Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,577
- 19,457
Naibu katibu mkuu wizara ya kazi amesema tamko la katibu mkuu wa Shirikisho la vyama vya ushirika TUCTA kusema kwamba shirikisho hilo litatoa tamko lake kuhusu mgombea urais anayewafaa wafanyakazi, kuwa ni kinyume na seria na kanuni za serikali ya Tanzania, amedai kazi ya shirikisho hilo ni kutetea maslahi ya wafanyakazi na si kuingilia uhuru wao wa kuchagua viongozi wanaowataka.
Na vilevile amedai wafanyakazi wameongezewa mishahara yao na kodi kwenye misharaha yao imepunguzwa.
My Take:
Kama wewe ni mbayuwayu, changanya na ya kwako.
Kwa wale waliosoma hadithi za Esopo watakumbuka hadithi hii:
Baharia mmoja aliyekuwa akienda safari ndefu baharini alichukua nyani mmoja (siyo NGABU lakini- teh! teh!) kwenye meli yake kusudi awe anamchekesha wakati wa safari ile. Baadaye kidogo baada ya kuanza safari yake kutoka bandarini kwenye pwani ya ugiriki, hali ya hewa ilibadilika ghafla na kusababisha mawimbi wakubwa yaliyopasua meli yake na kuwaacha yeye mwenyewe, nyani wake na mabaharia wengine kupambana kuoegelea majini ili wasalimishe maisha yao.
Samaki mmoja aina ya pomboo (dolphin) akamwona yule nyani akishindana na mawimbi, ila kwa vile samaki hao wana tabia ya kuwasadia binadamu wanapokuwa kwenye dhahama kama ile, basi akaja kumbeba nyani yule mgongoni mwake akidhani kuwa ni binadamu.
Baada ya pomboo yule kuogelea kwa muda mrefau kutoka maji merfu hadi karibu na ufukweni akamwuliza nyani yule kama yeye alikuwa ni mtu wa Athens (mji mkuu wa Ugiriki). Yule nyani akajibu kuwa ndiyo alikuwa mwenyeji wa Athens na alikuwa mzaliwa wa familia bora zaidi katika mji huo. Baadaye pomboo akamuwliza tena nyani kama alikuwa anaifahamu bandari maarufu ya Piraeus. Nyani akajibu, ndiyo namfahamau sana huyo mtu na kwamba alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana. Pomboo yule kusikia hivyo akakasirika na kumtosa nyani yule majini baada ya kugundua kuwa alikuwa anajipendekeza na kusema uwongo na....
Tumewabeba viongozi wetu hawa kuwatoa maji marefu hadi kuwafikisha karibu na ufukweni lakini wao hawaishi kujipendekza na kutuaambia uwongo kama vile hatustahili kuheshimiwa; inabidi tuwatose. Viongozi wote hawa leo ni matajiri wa kutupwa kutokana na sisi kuwabeba migongoni mwetu kwa muda mrefu sana. walitususia na kututishia lakini sasa ndio wanatambua umuhimu wa kura zetu na kuanza kujikomba kwetu na kutuambia uwongo. Watoswe kabisa hao