Afya za mawaziri watano ni tete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afya za mawaziri watano ni tete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 16, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  WAWILI WAENDA INDIA KIMYAKIMYA, DK CHAMI AWA MBOGO, ASEMA WANAOSUBIRI KUONA WENZAO KWENYE MASANDUKU WATASUBIRI SANA
  Waandishi wetu
  WAKATI tetesi za kupanguliwa Baraza la Mawaziri zikizidi kupamba moto, hali ya afya ya baadhi ya mawaziri imeelezwa kuwa tete hivyo kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.Miongoni mwa Mawaziri hao ni wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami ambaye jana aliibuka na kuwataka watu aliowaita wanye uchu wa kuchukua nafasi yake, waache mara moja kutumia afya yake kupiga propaganda chafu za kisiasa.

  Hadi sasa, mawaziri ambao taarifa za kuugua kwao zinafahamika ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya mwenye dhamana ya Maji, Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Chami. Wengine ambao taarifa zinaonyesha kuwa walikuwa nje ya nchi kwa matibabu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.

  Ingawa haijafahamika maradhi yanayowasumbua hadi sasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakichukulia hali ya afya ya baadhi yao kama moja ya sababu inayoweza kuwafanya wawekwe kando pale Rais Jakaya Kikwete atakapoamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kuwapa fursa ya kupumzika na kuendelea na matibabu.
  Dk Chami

  Dk Chami alisema jana kwamba tangu arejee kutoka India alikokwenda kutibiwa, afya yake imeimarika na hakuna siku aliyoshindwa kutekeleza majukumu yake huku akisema wanaoeneza uvumi huo ni mahasimu wake kisiasa wanaonyemelea nafasi yake.

  Alisema mbali ya kufika ofisini kwake kila siku, alishiriki kikamilifu kwenye Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliomalizika hivi karibuni Mjini Dodoma na kujibu hoja mbalimbali zilizoelekezwa kwa wizara yake.
  Aliwalinganisha maadui zake kisiasa na fisi mwenye uchu anayemfuatilia mtu kwa nyuma bila kujali umbali wa safari kwa matumaini ya kuneemeka mkono ukidondoka huku akisema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri wake kwa vigezo anavyoona vinafaa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

  “Nashangaa sana, afya yangu ni njema, imeimarika. Tangu nimerejea kutoka India, sijawahi kwenda hospitali wala zahanati yoyote, naingia ofisini kila siku kuanzia asubuhi na kutoka jioni, nimehudhuria Mkutano wa Bunge, Dodoma na leo nina kazi ya kutembelea viwanda, sasa huku ndiko afya yangu kuzidi kudorora?,” alihoji Dk Chami na kuongeza:
  “Suala kubwa hapa ni uwaziri, lakini mtu unaposema fulani anaumwa sana au haumwi lazima usimame katika ukweli.
  Hizi ni propaganda chafu za kisiasa zinazoenezwa na baadhi ya watu wenye uchu wa kutaka nafasi hii. Rais ana mamlaka yake ya kuteua mtu kwa vigezo anavyoona vinafaa na mamlaka hiyo haitegemei afya ya mtu. Anaweza kuwa mzima au mgonjwa lakini anateua kwa kadri itakavyompendeza yeye.”

  Dk Chami aliwataka wananchi wa jimbo lake la Moshi Vijijini kutokuwa na hofu kuhusu afya yake akisema imeimarika na amejipanga kuongoza mapambano ya kuleta maendeleo.

  Chami alirejea nchini mwishoni mwa mwaka jana kutoka India alikotibiwa kwa miezi miwili akiwashukuru Watanzania kwa moyo wa upendo walioonyesha kwake kwa baadhi yao kufunga na kufanya mikesha, kumuombea ili apone.

  Kinachomsibu
  Akizungumzia ugonjwa uliompeleka India, Waziri huyo alisema alikuwa akisumbuliwa na maumivu upande wa kulia wa kifua chake na alipofika India, ilibidi madaktari wamkate kipande cha nyama na kukisindika ili kutambua bakteria husika baada ya awali, kushindwa kuwabaini.

  Alisema wakati akiendelea na tiba hiyo, dawa alizokuwa akizitumia zilimletea athari, iliyosababisha mwili kuvimba. Alisema kifua kilipata ahueni mapema na muda mrefu ulitumika kutibu uvimbe aliopata.
  Akiwa katika ziara kutembelea kiwanda cha MMI Steel, Dk Chami alitumia fursa hiyo kuelezea pia afya yake akitamba yupo 'fiti' na hana mgogoro wa kiafya kama baadhi ya watu wanavyojaribu kumshinikiza Rais Kikwete afanye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

  “Nipo vizuri sana na uzito umeongezeka kwa kilo 15. Sasa wale ambao wanafikiria kuwaona wengine katika masanduku (majeneza) watasubiri sana” alisema.

  Kombani na Chikawe
  WaziriKombani alipelekwa nje ya nchi kutibiwa na sasa amerejea nchini. Awali, taarifa zilisema alipaswa kwenda kufanyiwa upasuaji ambao hata hivyo, haukuwekwa wazi.
  Waziri huyo hakuonekana katika Mkutano wa Sita wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema ndiye aliyekuwa akijibu maswali ya Wizara Katiba na Sheria.

  Jana, taarifa zilizopatikana wizarani kwake zilisema Kombani hajaonekana ofisini kwa takribani wiki tatu.
  Baadhi ya vigogo wa wizara hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, walisema waziri huyo hayupo ofisini kutokana na kuumwa na kwamba alikuwa nje ya nchi wa matibabu kwa takriban wiki tatu.

  Msemaji wa wizara hiyo, Omega Ng’ole alisema hajui kama Waziri Kombani alikuwa anaumwa huku akisema waziri kwenda nje au kutokwenda kwa ajili ya matibabu ni suala binafsi hivyo kushauri atafutwe mwenyewe.

  Akizungumza kwa simu, kuhusu afya yake Kombani alihoji: “Unataka kufahamu kama mwandishi au ndugu?” baada ya kujibiwa alisema si jambo baya kwa kiongozi kwenda au kupelekwa nje ya nchi kutibiwa.

  “Hivi mtu kuumwa ni jambo la kutangaza kweli… nini cha kushangaza kama mtu akiumwa?,” alihoji.

  Alisisitiza kwamba, hakuna ubaya kwa kiongozi yoyote kwenda nje ya nchi kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

  “Mtu akienda nje kufanyiwa uchunguzi hiyo nayo ni habari? Hilo jambo kwangu ni mambo madogo tu, hiyo siyo habari bwana,” alisema Kombani na kuongeza kuwa hawezi kusema kama ni mgonjwa au la kwa kuwa hilo ni jambo lake binafsi... “Mimi nakwenda nje kila siku, kila wakati katika shughuli zangu za kikazi na hata siku moja sijawahi kuulizwa na mtu.”

  Kwa upande wake, Waziri Chikawe naye anadaiwa kwamba hivi karibuni alikwenda India kupata matibabu. Hata hivyo, haikuelezwa kinachomsibu kutokana na usiri mkubwa uliopo serikalini juu ya matibabu ya viongozi hao.

  Dk Mwakyembe
  Dk Mwakyembe ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi na kupelekwa India Oktoba 9 mwaka jana, anatarajiwa kwenda tena nchini humo wakati wowote kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.

  Mmoja wa watu wa karibu na Dk Mwakyembe alisema juzi kwamba Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anatarajiwa kurudi katika Hospitali ya Appolo kwa ajili ya kuangalia kama matibabu aliyopata yamemsaidia kwa kiwango gani.

  Ingawa Dk Mwakyembe alijitokeza hadharani katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe hivi karibuni, hali ya afya yake haikuwa ya kuridhisha kutokana na ngozi yake kuonekana imeathirika.

  Profesa Mwandosya
  Profesa Mwandosya ambaye amekuwa akitajwa kama mmoja wa makada wa CCM ambao wangeweza kuwa tishio katika mbio za urais ndani ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Appolo kwa zaidi ya miezi mitatu. Sasa hivi, Waziri Mwandosya nchini India ambako anaendelea kupata matibabu.

  Ikulu
  Kuhusu taarifa za kuwepo kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Kurugenzi ya Mawasiliano imesema wajibu wa kubadilisha baraza hilo uko kwa Rais ikiwa ataona kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana jioni alipokuwa akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds FM na kusisitiza: “Rais atakapoamua kufanya hivyo atafanya kwa matakwa yake mwenyewe.”

  Habari hii imeandikwa na Joseph Zablon, Keneth Goliama, Fidelis Butahe na Boniface Meena.
  :A S 465:
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Cyril asubiri fagio la chuma la JK
  Kasikia kwamba mjomba anapangua baraza ikabidi aonge TV wampe promo!!
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Waendelee ktmalizana tu wenyewe neema itatujia waTz kupitia migongo yao
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  "Nashangaa sana, afya yangu ni njema, imeimarika. Tangu nimerejea kutoka India, sijawahi kwenda hospitali wala zahanati yoyote, naingia ofisini kila siku kuanzia asubuhi na kutoka jioni, nimehudhuria Mkutano wa Bunge, Dodoma na leo nina kazi ya kutembelea viwanda, sasa huku ndiko afya yangu kuzidi kudorora?," alihoji Dk Chami na kuongeza:
  "Suala kubwa hapa ni uwaziri, lakini mtu unaposema fulani anaumwa sana au haumwi lazima usimame katika ukweli.
  Hizi ni propaganda chafu za kisiasa zinazoenezwa na baadhi ya watu wenye uchu wa kutaka nafasi hii. Rais ana mamlaka yake ya kuteua mtu kwa vigezo anavyoona vinafaa na mamlaka hiyo haitegemei afya ya mtu. Anaweza kuwa mzima au mgonjwa lakini anateua kwa kadri itakavyompendeza yeye."
   
 5. N

  Ntuya Senior Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Madaraka matamu sana
   
 6. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nawapa pole sana, lakini uwaziri umewabeba sana, wangeuguzwa kwenye hizi hospitali zetu za rufaa tusingekuwa nao duniani.
   
 7. jameeyla

  jameeyla Senior Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  its time Rais sasa aangalie wachapa kazi na si kujaza baraza ambalo halina watendaji, hawa wanaoumwa kweli hata akiumwa mwaka hivi hizo kazi zake nani anazifanya kama si kurudisha maendeleo nyuma??hatuombei watu waachishwe kwa afya mbofumbofu bali tuangalie je maendeleo ya wizara hizo yakoje na maamuzi yatakayoleta ufanisi kwa nchi yafanywe..
   
 8. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Mfa maji haachi kutapatapa, mbaya zaidi yuko kina kirefu.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Siasa ina wenye afya mgogoro wa kutosha na wengine choka mbaya afya mgogoro pengine umri umechangia ingawa wanaonekana katika shughuli za kila siku. Tunahitaji maelezo ni nini kinawasumbua.


  Zitto Kabwe - alikwenda India.
  Ibrahim Lipumba - alifuatana na Mwandosya India.
  John Cheyo - Afya mgogoro
  Philemon Ndesambulo - Afya mgogoro
  Bob Makani - Afya mgogoro
  Edwani Mtei - Afya mgogoro
  Augustine Mrema - alipelekwa India.
  Anna senkoro Mvungi - Afya mgogoro
   
 10. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chami asimtafute mchawi, wanaosubiri nafasi zao ni watoto wao, maana ndio hao wakifa baba zao wanachukua fomu kugombea
   
 11. Aaronium

  Aaronium Senior Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye RED;Umaskini na dharau kwa walala hoi hazitakwisha kamwe, na ninyi wapiga kura msiyeona haya mnastahili kunyan'ganywa haki na kwanza HAMNA HAKI YA KUCHAGUA VIONGOZI kama watachaguliwa wanaofurahia kuzurura nje ya nchi ati kwa shughuli zao huku watu wanakosa mishahara, na kutibiwa kwao nje ndo kunawafanya wawadharau madaktari hata kama maisha ya walalahoi ambao daima huwachagua yapotee kwa kutokutambua kwao.Anafikiria kuandika imprest tu na kunyonya hii nchi mpaka ifirisike na tone la mwisho alione! ANGALIENI HAYA NINYI WAPIGA KURA MASIKINI WA KILA KITU!
   
 12. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini rais akiamua kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa sababu ya afya za mgogoro, atawapata wapi wa kuziba hizo nafasi maana wote wagonjwa!!!!!!! Si mliwaona walivyokuwa wanapigana vikumbo kule Loliondo kwa babu?
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyu na upstairs patupu-sasa kuongezeka kilo 15 ndo afya? Kama jk ilikuwa ambakize kwenye baraza sasa basi
   
 14. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kikwete anapenda kufanya kazi na wagonjwa
   
 15. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nao ni binadamu kama wewe na mimi!
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  JK ameanza vizuri anaweza kukubaliana na Chadema ili awape uwaziri Slaa, Zitto, Mbowe, Lissu, Mnyika na Mdee kabla ya 2015. hapo anaweza kuinusuru CCM isianguke chali 2015. Tatizo la CUF wanaendekeza Udini na Uzanzibari ebu angalia mambo ya Jussa, Hamad Rashid ni Popo (kigeugeu).
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Tuwaombee viongozi wetu wagonjwa ili wapone, mara nyingine watu wanatambua uwepo wa Kristu ambaye ni Bwana na Mwokozi katika wakati mgumu kama walio nao sasa hivyo huenda wakipona wataacha unafiki, ufisadi, wizi, kujikomba kwa kikwete badala ya kujikomba kwa wananchi waliowachagua.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wengi walishakunywa kikombe cha babu. Hakika nawaambia Tanzania ina wagonjwa wengi kuliko mnavyofikiri. Tukumbushane Viongozi walioenda kwa Babu Liliondo kisha muangalie siha zao; migogoro mitupu.
   
Loading...