Katiba ya nchi inatoa haki sawa kwa Watanzania wote katika kuabudu, kufanya kazi, uhuru wa kuamua na kuchagua. Hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya tume ya ajira au mashirika ya serikali kubagua watu wa makundi fulani kutokana na Umri. Hii haina tofauti na ubaguzi wa kijinsia au wa rangi na kinyume na katiba ya nchi. Cha kushangaza asasi za kijamii, kisheria na kiraia zimekuwa kimya katika hili.
Ni wakati wa kulipigia kelele hili ili kutokomeza ubaguzi wa kila aina katika nchi yetu.
Mungu Ibariki Tanzania!
Ni wakati wa kulipigia kelele hili ili kutokomeza ubaguzi wa kila aina katika nchi yetu.
Mungu Ibariki Tanzania!