Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,067
Agizo la Rais Magufuli kuwataka watumishi wa Muhimbili kuhama ofisi ndani ya siku mbili ili kuwaachia majengo wagonjwa waliokosa nafasi hospitalini hapo laanza kutekelezwa.
Rais alitoa agizo hilo alipoenda kumjulia hali Mufti mkuu wa Waislamu Tanzania, sheikh Abubakari Zuberi aliyelazwa hospitalini hapo na kukuta mazingira ya wagonjwa wa wodi ya wazazi yakiwa hayaridhishi, ambapo alikutana na malalamiko ya wakina mama waliomfuata na kumueleza kuwa wamekuwa wakilazwa hadi watano kitanda kimoja huku mazingira yakiwa machafu kutokana na maji kuchuruzika kutoka maliwatoni.
Ofisi hizo zilizokuwa zikitumika na watumishi wa wizara ya afya sasa imeagizwa zirejeshwe chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili walau kupunguza tatizo.
Habari na iwafikie..