wakuu salaam!
naomba kufahamishwa,mimi ninajua kuwa afya ya mgonjwa ni siri ya mgonjwa na Daktari wake!kama ndivyo,je na halali kwa watanzania kutaka kujua hali ya afya ya rais wao!au hiyo ni siri yake na daktari wake?
Kwanza kabisa napenda nikuhakikishie kuwa suala la afya ni siri kati ya mtu na daktari, hadi pale kutakapokuwepo na 'consent' miongoni mwao.
Lakini pia uelewe kuwa kuna kiwango cha umaarufu au hadhi '' fame /celebrity status'' ambacho mhusika anapoteza baadhi ya hifadhi zake ''private life' si kwa kupenda bali kutokana na mazingira. Pia ukumbuke kuwa ni jamii kwa wakati fulani inalipia gharama zinazoambatana na umaarufu au hadhi. Kwa mfano Rais analipiwa matibabu popote atakapo tena kwa maisha yake yote hata akistaafu. Ni kutokana na haki hizi Rais huyo huyo anapoteza ''privacy' yake. Raia watakuja juu sana kama wakisikia Rais wao ametibiwa Uwanja wa fisi na drip fake, na ndiyo hiyo hali inaoyondoa privacy yake kidogo kidogo.
Rais au viongozi ni watu wenye siri na mambo mengi yanayohusu usalama wa taifa. Kunapotokea jambo ambalo linazua hofu na mashaka kuhusu afya yake basi taifa linapatwa na kihoro. Mfano Rais Bush[baba] alipoanguka katika state banquet kule Japan, siku iliyofuata masoko yalipoteza thamani kwa kihoro. Hata sasa hivi kutokana na uchaguzi usiokamilika kule Australia masoko ya ndani na nje yanayumba kwa kutojua hatima ya PM ajaye. Hii nataka nikuonyeshe kidogo umuhimu wa viongozi kitaifa. Ili kuondoa sintofahamu na taharuki kuna wakati Rais analazimika kupotea ''privacy' yake kwa ajili ya Taifa, na hapa ndipo siri inapokuwa si siri tena.
Mwisho, kumbuka kuwa bado kiongozi au mtu maarufu anabaki kuwa na haki ya kutotaja tatizo, ila akasema anaumwa inatosha. Itakapotokea kwa kiongozi kama Rais wananchi wanaweza ambiwa kuwa kiongozi huyo hawezi au anaweza kuendelea na kazi kulingana na afya yake, lakini inakuwa imekwenda mbali sana kama umma unataka kujua anaumwa nini. Kwahiyo suala la privacy katika fame au celebrity status ni ngumu sana ku maintain hasa zama hizi za majarida ya udaku na upaparazi.
Kwa kiwango wananchi wanalipia kodi kwa ajili ya maisha mazuri yenye furaha ya viongozi na familia zao, basi viongozi hao hao wanawajibu kwa wananchi, na moja ya hilo ni kupoteza hata sehemu ya uhuru wao '' private life''. Jibu la swali lako lipo katika Logics zaidi kuliko YES or NO.