Afya za wana Appolo zinaendeleaje ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afya za wana Appolo zinaendeleaje ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanang'walu, Oct 16, 2011.

 1. N

  Ng'wanang'walu Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana JF, ni matumaini yangu makubwa muwenye afya njema , poleni kwa wale afya si njema sana Mungu awabariki napate kurudia afya zenu ilituweze kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo la nchi yetu.

  siku chache zilizo pita tukio la kuugua huyunaibu wazili wa ujenzi na kupelekwa huko India kwa uchunguzi na matibabu zaidi, lakini mpaka sasa hivi mpaka sasa kama kuna anaye jua hali ya kiongozi wetu kuwa anaendeleaje?

  Tukio hili kwanza binafisi limekuwa ni Gumuzo kilapande ya nchi hii ni nanma gani watanzania walivyo guswa na hili jambo, ninachokiona hapa iwapo kama kweli itathibitika yakuwa kweli alilishwa sumu, nchi na genge hilo ndani ya chama itakuwa katika wakati ngumu sana, kwamba sasa chama hiki cha ccm ndo mwisho wake, kinasambaratika kama ukomuniisti huko ulaya ya mashariki ulivyo sambaratika ndani ya mikono ya Michael Grobacho akiwa moja ya viongozi waliokuwa wamepandikizwa na maadui zao wa magharibi, nachelea kuuliza hawa jamaa nao nani kawatuma? Na kwa misingi ipi na kwafaida ya nani?

  Tukio la kuugua Mwandosya hadi kupelekwa India halikusikika zaidi kama la Mwakwembe, na iliripotiwa kuwa ana ugonjwa kama wa hayati JK. Nyerere, watu tukakosa imani ya afya ya huyu mzee, na pengine kwenda mbali labda ndo magonjwa ya viongozi wetu, viongozi hapa nchini wenye mapenzi ya nchi ndo wanao onekana yakuwa wanapigwa vita kali na kundi la waporaji wa rasilimali za nchi hii wengine waliwahi hata kuzuiwa kugombea nafasi ya Urasi wa nchi hii na Muasisi wa nchi hii.

  Na sasa ndo tunawaona ndo vinara wa mbinu chafu za kuondoa roho za wapigania haki katika taifa hili changa, nafika mbali zaidi katika kuwaza yakuwa kama walizuiwa kuwa hawafai kushika madaraka kama hayo na wakaona huyo ndo kikwazo kwao inawezekana mbinu hizo hizo wanazo zitumia kwa sasa kutaka kuwa toa roho wanao onekana ni kwazo kwao pia waliwahi tumia mbinu hizo hizo nawakafanikiwa kuingia madrakani kwa ulaini naakuanza kula mema ya nchi, nasasa wamejitokeza tena wanaowapinga hivyo wanaendeleza kamchezo kao hako kakinyama bila kujari mstakabali wa maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

  Hivyo basi naomba waumini wa dini zote kuiombea nchi hii watu hawa wenyeroho mbaya na nchi hii wasipate nafasi ya kushika madaraka tena na wananchi waamuke nakutowapigia kura tena.

  Nawasilisha.
   
 2. M

  MINAZI Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka hii hali ya sasa ya nchi hii inatisha sana,ni mkono wa Mungu tu ndio unaotupigania.Naamini wana Appolo Mungu atawaponya tu,kwani mwenye haki ataishi kwa haki yake na dhalimu ataishi kwa udhalimu wake.Tupo pamoja katika maombi kwa ajili ya wanaappolo.
   
Loading...