ana kipato gani na watapata vipi hela yake. Walitegemea faida ya haraka haraka. Athari yake ilikuwa kila sehemu ya jiji la dar maana bei ya viwanja na nyumba za kupanga ilikuwa balaa. Tena hali ilikuwa mbaya zaidi kama unapata kipato cha kihalali maana ulikuwa huthaminiwi na wenye nyumba walikuwa wana jeuri. Sasa JPM anawafundisha Economics 101, somo la leo - whenever there is a market failure, the government has to intervene. Raisi wangu JPM, endelea na kazi. Kulikuwa na market failure kwenye real estate, ukipata muda rudi kwenye hii sekta, tukumbuke kwa kuweka sera bora za kujenga majengo ya kupanga na kuuza kwa bei nafuu, sio unafuu wa NHC enzi za JK.Kiukweli huku mtaani hali ni mbaya, ila Slim ni mwekezaji Mtanzania anayejua kujituma na yuko very well connected ila licha ya kuwa ni mtoto wa mjini ana bahati mbaya.
Ndiye yeye mtu wa kwanza kuleta lebo yake kwa pamba kali ile lebo ya Check Bob Maarifa, ikafa!.
Ndiye yeye aliyeuziwa ule uwanja wa wazi wa Anatoglo ili ajenge a modern park yenye a 5-Star Hotel, paperwork yote ililamilika, akapewa building permit ile kuzungusha tuu uzio aanze ujenzi, uzio ulivunjwa ikakutikana kulifanyika janja janja.
Kumbe ndio akaweza Bagamoyo.
Kama mradi wake umepitia TIC anaweza kufanyiwa assessment kuestablish the viability ya mradi huo, kama uko viable kusupport Tanzania ya Viwanda, anastahili kupatiwa Government Guarantee, kwa kuonyesha ulikwama kwa sababu za unpredictability ya serikali yetu. Atasikilizwa.
Ila kiukweli kuna wawekezaji watalia!. Mfano Wachina wa AVIC City Kingamboni, kama Peninsular Apartments za Masaki zimedoda hadi kupigwa mnada, what are the chances za AVIC City apartments zake za TZS 600,000,000 kuuza? . NSSF nadhani wameshituka mapema kabla ya kuendelea na Dege Eco Village yao.
Mimi sio mchumi ila lawama zote za kuporomoka kwa uchumi anatupiwa Magufuli, kwani Magufuli amefanya nini kinachodidimiza uchumi? . Kama ni mishahara ni ile ile, hakuna aliyepunguzwa mshahara, sasa huu ukata unatoka wapi?.
Au ni kweli baadhi ya investments ziliwategemea wapiga dili, hivi hao Watanzania wakununu nyumba Kigamboni kwa million 600,000,000 ni Watanzania wepi hao? .
NHC inajenga Seven 11 pale Kawe City, nimeelezwa the cheapest ni TZS 400,000,000 single room apartments, 600,000,000 double room na 800,000,000 kwa vyumba vitatu! . Ni kwa ajili ya Watanzania wepi hao?, labda wenzetu ma diaspora, vingenevyo hawa wenzangu na mimi tutabaki macho kodo!.
Paskali