Agizo la Waziri Mkuu laendelea Kupuuzwa !

The Fixer

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
1,365
583
Wadau,

Nadhani lile agizo la Waziri Mkuu kusitisha uchimbaji wa yale madini katika vyanzo vya mto kule Upareni katika milima ya Shengena kama lilivyowakilisha na Anne Kilango pamoja na vielelezo vingine kama ushahidi wa kile alichokuwa anakipinga na hata baada ya Waziri Mkuu kuridhishwa na hali halisi ya uharibifu wa mazingira.

Waziri Mkuu akiwa anafunga kikao cha Bunge la bajeti lililopita alipiga marufuku Uchimbaji na Usafirishaji wa madini hayo kutoka katika chanzo hicho na pia kampuni ya Willy Enterprises ya mjini Arusha ikihusishwa na sakati hili moja kwa moja ikiwa yenyewe ndio hutumika kama " mode of transport " kuusafirisha mchanga huo huko Mombasa
Picha hii ndio hayo malori ya Willy Enterprises yakiwa yamepaki yakisubiri vibali vya kuvuka mpaka wa Horohoro kwenda Mombasa ( yako matano )ili kuendelea na zoezi lao la kuupeleka huo mchanga wa madini ( inasemekana ni wa dhahabu pia )

Kitengo cha TRA wao wanaendelea kutoa vibali vya kuvusha na Wadau wa Usalama wa Taifa wapo na wanangalia tu.

Je Agizo la Waziri Mkuu lilikuwa ni kiini macho tu ? Mpaka lini Tanzania hali itaendelea !

Magari yameshaanza kuondoka muda huu moja baada ya jingine yanaelekea Lungalunga-Mombasa- Kenya
 

Attachments

  • IMG00081-20120922-0953.jpg
    IMG00081-20120922-0953.jpg
    7.6 KB · Views: 83
Mkuu nchi hii haina utamaduni wa kusikiliza au kutii hoja za viongozi kila mtu alipo ni mkubwa !
 
inawezekana kabisa kuwa ni yeye mwenyewe anachimba (one of those within the government)
 
Zile kauli za Bungeni eti, naagiza mara moja.........usitishwe, tumelisikia,nitakwenda mimi mwenyewe,na nyinginezo upuuzi mtupu
 
Nchi inauzwa sana jamani.... Watu wanaila sana hii nchi ! Haya malori hayajawahi kukoma kupita hapa, kwanini lakini.......mpaka lini ?
 
Mkuu nchi hii haina utamaduni wa kusikiliza au kutii hoja za viongozi kila mtu alipo ni mkubwa !

Huu ni mfumo ambao watawala wamewarithisha watanzania na wao wakaupokea kwa nguvu zote. So viongozi hawawezi na wasimlaumu mtu bali wajilaumu wenyewe.
Hainiingii akilini kwa kiongozi Mkuu wa nchi kupuuzwa kama hvyo. Anaempuuza ina maana kati ya ile mihimili yeye ana mhimili wake unao-operate independently.
 
Mkuu nchi hii haina utamaduni wa kusikiliza au kutii hoja za viongozi kila mtu alipo ni mkubwa !

viongozi wenyewe walishajita nguo. Ni waongo ndo maana hata wananchi hawafuati wanachokiongea kwani ni porojo tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom