Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,770
- 1,173
AGNES MATHEW MARWA AAPISHWA KUWA MBUNGE WA BUNGE LA 13
Dodoma – Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Agnes Mathew Marwa, ameapishwa rasmi leo tarehe 11 Novemba 2025 kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiapo hicho kimefanyika katika kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 13, kinachoendelea jijini Dodoma.
Agnes Marwa ni miongoni mwa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa na Chama chake na kuthibitishwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni.
Bunge hilo linaendelea na shughuli zake rasmi ambapo Wabunge wote walioteuliwa na kuchaguliwa wanatarajiwa kuapishwa kabla ya kuanza kwa shughuli za kawaida za kibunge.