Afya ya Ndesamburo yazua utata

Afya ya Ndesamburo yazua utata

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,919
Reaction score
166,168
UTATA umegubika afya ya Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo huku taarifa zikidai kuwa anaumwa na anapatiwa matibabu nchini Uingereza.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Ndesamburo, Waziri wa zamani wa Elimu, Jackson Makwetta inaelezwa kuwa hali yake ni mbaya.

Ndugu wa karibu wa mbunge huyo wa zamani wa Njombe Kaskazini aliyekataa kutaja jina lake gazetini, alisema Makweta alianza kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu jambo lililosababisha kulazwa katika Hospitali ya Consolata Ikonda iliyopo Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa.

"Hali yake ilianza kubadilika juzi akiwa hospitalini na kulazimika kumhamishia jijini Dar es Salaam ambapo alikodiwa ndege maalumu kwa ajili ya kwenda kupata matibabu zaidi," alisema.

Makwetta aliyetumikia Jimbo la Njombe Kaskazini tangu 1975 hadi 2010 kabla ya kustaafu, alishika nyadhifa mbalimbali ikiwamo Waziri wa Elimu.

Ndesamburo adaiwa kufanyiwa upasuaji

Taarifa zilizozagaa mjini Moshi zinadai Ndesamburo alifanyiwa upasuaji nchini Uingereza na anaendelea vizuri, lakini taarifa nyingine zikidai hajafanyiwa upasuaji bali anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Ndesamburo hajaonekana katika medani za kisiasa kwa takriban mwezi mmoja sasa na hata kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kilema Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini na Nanjara Reha wilayani Rombo hakushiriki.

Mbali na kutoshiriki katika kampeni hizo, mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, hakuhudhuria vikao vya Bunge vilivyomalizika Ijumaa kutokana na kuwapo kwake nje ya nchi.

Habari zisizo rasmi zilizopatikana jana zilidai hata mtoto wa Mbunge huyo, Lucy Owenya aliondoka nchini hivi karibuni kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kumuuguza baba yake na bado yuko nchini humo.

Habari zilizomkariri mmoja wa ndugu wa karibu wa familia ya Ndesamburo zilidai mbunge huyo ni mgonjwa, lakini kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kutibiwa Uingereza.

"Ni kweli mzee anaumwa, lakini sasa hivi anaendelea vizuri, huo uvumi kuwa hali yake ni mbaya sijui unaanzia wapi,"alisema mwanafamilia huyo aliyekataa jina lake lisitajwe.

Hata hivyo, Owenya ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema alipoulizwa kwa simu na gazeti hili juzi kutoka nchini Uingereza alikanusha baba yake kuugua.

"Nini? Eti unasema?" aliuliza Owenya kwenye simu na baada ya kuelezwa kuna taarifa zimezagaa baba yake ni mgonjwa alijibu kwa kifupi, "Hakuna kitu kama hicho."

Habari zaidi zilidai kuwa mbunge huyo anatarajiwa kurejea nchini leo na yuko salama tofauti na taarifa zilizozagaa jimboni kwake kuwa ni mgonjwa.

Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde alisema kuwa ni kweli Ndesamburo anaumwa na yuko nchini Uingereza kwa matibabu.

"Ni kweli yuko Uingereza anaumwa na anaendelea na matibabu ila anaendelea vizuri."

Silinde ambaye pia ni mbunge wa Mbozi Magharibi alisema, Ndesamburo alikuwa nchini Uingereza kwa mapumziko na kuumwa kwake kulitokea huko huko na si kwamba alikwenda kwa matibabu.

"Alikuwa Uingereza kwenye mapumziko na huko huko hali ya ugonjwa ikamtokea," alisema Silinde na kuongeza: "Nitafuatilia nijue anarudi lini kwa kuwa sasa hivi sina taarifa kamili za kurudi kwake."

Na Daniel Mjema, Moshi na Boniface Meena, Dar | Mwananchi | Novemba 13 2012
 
kuna mawaziri wanaenda south africa wengine UK wengine germany wengine india...kwanini wasichague moja kama ni uk tujue uk au kila tunda na mti wake sio
 
Tanzania haina karakana ya Afya kwa ajili ya afya za "viongozi"?

Hata karakana kuu ya Muhimbili (hospitali ya rufaa, hospitali kuu) haifai kwa ajili ya afya za hawa wala kodi za walalahoi?
 
Get well soon babu Ndesamburo a.k.a NdesaPesa!
 
hii habari hata nimeshindwa kutoka na moja lililo concrete mara hivi mara huyu kakanusha mara habari za uhakika nini maana yake!!huu siyo uandishi mzuri!! mother
 
Ndesamburo,Makweta,Mangula hizi habari zina uhusiano gani kwa sasa?
 
huyo mwandishi kama mulugo tu, akajipange ili aeleweke,
sasa hapa anatupatoa stori km za kijiwe cha kahawa.
 
mwandishi wa shule zetu za kata nini mbona haeleweki!
ni wa gazeti gani huyu!:confused2:
 
get-well-soon-purple-graphic-for-orkut.gif
 
Lucy Owenya siyo mwanae ila ni mke wa mwanae hivyo kwake ni Baba mkwe
 
Lucy Owenya siyo mwanae ila ni mke wa mwanae hivyo kwake ni Baba mkwe

vitu vingine kama hujui kaa kimya .... Lucy ni mtoto wa kike wa Mzee Ndesamburo ameolewa na Dr. Owenya ... aliyeolewa na mtoto wa Ndesamburo anayeitwa Sindato ni Grace Kiwelu mbunge
 
Tunamtakia kila la Kheri Mh kamanda Ndesamburo, Mungu amjalie apone haraka arudi kwenye mapambano Na afya njema
 
Back
Top Bottom