GE2025 Agnesta Kaiza: Rais Mama Samia alisema mimi kama mwanamke lazima nimtue mwanamke wa kata ya Kisulu ndoo kichwani kwa kumpelekea maji

GE2025 Agnesta Kaiza: Rais Mama Samia alisema mimi kama mwanamke lazima nimtue mwanamke wa kata ya Kisulu ndoo kichwani kwa kumpelekea maji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia CHAUMMA, Agnesta Kaiza, ametambua changamoto kubwa zinazowakabili wakazi wa kata ya Kisukuru ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Akizungumza katika muendelezo wa kampeni zake, Agnesta amesema hali hiyo imekuwa ikiathiri maisha ya wakazi hao, hasa wakinamama wanaopata taabu kubwa wakati wa kwenda kujifungua kutokana na barabara kutopitika.

Soma pia: Agnesta Kaiza: Wananchi wa Segerea naombeni mnijaribu kwa miaka 5



Ameongeza kuwa ajali za bodaboda na bajaji zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kutokana na ubovu wa barabara za ndani ya kata hiyo.

Aidha, Agnesta ameelezea kutoridhishwa kwake na michango ya mara kwa mara inayotozwa kwa wazazi katika shule za msingi na sekondari, kinyume na sera ya Serikali kuwa elimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
 
Back
Top Bottom