Agenda ya CCM Igunga ni ipi hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agenda ya CCM Igunga ni ipi hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Aug 21, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika mazingira ambayo kila kiongozi ni gamba la kuvuliwa agenda ya chama cha mapinduzi Igunga ni nini hasa? Ni nani ataokota jiwe na kuanza kumponda Rostamu. Kimsingi wananchi wa Igunga wamesikia kutoka kwa Rostamu kwa nini hasa aliachia ngazi katika uongozi ndani ya ya CCM kwa kifupi na kwa maneno makali alisema sababu hasa ni "siasa uchwara". Wananchi wa Igunga wanayo haki ya kutaka kujua kutoka CCM kulikoni na kipenzi chao, mbunge wao na mfadhili wao? Kama hili halikujibiwa vizuri CCM imekwisha.


  Nasaema hivi kwa sababu agenda ya vyama kinzani katika jimbo la Igunga ni moja tu nayo ni "Ndiyo kweli Mbunge Rostamu alikuwa na tuhuma za ufisadi, lakini si kwa manufaa yake binafsi bali ilikuwa kwa manufaa ya mfumo wa chama katika uchaguzi wa 2005 na kwa hiyo leo hakustahili kushikiwa bango pekee yake na kufanywa kondoo wa kafara. CCM haiwezi kujitakasa kwa RA kuwa kafara, ni busara yake ndiyo imemtuma kujiondoa katika kuendesha siasa uchwara `ili asiathiri shughuli zake za kibiashara.


  Sikubaliani na hoja yoyote ya kumtetea RA lakini katika mazingira ya sasa ya siasa za Igunga anaweza kuwa asset or a liability to any political party. Ushauri kwa mameneja wa campain wa vyama vyote ni kama ifuatavyo; CCM avoid mentioning RA or talk very aggressively on issue to inform your voters. Opposition parties keep on punching for CCM to tell the truth over the story. Achaneni na hoja ya ufisadi hiyo waachieni ccm wamalizane wao kwa Igunga kwani ndiyo walioitumia kummaliza mwenzao. Kazi kwenu ni kuhakikisha wananchi wanawabana waizungumze hata pale ambapo hawaipendi kuizungumzia pia kila wakati warushieni makombora ili walazimike kutoa ufafanuzi ambao utawapa upenyo wa kuwashambulia strategically
   
Loading...