Afya ya akili yako

Nov 2, 2020
68
90
Habari Wakuu,

Akili ni rasilimali muhimu katika kufanikisha shughuli za maisha yako ya kila siku.

Zingatia nini unasikiliza, Wapi, toka kwanani na muda gani.

Wataalam wanashauri kuwa si vema kulala ilihali umesoma au kuangalia picha, au tamthilia zenye kuogofya kwani kile cha mwisho kutazama, ndio ambacho ubongo unalala nacho, usije shangaa kikakuchosha Usiku kucha kwa kuogofya hata mwenyewe kitandani.

Vivyo hivyo udamkapo asubuhi, usianze na jambo ambalo litaishughulisha Akili yako ndivo sivyo. Mfano kuanza kwa kushika simu yako na Kupitia ujumbe wa maandishi au hata simu zilizopigwa ulipolala. Au wengine uamka na mitandao ya kijamii. Ukikutana na habari mbaya, ndivo hivo siku yako yote itakua mbaya hadi jioni.

Anza Asubuhi yako kwa maombi kwa Muumba wako kadiri ya Imani,Fanya mazoezi, zungumza maneno ya kujenga na mwenzi wako,Au hata kwa kuwabusu na kuwaombea watoto wako.

Kumbuka siku zote wewe ni zao la unachofikiria.

Linda Afya ya Akili yako.
 
Back
Top Bottom